Friday, February 28, 2014

Sisi ndo makamanda bwana! Cheki picha za yanayoendela kampeni za ubunge jimbo la Kalenga.

 Mwigulu (4th) na mgombea wakitroti na Green Guard, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Katibu wa CCM, wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu, alionyesha mbao zenye misumari inayodaiwa kutegwa njiani na Chadema, kwa nia ya kudhuru msafara wa mgombea wa CCM ktk jimbo la Kalenga. 
 Wananchi wakinyoosha mikono kuunga mkono kuwa mgombea wa CCM anafaa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.

Abdul Adam, Mtoto wa Spika wa Bunge wa zamani Chifu Adamu Sapi Mkwawa, akimpongeza mgombea wa CCM katika Uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Godfrey Mgimwa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.


 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba akionyesha makada wa CCM,  Alphonce John (kushoto) na Musa Tesha, walionusurika kuuawa na watu wanaodaiwa kutumwa na Chadema kwa mmoja kumwagiwa tindikali na mwingine kutobolewa jicho kwenye kampeni zinazohusu udiwani na Ubunge, katika maeneo ya Igunga na Kahama, alipokuwa akieleza fuji za Chadema, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.

  Alfonce aliyetobolewa jicho Kahama akizungumza jukwaani.
  Mwigulu akihutubia, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.



 Katibu wa CCM  mkoa wa Iringa, akishauriana jambo na Mwenyekiti wake Joyce Msavatavangu
 Mjumbe Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana,  akitema cheche jukwaani, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
Godfrey Mgimwa-Mgombea wa CCM uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa
habari kamili :: read more...

Kazi imeanza huko Uganda baada ya kusainiwa ile sheria. World Bank wazuia dola million 90 za msaada.

Benki ya dunia imebana msaada wa dola milioni 90 kwa Uganda , siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kuishinisha sheriua mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.

Benki hiyo imesema kuwa inataka kufanya tathmini yake kuhakikisha kuwa malengo yake ya maendeleo nchini Uganda katika sekta ya afya, ambayo msaada huo ulikuwa unanuiwa, hayataathirika .
Sheria iliyoidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Wafadhili wengine tayari wameanza kusitisha misaada Uganda. Wahisani kama Denmark na Norway wamesema kuwa wataanza kufadhili mashirika moja kwa moja badala ya serikali.

Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.

Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola.

Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.

Hadi kufikia sasa Waziri wa Fedha Wa Sweden, akiwa mjini Kampala, alisema waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na wakati mgumu kuweka pesa zao nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa sheria yo yote inaweza kupitishwa kuwadhulumu watu.

Jana serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa muda misaada kwa Serikali ya Uganda. Norway na Denmark pia zimetangaza kupunguza au kusimamisha kwa muda misaada yake kwa Uganda.
habari kamili :: read more...

Nililazimika kukeketwa ili nisomeshwe; Wazazi hivi kwa nini hamtaki kubadilika????


ESTER CHARLES (16) ambaye anasoma kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Rebu iliyoko wilayani Tarime mkoani Mara, alishindwa kujizuia na kudondosha machozi katika ukumbi wa kantini ya jeshi la polisi wilayani Tarime baada ya kueleza masaibu aliyokumbana nayo kwa kufanyiwa ukeketaji na wazazi wake.Anapofanyiwa ukeketaji huaminika kuwa mwanamke kamili aliyeondolewa mkosi na ambaye anastahili kuolewa. Wakati anafanyiwa ukatili huo, Esta alikuwa anasoma darasa la saba katika shule ya msingi Rebu, ambapo mara baada ya kukeketwa, anasema alipata maumivu makali ikiwa ni pamoja na kutokwa na damu nyingi.Anasema alikubali kufanyiwa ukeketaji na wazazi wake baada ya kufaulu mtihani wa darasa la saba na alikuwa na hamu ya kuendelea na masomo, lakini akapewa masharti na wazazi wake kuwa ili aendelee na masomo lazima akeketwe.
“Sikuwa na jinsi, nilijua ningeenda kukumbana na maumivu makali na kwasababu nilikuwa napenda  shule ilinibidi kukeketwa” anaeleza.
Kutoka maktaba ni moja ya nyenzo za ukeketaji.
UKEKETAJI UNAFANYIKAJE?
Anasema aliamshwa saa 11:30 alfajiri akiongozana na mama yake na wanawake wengine watatu alikwenda kuungana na wasichana wenzake waliokuwa kwenye orodha ya kufanyiwa ukeketaji na kupelekwa mtoni kuogeshwa!

Tuliogeshwa na kupewa maneno ya ujasiri ili tusilie wakati wa kukeketwa “ anasema na kuongeza kuwa Ngariba alilipwa kiasi cha Sh. 10,000/= kwa kila msichana aliyekeketwa (kwa wakati huo). Esta anasema kuna eneo maalum lililotengwa kwaajili ya shughuli hiyo na msichana hushikwa mikono yake kwa nyuma na mama aliyekeketwa.

“Baada ya kufika eneo lile, tulitangaziwa na ngariba kuwa kila mmoja awe na wembe wake, ambao ndiyo alitumia kukeketa” anasema.

Anachokumbuka siku hiyo ni kujikuta tayari amekwisha keketwa huku akitokwa na damu nyingi na maumivu makali. Anasema baada ya kukeketwa, wasichana wote waliwekwa katika uangalizi wa akina mama wasaidizi wakiwemo baadhi ya ngariba, huku wakiwapatia dawa za kienyeji wale wanaovuja damu iliisiedelee kuvuja.

“Nilishindwa kula, nilikunywa uji tu, siku ya pili nilipata maumivu makali baada ya kuamshwa asubuhi kwenda kuogeshwa” anaeleza.

Wakisikiliza kwa makini ni washiriki wa Kongamano hilo lililokuwa mahususi kwa ajili ya kuibua changamoto zilizopo katika jamii kuhusu suala la ukeketaji
Anasema msichana anapotoka jandoni inambidi ashiriki tendo la ndoa na mwanaume ambaye amefanyiwa tohara kama ishara ya kukubali kuwa binti aliyekeketwa kuwa mwanamke kamili na anayestahili kuolewa. Msichana aliyekeketwa huitwa ‘Omonke’.

Anaiomba serikali, asasi za kiraia na waandishi wa habari kutoa elimu ya madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike, na kwa ngariba wapewe elimu ya kutosha dhidi ya madhara ya ukeketaji.

“Wengi huku Tarime wanafanya hivyo, wakijivunia kukeketwa kutekeleza mila lakini pia ngariba bado hawajapata elimu ya madhara ya ukeketaji, naiomba serikalia na wadau wengine watoe elimu zaidi juu ya madhara ya ukeketaji” anasema na kuongeza kuwa jamii yao huamini kuwa wakimkeketa motto wa kike huleta Baraka katika familia.

NI MADHARA GANI ALIYOKUMBANA NAYO?
Anasema baada ya kukeketwa aliumia sana na aliathirika kisaikolojia ikiwemo kuzomewa nna wasichana wa rika yake ambao hawakuwa tayari kukeketwa.

“Siku niliyokeketwa, nilipata shida sana, nilikuwa na hofu hata wenzangu walikuwa wakinicheka, hata nilipopona nilichukua muda kurudi shule, niliathirika sana” anasema madhara mengine aliyo yapata ni pamoja na kuchanika sehemu zake za siri, kutokana na kukeketwa akiwa na wasiwasi kama atajifungua salama siku za baadaye.

“Mimi nahisi hata wakati wa kujifungua, nitapata matatizo, naomba wazazi wetu wabadilike waanze kwenda na wakati na watambue kuwa wanapotufanyia ukeketaji wanatufanyia ukatili wa kijinsia na kilema cha maisha” anasema.

Anasema kuwa kuna uwezekano wa wasichana wanaokeketwa kupata virusi vya ukimwi kutokana na kukeketwa ba ngariba mmoja, ambaye hukeketa zaidi ya wasichana 50 kwa siku.

Ester anaahidi kuhakikisha wadogo zake Neema na Happy kuwa hawato keketwa kwani yeye kashakuwa mkubwa anayejitambua ana kujua kujieleza.

NDOTO ZA BAADAYE ZA ESTA.
“Nitasomea uandishi wa habari, nitafanya kazi kwa bidii na natamani niwe kama Waziri wa Maendeleo ya Wanawake, Jinsia na Watoto, Sophia Simba. Nampenda jinsi anavyo wahudumia wanawake” anasema.

Ameiomba serikali kupitia jeshi la polisi kuwakamata mangariba wote wanao husika kufanikisha ukeketaji na kuwafikisha mahakamani, ili sheria ichukuemkondo wake .

Anaitaka jamii ya Wakurya kuendeleza watoto wa kike kitaaluma zaidi badala ya kuwaoza wakiwa katika umri mdogo, na hivyo kushindwa kuhilili kutunza familia.

Kamanda Emmanuel Mkoma.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime – Rorya, Emmanuel Mkoma anasema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau wengine wilayani Tarime, limeanza kutoa mafunzo ya tohara mbadala itakayo iwezesha jamii kutambua athari za ukeketaji kwa watoto wa kike.

Askari polisi, wanafunzi wa shule za sekondali na tiba ni sehemu ya kusanyiko la washiriki wa Kongamano lililokuwa mahususi kwa ajili ya kuibua changamoto zilizopo katika jamii kuhusu suala la ukeketaji.


Hisia za mmoja kati ya wanafunzi wa kiume na uelewa wa suala la ukatili wa kijinsia na ukeketaji wilayani Tarime mkoani Mara.

Wakisikiliza kwa makini ni wadau wa KIVULINI, Jeshi la Polisi na Wanahabari.
Lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa jamii, ambapo watoto wa kike watapewa elimu ya malezi ya Afya zao itakayo wasaidia wasikeketwe, msisitizo wake ni kuelimisha jamii ione madhara ya ukeketaji na kadri siku zitakavyo kwenda jeshi la polisi linaimani kuwa jamii itaachana na ukeketaji.

CREDIT: matukiotz.com
habari kamili :: read more...

Thursday, February 27, 2014

Cheki video ikionesha tofauti ya mdada na mkaka wakati wa kujiphotoa.


Kweli tuna tofauti ndo maana hata maamuzi yetu huwa pia tofauti. Nilikua najiuliza kwa nn picha nyingi chafu zinazozagaa mtanadaoni ni za wadada jibu hili...

Cheki video hii hapa chini chini utajua ni kwa nn.

habari kamili :: read more...

Nani atazima moto wa Lowassa CCM

Wana CCM msiwe na shaka, tutavuka kwa nguvu zetu... wingi wenu  huu unanipa  faraja kuwa katika safari yetu na kwa kumte gemea Mungu tutashinda ...Tulifurahi pamoja, tulihuzunika pamoja na tutashinda pamoja.”
 
WanaCCM msiwe na shaka, tutavuka kwa nguvu zetu... wingi wenu  huu unanipa  faraja kuwa katika safari yetu na kwa kumte gemea Mungu tutashinda ...Tulifurahi pamoja, tulihuzunika pamoja na tutashinda pamoja.”

Nguvu ya makundi ya watu wanaotajwa kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinaendelea kukitikisa chama hicho huku makada wake wakitoa angalizo wakiutaka uongozi wa juu wa kuchukua hatua haraka  za kinidhamu kwa wahusika.
Wiki iliyopita wanachama wa chama hicho wanaodaiwa kutoka katika kambi tofauti zinazoisaka nafasi ya urais waliibuka na kutoa kauli zinazoonekana wazi kupigana vijembe, kila upande ukiuponda mwingine kuwa unavunja kanuni na katiba ya chama hicho.
Malumbano hayo ya makada wa CCM yanayoonekana dhahiri kuchagizwa na makundi pamoja na wafuasi wa vigogo wanaousaka urais kupitia chama hicho.

Ingawa makundi yanayosaka urais kupitia chama hicho ni mengi, ni kundi moja tu linalomuunga mkono aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa ndilo linaloonekana dhahiri kupigiwa kelele kwa kutajwa kwa majina bila kificho, hasa baada ya kauli yake kuwa ameanza safari, aliyoitoa mbele ya wageni wakati wa kuadhimisha mwaka mpya 2014.
Kutokana na kauli hiyo na mambo mengine, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UV-CCM, Paul Makonda aliibuka na kumshambulia Lowassa, suala ambalo limeyaibua makundi mengine, baadhi  yakiunga mkono kauli ya Makonda na mengine yakiibeza na kumshushia tuhuma za kuvunja kanuni za chama.

Mmoja kati ya waliojitokeza ni Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Malecela ambaye ameonyesha waziwazi kutofautiana na mipango na mikakati ya Lowassa.
Malecela anamuunga mkono Makonda, kwa kauli yake, ikiwamo kwamba Lowassa anafadhili mikakati ya kupingana na juhudi za sekretarieti ya CCM chini ya Katibu Mkuu, Abdulrahaman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Wakati Makonda na Mzee Malecela wakitoa tuhuma hizo, makundi mbalimbali ya Jumuiya ya Vijana UVCCM nao wameibuka na kumshutumu Makonda kuwa aliyoyasema ni maoni yake na siyo msimamo wa Jumuiya hiyo.
Kauli hiyo ya Makonda imeibua malumbano baina ya viongozi wa jumuiya hiyo, wengi wakimshutumu kwa “kutumiwa kumchafua Lowassa” na kwamba kauli aliyoitoa ni ya kwake na idara yake, wala isihusishwe na Umoja wa Vijana wa CCM.
Baadhi ya waliojibu ni pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kupitia kundi la vijana, Jonas Nkya na Ramadhani Kimwaga,  pamoja na Mjumbe wa Baraza Kuu la jumuiya hiyo Mkoa wa Mbeya, Adam Mwakalinga.
Vijana hao kwa nyakati tofauti wanasema wamehuzunishwa na matamshi ya Makonda akimshutumu Lowassa na kutamka kuwa umoja huo hautaki kuingizwa katika masuala binafsi ambayo yanaweza kukigawa chama na jumuiya zake.
Mwakalinga anasema Makonda anapaswa kufanya kazi ya idara yake ya watoto badala ya kukurupuka na kutaka kuwaaminisha Watanzania kuwa Edward Lowassa si kiongozi mzuri huku akijua wananchi wenyewe na hata wapinzani wanaona uthubutu wake katika maendeleo hasa kwa vijana.


 Kauli ya Sadifa
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis anasema kutangaza nia ya kugombea nafasi yoyote ndani ya chama si kosa mradi tu mhusika ataridhika kuwa na nia, sifa na uwezo wa kile anachokisema.
Anasema ingawa UVCCM haijakaa kujadili watu hao, lakini haoni kosa lolote kwa mwanaCCM kujitokeza na kutangaza nia yake hadharani.
“Nikuulize mwandishi, kutangaza nia ni kosa? Kama mtu ameamua kueleza nia yake anakuwa amevunja sheria gani…sioni kosa lolote endapo mtu ameeleza nia yake baada ya kujiona anazo sifa, uwezo hiyo ni haki kikatiba,” alisema
Hata hivyo, Sadifa anasema kosa analoliona na ambalo ni kinyume na kanuni za chama ni kwa mtu kujipitisha na kuanza kusaka kuungwa mkono ingawa alikiri kuwa kwa yeye kama mwenyekiti hakuna aliyejitokeza kuomba amuunge mkono.
Anaongeza kusema kuwa kauli iliyotolewa na Makonda si ya Jumuiya kwa kuwa UVCCM haimuungi mkono mgombea yeyote.
“Msemaji wa UVCCM ni mmoja kitaifa na ndiyo mimi, hakuna msemaji mwingine…yaliyosemwa na Makonda ni yake mwenyewe na siyo msimamo wa jumuiya,” anasema.
Anaongeza kuwa ingawa Makonda anayo haki ya Kikatiba kutoa maoni yake lakini siyo sahihi wala busara kwa mwanachama kumsema mwanachama mwingine hadharani, badala yake mambo hayo yangepaswa kujadiliwa kwenye vikao vya ndani vya chama.
Wito kwa wanaCCM
Sadifa anatoa wito kwa makundi yote yanayoibuka na yaliyopo ndani ya chama hicho kutulia kwa kile alichosema muda wa kampeni haujafika na kwamba hali hiyo ikiendelea itasababisha chama kushindwa kumpata mgombea safi maana wote watakuwa wameshachafuka.
“Ushauri wangu ni kwa wanaCCM wote kuwa watulivu kwa faida ya chama…kuchafuana au kuharibiana ni kukiharibia chama kwani wakati ukifika tutashindwa kumpata mgombea safi,” anasema Sadifa.

Kauli ya Msekwa:
Wakati malumbano hayo yakiibuka, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa anawaonya wanachama wa chama hicho wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao kuzingatia kanuni za chama hicho, vinginevyo watahukumiwa kwa mujibu wa kanuni zenyewe.
Msekwa anasema kutangaza nia kabla ya wakati ni kukiuka kanuni za chama ambazo zinaeleza wazi kuwa wagombea wa nafasi mbalimbali watajitangaza baada ya chama kutoa ratiba yake.
Anasema CCM inaongozwa kwa mujibu wa kanuni na katiba yake na kwamba katika jambo hili linaloibuka sasa kanuni ndiyo zinayohusika ambazo zinaeleza wazi mgombea afanye nini na kwa wakati gani.
 “Mimi mwenyewe nilishiriki kuandika hizi kanuni, utakapofika wakati, chama kitatoa ratiba yake na kila mwenye nia atakuwa na uhuru wa kueleza nia yake, lakini kutangaza kugombea sasa kabla ya wakati ni kukiuka kanuni za chama na ni kosa kubwa,” anasema Msekwa.
Msekwa anatoa angalizo kwa wale wanaodhani kuwa kwa kuvunja kanuni wanakivuruga chama, badala yake wahusika wanafanya makosa yatakayowaathiri wenyewe.
Hii si mara ya kwanza kwa Msekwa kukemea makundi ndani ya chama hicho, akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, wakati akiwahoji watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho, alipata kusema makundi ya wanaowania urais, yanakivuruga chama na kuwa hakitawavumilia wanaochochea migogoro hiyo kwa masilahi yao binafsi.
CREDIT:Mwananchi.

habari kamili :: read more...

Saturday, February 22, 2014

Mke amfumania bwanaake na kimada kitandani kwake.


NI kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni! Fumanizi la aina yake lilitokea juzikati asubuhi ya saa 2, Mtaa wa Mbwela, Tandika jijini Dar ambapo mjamzito aliyejulikana kwa jina la Semeni  alipata ‘kichaa’ cha muda baada ya kumfumania mumewe, Dullah akiwa na mwanamke  mwingine chumbani kwao, Risasi Jumamosi lina kisa kizima.

Akisimulia mkasa huo, Semeni mwenye ujauzito wa miezi 6 alisema kabla ya tukio aligombana na mumewe akarudi kwao kwa muda wa siku mbili lakini walikuwa wakiwasiliana mpaka asubuhi ya tukio ambapo alimpigia simu kumwambia anafuata nguo kwa vile anakwenda kliniki. 
“Nilipokuwa njiani nilimpigia simu mume wangu, nikamwambia nimekaribia, lakini akasema yeye amekwenda Posta. 




“Pamoja na majibu hayo, niliamua kwenda. Nilipofika nilikuta mlango umefungwa kwa ndani, nikampigia simu mume wangu, akasisitiza hakuna mtu, yeye yupo Posta.

“Nilichungulia na kuona funguo, nikajua kuna mtu ila hataki kunifungulia, hapo wasiwasi ukazidi kwamba huenda kuna jambo linaloendelea,” alisema Semeni.

Mwanamke huyo aliendelea kuanika kwamba kufuatia hali hiyo aliwaita majirani ambao ilibidi wamtishe mtu aliye ndani kwamba asipofungua watavunja mlango, ndipo mlango ukafunguliwa na kumkuta Dullah akiwa na mwanamke mwingine chumbani, lakini mumewe huyo alichoropoka na kukimbia.
“Nilishtuka, nikapiga kelele ya mshangao kutokana na kitendo alichokifanya mume wangu, kumleta hawara mpaka kwenye chumba tunacholala!

“Sijaamini kilichotokea! Yule ni mume wangu, amewezaje kumleta mwanamke ndani ya chumba tunacholala tena kuna wapangaji wenzangu wameshuhudia,” alisema mwanamke huyo huku akilia machozi.
Akaendelea: “Mimi hapa nyumbani siachiwi hela ya kula, kila siku nakula nyumbani kwetu,  nikijua labda mume wangu hana, kumbe anamalizia kwa hawara! Jamani inaniuma sana, kama hivyo bora amuoe basi tuje tuishi wote au aniache akae yeye.”

Akizungumza na gazeti hili kwa uso ‘uliochunwa’, mwanamke aliyedaiwa kufumaniwa, Mwanaidi huku akiwa ‘ametaitiwa’ ndani, alijitetea kuwa hakufahamu kama Dulla ana mke.
“Mimi aliniambia hana mke wala mtoto na ndiyo maana nilikubali kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na yeye si vinginevyo, kama ningejua nisingekubali kuja, kwa hiyo siyo kosa langu,” alisema Mwanaidi.
Baada ya hali kutulia, baba mzazi wa Dullah ambaye anaishi jirani aliitwa kuamua ugomvi huo na kuamuru wote waende nyumbani kwake ambapo  aliagizia gari.
Wawili hao walipofika nyumbani kwa mzazi huyo walimshusha Semeni na kumtaka atangulie ndani, alipoingia tu, nyuma dereva alitakiwa kuondoka gari hilo kwa kasi  huku Mwanaidi akiwemo ndani ili kumnusuru.
Baada ya kubaini ‘triki’ hiyo, Semeni alijirusha chini kwa hasira na kujigalagaza kisha kulikimbiza gari hilo bila mafanikio.
habari kamili :: read more...

Mwanafunzi ajidunga kisu baada ya kufeli kidato cha nne.


Kijana ambae jina lake halijafamika mpaka sasa,anayeishi mwnanyamala dar es salaam ambaye inasemekana kuwa ni mwanafunzi ambae alimaliza kidato cha nne mwaka jana yan elfu 2013 alikutwa amejichoma kisu shingoni na kuwahishwa hospital ,huku chanzo kikisemekana kuwa ni matokeo yako ya kidato cha nne,matokeo yake hayakuwa mazuri maana amefeli kwa kupata zero.
habari kamili :: read more...

Tuesday, February 18, 2014

Nguo maalumu za ndani zatengezwa kusaidia kukabiliana na ubakaji.

 
Kampuni moja ya kupambana na ubakaji wametengeza chupi maalum AR VPL ili kuzuia ubakaji wa wakinamama lakini wakosoaji wa chupi hizo wanasema zinawatia hofu wanawake kwamba vitendo vya ubakaji vimeongezeka.

Chupi aina za AR zimezinduliwa rasmi kwenye mtandao hivi karibuni (online) kusaidia kufikisha ujumbe kwa rai wa Uingereza kwa haraka sana .

Chupi hizo zimekuwa zikikosolewa sana kwamba si suluhisho la ubakaji na unyanyasi wa kijinsia kwa wakinamama na wasichana wadogo kwa sababu mtu anaweza kupambana hata na kitu cha ncha kali na kuchana chupi hiyo kwenye purushani ya kutaka kumbaka.

Kuundwa kwa chupi hizo kunawapa wasichana wengi faraja ya kutembea usiku, kusafiri peke yako, kwenda nje kwenye klabau za usiku.
Mradi huo ulianzishwa na chama cha watetezi wanawake wa jiji la New York (NYACK), New York ambao wanasema kuwa walifanywa utafiti kwa miaka mitatu kabla ya kuja na aina za chupi hizo
habari kamili :: read more...

Monday, February 17, 2014

Picha na matukio ya Mgombea ubunge jimbo la Kalenga kupitia CHADEMA alipochukua fomu.

 Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kalenga Bi Pudensiana Kisaka akimkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Kalenga Bi. Grace Tendega anayeiwakilisha CHADEMA katika ukumbi wa sayansi na kilimo cha wilaya ya Iringa vijijini leo hii.

kiongozi huyo wa CHADEMA alipokuwa anawasili katika eneo la ukumbi huo kwenda kuchukua fomu hiyo ambayo kwa mujibu ya sheria za uchaguzi huo inatakiwa kurudishwa tarehe 18/02/2014 (kesho, Jumanne)


msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo la Kalenga; Bi. Pudensiana Kisaka alipokuwa anamkaribisha kiongozi huyo wa CHADEMA, Bi. Grace Tendega kuchukua fomu hiyo katika ukumbi huo.

Bi. Grace Tendega alipokuwa anakaribia kukabidhiwa fomu hiyo ya ugombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo hilo la Kalenga kupitia CHADEMA

Kiongozi huyo (Grace Tendega) alipokuwa katika ofisi ya  CHADEMA wilaya ya Iringa katika eneo la Mshindo; alipokuwa akijibu maswali waandishi wa habari.
Na Riziki Mashaka.
habari kamili :: read more...

Kesi ya Elizabeth Michael LULU imehairishwa hadi mahakama itakapotoa taarifa tena.


Elizabeth Michael 'Lulu' (katikati) akiwa na mama yake mzazi, Lucresia Karugila (wa pili kushoto) na Dk. Cheni (kulia) ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo.

 Leo February 17 kutoka Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam, msanii wa maigizo nchini Tanzania Elizabeth Michael maarufu kama Lulu alikuwa akisomewa shitaka lake la kuua bila kukusudia msanii mwenzake wa maigizo Marehemu Steven Kanumba April 07 2012  eneo la Vatican.

Akisoma maelezo ya awali wakili wa serikali Monica Mbogo mbele ya Jaji anayesikiliza kesi hiyo Rose Teemba amesema mshtakiwa siku ya tukio kulikuwa na ugomvi kati ya marehemu na mshtakiwa na baadaye mshtakiwa aliondoka usiku wa saa sita baada ya marehemu kuanguka chumbani ambapo alfajiri ya April 07  majira ya saa 11 alfajiri Lulu alikamatwa eneo la Bamaga.

  Kwa upande wake wakili  Peter Kibatala ambaye anamtetea Lulu amesema wameridhishwa na sehemu kubwa ya  maelezo ya awali ya mteja wao, ambapo kesi hiyo imeahirishwa mpaka itakapopangwa tena huku kila upande ukitarajia kuleta mashahidi watatu.

 Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie waliohudhuria leo mahakamani ni Dr.Cheni na Kajala.
habari kamili :: read more...

Nape: Msimamo wa CCM ni Nchi kuwa na Muundo wa serikali mbili.




Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa Habari nje ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma ambapo aliwaeleza kuwa Kikao cha NEC kilikamilika vizuri ambapo wajumbe waliijadili Rasimu vizuri na CCM kubaki na msimamo wa Serikali mbili .


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa Habari nje ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma na kuwaambia CCM bado imebaki na msimamo wake wa muundo Serikali mbili wenye maboresho.
habari kamili :: read more...

Jamaa amgwaya mgoni na kumpa kichapo mkewe baada ya kuliwa uroda usiku kucha na mshikaji huyo.

Hapa akiwa amelala hajitambui baada ya kupata kipigo
Tukio hili limetokea leo asubuhi ,katika mji wa Iringa maeneo ya mwangata. Paparazzi wetu alifanikiwa kulinasa hili tukio.Jamaa mmoja jina halikuweza kupatikana amemfumania mkewe gesti baada ya kumfumania alichokifanya ni kumruhusu yule mwanaume aliyemfuma na mke wake nakusema jamaa hana kosa mwenye kosa ni mke wake.Jamaa akazidi kufunguka nakusema mke 
wake alitakiwa kukataa alipotongozwa moja kwa moja mke wangu ndiye mwenye makosa huyu mgoni hana kosa kabisa.

Kilichofuata baada ya hapo alimpa kichapo kikali kama unavyoona kwenye picha. Mwisho wa siku akambeba na kurudi naye nyumbani maeneo ya mwembetogwa ili kumfungashia mizigo yake na kumrudisha kwa wazazi wake. 





 Hapa wananchi wakiwa wanashudia jamaa akimpa kichapo mkewe baada ya kumfumania
 
Picha hii jamaa amembeba mke wake baada ya kumfumania na kumpa kipigo kikali wakielekea nyumbani
Maoni yetu: Ukimegewa sh wako basi komaa na aiyekumegea mbona waleta ujinga kumpiga mkeo.  
habari kamili :: read more...

Du kumbe kuna dawa ya kurudisha bikira, Mchina noma; soma hapa.

Watu wengi hujiulizia  kama  kuna dawa  ya  asili  ya  kurejesha  bikira  kwa wanawake.
Ni kwamba,  haipo  dawa  ya  asili  inayo  weza  kurejesha  bikira  kwa  mwanamke.
Dawa  zilizopo ni dawa  za  kichina, na  zinamadhara.

Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, mwanamke  anaye  tumia  dawa za  kichina  kwa  ajili  ya  kurejesha  bikira  yake anajiweka  katika   hatari  kubwa sana  ya  kupatwa  na  ugonjwa  wa  kansa kutokana  na  kemikali  mbalimbali zinazo  patikana  katika  dawa  hizo.

USHAURI  WETU :
Tunashauri  usitumie  dawa  za kichina  kwa  ajili  ya  kurejesha  bikira  kwa  sababu madhara  yake  ni makubwa sana.


UTUMIE  DAWA  GANI?:
Hakuna  dawa  ya  kurejesha bikira, dawa  za  asili  zilizopo  ni  dawa  zinazo  fanya kazi  ya  kuufanya  uke  kuwa  tight sana  lakini  hauwi  bikira. 
Bikira  ikishatoka  haiwezi  kurudi  tena.
habari kamili :: read more...

+18 only; Video a wanachuo wakifundishana jinsi ya ku du hii hapa; Kweli hapa hamna shule.

Kweli vyuo vyetu siku hizi maadili hamna yaani badala ya kusoma wadada hawa wamebuni namna ya kuwafundisha wengine namna ya kumhandle mwanaume.


Inasemekana haka kamtindo kameenea sana baada ya wanachuo wengi hasa wanaotoka vivijin kutofahamu staili mbalimbali hivyo hufurahia sana lesson hiyo.
Icheki mwenyee hii hapa
habari kamili :: read more...

Ukiwa na mke wa staili hii basi ujue hamna kitu hapo ebu cheki anachokifanya anapokuwa bafuni.

Ukiona una mke anakienda kuoga anakawia sana basi ujue ndo anafanya haya ya huyu mdada na kama uamini basi nyemelea siku moja utagundua.

Huyu ni mwanamuziki toka nchini Nigeria aitwaye Maheeda, ni mmoja kati ya wanamuziki wasioisha na vituko. Kimtindo ni mwehu na hakika hatoacha wehu wake
habari kamili :: read more...

Saturday, February 15, 2014

Dayna na Cindy wa Uganda wababwiwa mbaya na mashabiki usiku wa Valentine kwenye shoo.

 

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Dayna Nyange akikamua vilivyo usiku huu wa Valentine Day katika Ukumbi wa JB Belmonte Hotel katika jiji la Rocky City (Mwanza) ambapo katika ukumbi huo huo alikuwepo na mkali  wa muziki Cindy Sanyu kutoka Nchini Uganda pamoja na wasanii wengine wa hapa jijini Mwanza.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Dayna Nyange akifanya mambo yake jukwaani usiku huu.

Dayna akiimba kwa hisia moja ya wimbo wake mbele ya mashabiki wake
Nivute kwako!!! ni wimbo wake msanii Dayna akiuimba vyema Jukwaani leo kwenye Ukumbi wa JB Belmonte Hotel katika jiji la Rocky City (Mwanza) leo Valentine Day.

Dayna Nyange amekamua nyimbo zake kadhaa huku wadau wakimkubali zaidi katika ukumbi huu. Cha zaidi kwa Dayna hakuweza kuficha tabasamu lake huku akijua ni sikukuu ya Wapendanao hivyo amekamua kisawasawa!!!


Cindy Sanyu kutoka Nchini Uganda(katikati) akicheza kwa pamoja na wanamuziki wake kuwapa kile Wabongo walichomwitia katika ukumbi huu wa JB Belmonte Hotel.

habari kamili :: read more...

Ndoa ya Ray na Chuchu utata mtupu; Inasemekana eti Chuchu ana bwana ake yuko nje.

Ni pigo kubwa! Ile ndoa inayodaiwa kukaribia kufungwa kati ya nyota wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Miss Tanga 2006 aliye pia msanii wa filamu Bongo, Chuchu Hans imepingwa isifungwe mpaka mambo
f’lani yakae  sawa.


Kwa mujibu wa mtonyaji wetu, Ray na Chuchu wako mbioni kufunga ndoa wakati wowote kuanzi Mei, mwaka huu, lakini mjadala mzito uliopo mbele yao kwa sasa ni uhalali wake.
“Unajua wanachofahamu wao (Ray na Chuchu) wanaweza kufunga ndoa kwa ulaini kabisa, lakini ukweli ni kwamba kuna ugumu mkubwa

UGUMU ULIPO
“Kanisa analosali Ray, viongozi wanasema wao si wa dunia hii mpaka wakubali kufunga ndoa ambayo mmoja wa wahusika ana ndoa yake,” kilisema chanzo hicho.
Kikaendelea: “Kwa hiyo kama wako tayari kufunga ndoa hiyo lazima Chuchu akubali kubadili dini yeye ndipo ataruhusiwa kungia kanisani kufungishwa ndoa.”


Ray na Chuchu wakijiachia.
KANISA LA RAY
Juzi Alhamisi, Risasi Jumamosi lilifunga safari hadi kwenye Kanisa la Living Water-Makuti Kawe, Dar ambako mpaka mwaka uliopita magazeti pendwa yaliandika Ray anaabudu huko.
Lengo la Risasi Jumamosi lilikuwa kuonana na Mtume na Nabii Onesmo Ndegi lakini hakuwepo ofisini, ila msaidizi wake mmoja alipopatikana alikiri kumfahamu Ray.
Msaidizi:  Ray alishasali hapa, lakini sijamwona siku nyingi, sijui ana matatizo gani?
Risasi Jumamosi: “Oke, tukiacha hilo la kutofika kwa siku nyingi. Lililopo sasa hivi ni kwamba anataka kufunga ndoa na dada mmoja anaitwa Chuchu Hans ambaye ana ndoa tayari, hajaachika na mumewe yu hai. Unasemaje kuhusu hilo?
Msaidizi: “Sisi hatuamini katika kuachana. Kama alishafunga ndoa na mume yupo hai, hao wametengana tu, lakini ndoa yao ipo.
“Huyo mwanamke alishajifunga, kifungo chake kitatenguliwa pale tu mumewe atakapoondoka duniani (kifo).

KANISA LA MTAKATIFU MAXIMILIAN KOLBE
Baada ya kuondoka kanisani hapo, mapaparazi wetu walikwenda Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe, Mwenge, Dar es Salaam.
Risasi Jumamosi liliambiwa Baba Paroko hakuwepo kwa wakati huo, lakini muumini mmoja aliyesema yeye ni mwalimu alipoulizwa kuhusu nafasi ya Ray kufunga ndoa na Chuchu Hans alisema:
“Maandiko yako wazi. Sasa kama huyo mwanamke ana mume wake tena mmesema yupo nje ya nchi, siku akija si atamshika ugoni kwa mke wake?
“Huwezi kufunga ndoa kama bado una ndoa. Mungu hajaagiza hivyo. Ndiyo maana sisi (Wakristo) huwa tunatoa siku ishirini na moja za kutangaza ndoa ili kama kuna mwenye pingamizi ajitokeze na kulianika.
“Watu waongo siku hizi. Wapo wachumba wanakuja kuandikisha ndoa kumbe mmoja bado yupo kwenye ndoa halali.”

IMANI YA KIISLAM INASEMAJE?
Mapaparazi wetu hawakuchoka, walimtafuta Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum ambaye kuhusu Ray na Chuchu kufunga ndoa alifunguka hivi:
“Kama Chuchu ni Muislam, itabidi Ray abadili dini awe Muislam, si vinginevyo.”
Risasi Jumamosi: Chuchu alifunga ndoa Bomani na mume Mkristo, ila yeye Muislam. Inakuwaje hapo?
Sheke Mkuu: “Itakubalika kama Ray atabadili dini tu, maana hiyo ndiyo ya Bomani, Kiislam siyo.”

JOHARI, MAINDA WAPATANA
‘Johari’ ambaye ni Blandina Chagula na ‘Mainda’ mwenye uhalisia wa jina la Ruth Suka (zamani Mwanaid), wawili hao sasa ni mashosti wakubwa baada ya kuwa na bifu la miaka 8 kisa kikitajwa  kuwa ni ‘kaka mkubwa’ huyo (Ray) kuwachanganya kimapenzi.
Kwa mujibu wa chanzo, mastaa hao wanaotamba kwenye filamu za Bongo kwa miaka mingi wameamua kumaliza tofauti zao huku wengi wakitafsiri kuwa, wanashikamana kwa sababu ya  kuumaliza uhusiano wa Chuchu na Ray. Haikufafanuliwa.

MADAI MENGINE
Pia ilidaiwa kuwa, Mainda aliamua kumaliza bifu na Johari kwa sababu mchungaji wake alimtaka  kufanya hivyo.
“Niliwakuta kambini wakishuti filamu, Mainda akaniambia aliitwa kushiriki filamu hiyo kama mpambaji, Johari yeye amecheza baadhi ya  vipande ndipo Mainda akamtaka mwenzake wamalize tofauti zao,” kisema chanzo chetu.
Hivi karibuni, Risasi Jumamosi liliinasa picha iliyotundikwa mtandaoni na Mainda akimwonesha yeye, Johari na Mtangazaji wa StarTV, Sauda Mwilima.
Mainda aliisindikiza picha hiyo na maneno  yaliyosema: “Nimejifunza kitu katika maisha, kusamehe.” KAKA MKUBWA RAY
Juzi, Risasi Jumamosi lilimpigia simu ya mkononi Ray lakini hakupokea. Akatumiwa meseji, hakujibu! CHUCHU HANS
Baada ya kusomewa mashitaka yote, alijibu kwa ufupi: “Sina cha kuongea.” JOHARI
Johari naye hakupokea simu yake ya mkononi licha ya kuita kwa muda mrefu na kukatika kisha kupigwa tena. Akatumiwa meseji, hakujibu! MAINDA
Na yeye simu yake iliita sana bila kupokelewa, akatumiwa meseji, hakujibu!
habari kamili :: read more...
 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top