Thursday, July 31, 2014

Al Shabab yaua mama kwa kutofunga niqabu; Inasikitisha sana.

Wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabab wamempiga mwanamke mmoja risasi na kumuua kwa kukosa kujifunga niqab kichwani.

Jamaa za mwanamke huyo mwenyeji wa mji wa Hosingow kusini mwa Somalia wanasema mwanamke huyo alikataa kujifunika kitambaa kichwani kuambatana na sheria za dini ya kislamu .

''alikuwa ameonywa ajisitiri lakini wapiganaji hao waliporejea wakashikwa na hasira walipopata kuwa hakuwa amejifunika na hivyo wakampiga risasi''.

Jamaa zake wameiambia BBC kuwa Ruqiya Farah Yarow alikuwa amewafokea wapiganaji hao akiwataka waondoke kwake na kusema kuwa angejisitiri baadaye.

Kundi la Al Shabab linalomiliki asili mia kubwa ya maeneo ya Kusini na Katikati ya Somalia na limekuwa likishinikiza kutumiwa kwa sheria kali za kiislamu.

Hata hivyo msemaji wa kundi hilo amekanusha kuwa ni wao waliomuua mwanamke huyo .

Msemaji huyo anasema kuwa licha ya kudhibiti maeneo makubwa nchini humo kundi hilo bado halijatoa maelezo ya vipi wanawake wanastahili kujisitiri.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Liverpool yailaza Mancity kwa mikwaju ya Penati huko New York.

Liverpool iliwalaza mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza Manchester City mabao 3-1 kwa mikwaju ya penalti timu hizo zilipokutoshana nguvu 2-2 katika muda wa kawaida katika mechi ya kirafiki ya kuwania taji la mabingwa wa kimataifa (International Champions Cup).

Mechi hiyo iliyovutia mashabiki elfu 50,000 katika uwanja wa yankee ulioko New York ilianza bila ya msisimko kipindi cha kwanza kikikamilika matokeo yakiwa ni suluhu bin suluhu.

Lakini katika kipindi cha pili, mabingwa hao walidhibitisha niya yao mapema kupitia bao la Stevan Jovetic.

Kiungo cha kati wa Liverpool ,Jordan Henderson aliisawazishia timu yake kabla ya Jovetic kuirejeshea City uongozi .

Uongozi huo hata hivyo haukudumu kwa muda mrefu kwani Raheem alifanya mambo kuwa 2-2.

Waandalizi waliamua mechi hiyo ikamilishwe kwa kupiga matuta ya penalti.

Na hapo vijana wa Brendan Rodgers walitamba na kujikatia tikiti ya nusu fainali ambapo sasa watachuana na AC Milan ya Italia .

City sasa itakwaruzana na Olympiakos ya Ugiriki.

Mchuano huo unajumuisha timu 8 za kimataifa.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa tuzo ya kimataifa ya Nyota wa Demokrasia Afrika 2014.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa mara nyingine ametunukiwa tuzo la kimataifa – zamu hii kwa kuwa mshindi waTuzo la Nyota wa Demokrasia Afrika  2014 – Icon of Democracy Award Winner for 2014 in Africa.

Kwa mujibu wa barua aliyoandikiwa Rais Kikwete na kupokelewa Ikulu, Dar Es Salaam, Rais Kikwete amekuwa mshindi wa kwanza, na kwa mbali kabisa, katika mchuano na marais watatu wa Afrika ambao walifikia mwisho mwa mchuano wa kuwania tuzo hilo.

Katika barua hiyo, Mchapishaji na Mhariri Mkuu wa Jarida hilo, Pastor Elvis Iruh, akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Tuzo 2014, amesema kuwa uongozi wa Rais Kikwete umekuwa ni hadithi ya kusifiwa ya mafanikio katika Bara ambako hadithi za namna hiyo siyo nyingi.

Tuzo hilo hutolewa na Jarida la The Voice na mwaka jana mshindi alikuwa ni Rais Bai Koroma wa Sierra Leone ambaye alikuwa ni mshindi wa pili wa Tuzo hiyo ambalo ilitolewa kwa mara ya kwanza kwa Rais wa Kwanza wa Zambia, Mzee Kenneth Kaunda.

Sherehe maalum ya kukabidhi tuzo hiyo imepangwa kufanyika Oktoba 17, mwaka huu, 2014, katika Hoteli ya Van der Valk, iliyoko Almere, Uholanzi.

Miongoni mwa sifa nyingine, Rais Kikwete anatunukiwa Tuzo hiyo kwa sababu ya kuwa msimamizi mzuri na wa kweli wa demokrasia, kuendelea kuhakikisha kuwa amani, utulivu na maendeleo vinaendelea kupatikana katika eneo la Afrika ambalo limepitia vipindi vingi vya migogoro na matatizo.

Aidha, gazeti hilo linasema kuwa Rais Kikwete amekuwa kiongozi wa mfano, kimataifa na kikanda, na linatoa mfano wa mchango wake katika kusuluhisha mgogoro mkubwa wa kisiasa nchini Kenya kufuatia uchaguzi mkuu wa 2007.

Rais Kikwete pia anasifiwa kwa mchango wake katika kusimamia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbali mbali – kilimo, elimu, miundombinu, maendeleo ya viwanda, utalii na pia mchango wake katika kuendeleza vijana na kutoa nafasi nyingi kwa akinamama kushika nafasi nyingi za uongozi.

Jarida la The Voice pia limempongeza Rais Kikwete kwa kuimarisha Umoja na Muungano wa Tanzania na kutoa nafasi kwa wananchi kujadili na kukubaliana kuhusu Katiba mpya ya Tanzania.

Aprili mwaka huu, Rais Kikwete alitunukiwa tuzo la kuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya Afrika kwa mwaka 2013 – The Most Impactful Leader in Africa 2013.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.

30 Julai,2014

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA ATOROKA SHULE NA KWENDA KULIWA URODA GESTI MCHANA KWEUPE MORO;


Askari wa jeshi la polisi na wasamaria wema wakiwa wamemdhibti binti anayedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba moja ya shule ya msingi Manispaa ya Morogoro, binti huyo anadaiwa kukurupushwa katika moja ya nyumba ya kulala wageni eneo la Mawenzi wakati akipelekwa kituo kidogo cha polisi. Kwa kile kinachodaiwa kujihusisha na mapenzi na masomo.

Wasamalia wema wakiwa wamemdhibti binti anayedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa darasa la saba Manispaa ya Morogoro baada ya kumnusuru na kipigo

kutoka kwa kundi la wananchi wenye hasira waliotaka kufuatia binti huyu kudaiwa kukurupushwa katika moja ya nyumba ya kulala wageni eneo la Mawenzi mkoani Morogoro.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya. 

ISOME NA HII PIA

Binti afanyiwa mchezo mchafu chooni baada ya kulewa vibaya akiwa Night Club SINZA DAR.

 

habari kamili :: read more...

NDOA YA LUCY KOMBA NI MIZENGWE MITUPU.


HUKU akiwa kwenye vikao vya maandalizi ya harusi na Mzungu, staa wa filamu Bongo, Lucy Francis Komba (pichani na mchumba wake), amejikuta katika wakati mgumu baada ya habari kudai kwamba, mchumba wake huyo amemwambia ili ndoa ifungwe lazima aoneshe cheti cha kipimo cha Ukimwi kwanza.

Staa wa filamu Bongo, Lucy Francis Komba akiwa na mchumba wake.

Chanzo chetu cha habari kikizungumza na Amani juzi, kilisema kwa sasa Lucy anahaha kutafuta cheti feki cha kipimo hicho kwa kwenda hospitali mbalimbali ili anunue kwa gharama yoyote lakini imeshindikana.
“Ukweli Lucy anahaha kutafuta cheti cha Ukimwi, mchumba anasubiri akione vinginevyo hawatafunga ndoa,” kilisema chanzo.

Ilidaiwa kuwa, mpaka sasa Lucy ameshafika kwenye hospitali tatu kubwa mbili, TMJ na Marie Stopes ili kufanya maarifa lakini imeshindikana.

Baada ya kupata habari hizo paparazi wetu alimtafuta Lucy ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Si kweli! Hao wanaosema hivyo ni wanafiki, sijui wanataka nini maana kila siku wanazusha mambo ya ajabu. Kwanza mimi huwa sitibiwagi kwenye hospitali hizo ulizozisema, natibiwa Regency.

Lucy Francis Komba.

“Kuhusu  kupima Ukimwi, mimi na mchumba wangu tulishapima hukohuko kwao Ulaya (Denmark) ndiyo maana tukaanza taratibu za ndoa.

“Namshangaa sana huyo aliyesema hayo hata kama ni mtu wangu wa karibu, mimi huwa simwelezi mtu mambo yangu binafsi kwa sababu duniani hakuna rafiki wa kweli, rafiki anakuchekea machoni lakini wote ni wabaya,” alisema Lucy.

Amani lilifika kwenye hospitali hizo lakini kukakosekana ushirikiano kwa madai kwamba, hakuna utaratibu wa kumtaja jina mgonjwa kama alikwenda kutibiwa



Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

MUME AMPIGA VIBAYA MKEWE AKISWALI.


TUHUMA nzito ya aina yake ambayo haijawahi kutokea ambapo mkazi mmoja wa Tandale – Kwatumbo wilayani Kinondoni jijini, Idd Mpenda anadaiwa kumshambulia na kumjeruhi hadi kuzimia mkewe, Nasra Dafa (30) wakati akiswali.

Bi. Nasra Dafa (30) aliyeshambuliwa na mume wake wakati akiswali.

Akizungumza na Amani huku akimwaga machozi, mwanamke huyo alisema tukio hilo lilijiri Julai 28, mwaka huu saa saba mchana wakati akiswali maeneo ya duka lake lililopo Tandale.

ILIKUWA KUSHTUKIZA
Alidai kwamba alikuwa katika kusujudu,  mara mumewe alitokea na kumshambulia kwa mateke, ngumi na viatu kisha akamburuza chini hadi nje hali iliyosababisha nguo aliyovaa kuvuka na kubaki kama alivyozaliwa!“Kama unavyoniona, nimeumia sehemu mbalimbali za mwili. Kiatu ndiyo kimeniumiza sana.

Majeraha ya mguuni aliyopata Bi. Nasra Dafa.

ATINGA KITUO CHA POLISI
Alisema baada ya tukio hilo kutokea  alijivuta na kuvaa gauni lingine kisha akakimbilia Kituo Kidogo cha Polisi Tandale ambapo polisi walimwambia ishu yake ni nzito na kumtaka aende Kituo cha Polisi Magomeni (vyote vipo Dar).

ASIMULIA VIPIGO, UKE WENZA
Mwanamke huyo aliweka hadharani kwamba mumewe amekuwa akimpiga mara kwa mara na tatizo kubwa ni uke wenza ambapo alidai ameoa mke wa pili hivi karibuni na mapenzi baina yao yamezorota.

“Mimi kabla ya kufunga naye ndoa Januari Mosi, 2013 mume wangu alikuwa na mke mwingine lakini aliamua kumpa talaka baada ya kumweleza kuwa mimi sitaki kuwa mke mwenza.
“Tukawa tunaishi naye lakini hata hivyo hakuchukua muda mgogoro ukaanza ndani ya nyumba.

Picha hii ikionyesha majeraha ya mkononi na shingoni aliyopata Bi. Nasra Dafa.

SAKATA LAFIKA KWA NDUGU
Mwanamke huyo aliendelea kusema kwamba hali ilizidi kuwa mbaya hadi ikafika kwa wana ndugu kwa suluhu, walipatanishwa lakini baada ya muda mgogoro ukaendelea na kuna siku mumewe akamwambia ameoa mke mwingine wiki tatu nyuma.

SIKU YA TUKIO
“Siku ya tukio, nilikuwa naswali. Unajua wakati wa Mfungo wa Ramadhani lazima Muislam kuswali kwa kuzingatia taratibu zote za dini. Basi, alikuja na kuniita nitoke nje lakini sikutoka.“Niliona nimalize kwanza kuswali  ndipo nitoke, lakini kabla sijamaliza akaja na kunishambulia kama niliovyokwambia kisha akachukua funguo na kufunga duka.

“Alipotoka hapo akaenda kwenye duka lingine la kuuza vocha nalo akalifunga na kuchukua fedha zote na kuondoka nazo huku muuzaji akiambiwa aende kwake,” alisema mwanamke huyo.

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum akifafanua jambo.

Amani lilifika kwenye Kituo cha Polisi Magomeni na kuambiwa na askari mmoja kuwa taarifa hizo zipo na mtuhumiwa anashikiliwa hapo, lakini akashauri atafutwe Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura kwa maelezo zaidi. Kamanda huyo hakupatikana ofisini kwake hadi tunakwenda mtamboni.

SHEHE MKUU ASAKWA
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum hakupatikana kuzungumzia makosa ya mume wa Kiislamu kumpiga mkewe wakati akiswali ndani ya Mwezi Mtukufu.Hata hivyo,  Maalim Hassan Yahya Hussein wa Magomeni Mwembechai alipoulizwa alisema  Uislamu haujatoa ruhusa kwa mwanaume kumpiga mkewe wakati anaswali hata kama amefanya kosa kubwa kiasi gani.

“Uislamu haujaruhusu kwa hali yoyote udhalilishaji na kuna hadithi zinazokataza mtu kumdhuru mwenzake. Kuna masharti sita yamewekwa kabla ya mume kufikia hatua ya kumwadabisha mkewe,” alisema Maalim Hassan.Akaendelea: “Kabla mume hajampa adhabu mke anapaswa kwanza kumpa nasaha kwa kosa alilotenda na sharti la pili ni kumpa mawaidha ama yeye mwenyewe au atafute mtu.

“Sharti la tatu ni kumkumbusha mara kwa mara na  sharti la nne ni kumhama malazi, yaani kumuacha alale peke yake. Sharti la tano, akikosa ni kwenda kushitaki kwa wazee au katika vyombo vya sheria ikiwemo kwa kadhi na viongozi wa dini.“Sita ndiyo kumpiga, lakini kipigo ambacho hakitamdhuru kwani hutakiwi kumpiga ukiwa na hasira.”


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Tuesday, July 29, 2014

RAIS JK KATIKA SWALA YA IDDI DAR ES SALAAAM LEO HII.

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kuswali sala ya Iddi El Fitr katika mshikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiswali sala ya Iddi El Fitr katika masjid Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

"...Eid Mubarak....Eid Mubarak..."

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

SANGOMA AMFYEKA MTOTO NYETI NA KUTOKOMEA NAZO, WAZAZI ALIWADANGANYA ETI TOHARA.

 NI jambo lililowaacha midomo wazi madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam ambapo mtoto Almasi mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi (pichani akiwa na muuguzi) kufikishwa hospitalini hapo akiwa amekatwa nyeti na mtu aliyedaiwa ni mganga wa kienyeji ‘sangoma’ na kuipeleka kusikojulikana.

Mtoto Almasi mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akizungumza na Uwazi kwa masikitiko makubwa mwishoni mwa wiki iliyopita, baba wa mtoto huyo, Ismail Kamaga alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Kijiji cha Omukagando, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Alisema sangoma huyo aliyemtaja kwa jina moja la Adinali alifanya kitendo hicho  kwa watoto wawili akidai anawafanyia tohara.“Alidai anawafanyia tohara watoto wawili, baada ya muda mwenzake alipona wa kwangu hakuna kitu na nyeti aliondoka nayo, sina namna tena  ya kumsaidia mwanagu.

Nilimpeleka Hospitali ya Mugawa, Kagera ambako aliwekewa mpira wa kutolea haja ndogo na madaktari wakasema hawana jinsi.“Pia nilikwenda Kituo cha Polisi  Karagwe kuomba msaada wa kumkamata  mtuhumiwa lakini imeshindikana,” alisema baba huyo.

Mzazi huyo aliiomba serikali kumtafuta  mtuhumiwa akisema tukio alilolifanya ni sawa na kuuondoa uhai wa mtu.Kwa upande  wake,  muuguzi  wa  zamu aliyekuwa hospitalini hapo, Kulwa Kaombwe alisema kitendo kilichofanywa na mtu huyo si cha kuvumiliwa akaiomba serikali kuchukuwa hatua ili mtuhumiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

“Kwa ujumla huyu mtoto amebadilishiwa  staili ya maisha na hicho ni kilema. Kumkata uume maana yake mtoto huyo hatapata mke wala watoto katika maisha yake,” alisema muuguzi huyo.
Kuhusu matibabu, alisema wanaendelea naye lakini tabu anayoipata Almasi ni kujisaidia kwa shida hasa haja kubwa.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

ALEX MASSAWE AFANYA KUFURU YA FEDHA SAUZI.



WAKATI akisakwa kwa udi na uvumba na serikali ya Tanzania ili kuunganishwa katika kesi ya mauaji jijini Dar es Salaam, mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe anadaiwa kufanya jeuri ye fedha nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’.

Mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe akiwa ndani ya gari.

Katika video iliyowekwa katika mtandao mmoja wa internet na kurushiwa kwenye gazeti hili juzi, inamuonesha mtu anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara huyo akiwa na afya njema, akiwa na kijana mmoja aliyekuwa akimsifia mzee huyo kwa kumiliki fedha nyingi na gari la kifahari la kutembelea aina ya Toyota Lexus.

Kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Floyd akitamba kuwa jina lake lingine la utani ni ATM Mashine, anasikika akimpamba mfanyabiashara huyo kuwa hana shida na fedha, kwani gari alilokuwa akiliendesha pekee lina thamani ya Dola za Marekani 120,000 (karibu shilingi milioni 200 za Tanzania).

SIKIA MAELEZO YA KIJANA
Huku wakiwa ndani ya gari moja, kijana huyo anasikika akisema: “Hi guys, huyu hapa ni Mr. Alex Massawe, anaendesha gari lenye thamani ya dola 120,000 za Marekani na hapa ana pesa anazokwenda kufanya ‘shopping’ pale Mike Ranger Mall. Ni fedha ndogo sana kwake.

Akionyesha jeuri ya pesa

Ni za kununulia nguo na viatu tu,” anasema kijana huyo mdogo huku video ikimuonesha mfanyabiashara huyo aliyewahi kutangazwa kuwa ni bilionea, akitoa burungutu la dola katika mfuko wa koti.

MWONEKANO WAKE
Katika video hiyo, mtu huyo anaonekana  akiwa amevaa suti nyeusi, kofia nyeusi, miwani, pete kwenye vidole vya mkono wa kushoto na akiashiria kujiamini kupita kiasi.

NJIANI KUPONDA RAHA
Aidha, kijana anayemsifia ambaye pia amejitambulisha kwa jina la Half a Billionaire Man, aliendelea kusema kuwa walikuwa njiani kuelekea kuponda raha, hasa kwa vile siku hiyo ilikuwa ni Jumapili.
Mkononi kijana huyo akaonekana ameshika dola alizopewa na mtu huyo na akasema ni 15,000 (kama shilingi milioni 25).

“Hatuna shida na fedha, tunazo na tunatumia bila wasiwasi, tunaendesha magari mazuri kama hili unaloliona, Lexus na Guchi,” aliendelea kutamba kijana huyo huku mtu huyo akiwa anaendesha gari lake kwa utulivu bila kusema neno.

Mfano wa gari analomiliki

WADAU WASEMA NI DHARAU
Baadhi ya wadau katika maoni yao walisema kama kweli mtu huyo ni Alex Massawe ni dharau kwa mamlaka zinazohusika nchini kwa vile mtu huyo anaonekana hana hofu yoyote huku serikali ya Tanzania ikimsaka na ni vigumu kumkamata  .“Kama kweli inamsaka, mbona anatanua bila wasiwasi wowote ule jamani?” alihoji mdau mmoja.

AMETENGENEZWA?
Baadhi ya watu walitilia shaka kuwa, huenda video hiyo ilitengenezwa lakini Uwazi iliipeleka kwa wataalam wa kompyuta IT ambao walipoiangalia walisema hakuna kilichotengenezwa, ni halisia. Uwazi lilichukua picha za video hiyo na nyingine kwa kuziweka pamoja zikaonesha kushabihiana kwa sehemu kubwa.

RPC KINONDONI AZUNGUMZA NA UWAZI
Baada ya kuinyaka video hiyo, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura ambaye anasimamia upelelezi wa tukio la mauaji ya mfanyabiashara aliyeuawa katika mkoa wake.

Mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe.

Yeye alisema: “Hilo suala lipo kwa Polisi wa Kimataifa (Interpol), wao wanamfuatilia kwa karibu sana. Atapatikana tu.”

KAMANDA KOVA NAYE
Baada ya hapo, Uwazi likamtafuta Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova ambaye alisema:

“Alex Massawe anaendelea kusakwa, Interpol inamfuatilia kila kukicha. Atanaswa tu.”
Aidha, Kamanda Kova alitaka kujua jinsi inavyopatikana hiyo video ambapo alielekezwa na mwandishi wetu.

DCI AONGEA
Uwazi likamsaka Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Tanzania DCI, Isaya Mngulu na kumuuliza anasemaje kuhusu mtu huyo kudaiwa ni Alex Massawe kutanua Afrika Kusini ambapo alisema:
“Kwanza niko nje ya nchi. Lakini Massawe anafuatiliwa kwa karibu na Polisi wa Kimataifa (Interpol). Kwanza tayari yuko kwenye mazingira mazuri ya kumkamata, tena muda si mrefu.”

MASSAWE AMEFIKAJE HAPA?
Massawe na mfanyabiashara mwenzake, Abubakar Marijani ’Papa Msofe’ na mtu anayejulikana kwa jina la Makongoro Nyerere (si wa hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere) wanadaiwa kuhusika na kifo cha mfanyabiashara Onesphory Kituly mwaka 2012 nyumbani kwake, Magomeni Mapipa jijini Dar.

Papa Msofe na Makongoro wapo Gereza la Keko, Dar kwa kesi hiyo huku Massawe akiwa anaendelea kusakwa aunganishwe na watuhumiwa wenzake hao.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Israel:Tutajilinda na Hamas

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel inatakiwa kujiandaa kwa ajili ya mpango wa muda mrefu katika Gaza.
Hata hivyo ameelezea msimamo wake dhidi ya kundi la wapiganaji wa Hamas. Netanyahu amesema Hamas wanapaswa kusambaratishwa na hilo ndilo lengo la Israel.
‘Tulijua kuwa tungekuwa na siku ngumu, hii ni siku ngumu na ya maumivu kutokana na mashambulizi haya, nguvu na malengo vinatakiwa ili kuendeleza mapambano dhidi ya kundi hilo, anasisitiza Netanyahu.
Wizara ya afya ya Gaza imesema kuwa raia 10 wa palestina wameuawa katika shambulio la makombora yaliyolenga uwanja wa mpira yakitekelezwa na Israel..

Kati ya waliouawa katika shambulio hilo ni watoto saba waliokuwa wakicheza uwanjani hapo ambapo walipigwa na kufa papo hapo.

Hamas imeilaumu Israel kwa shambulio hilo,huku msemaji wa Israel akidai kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa bahati mbaya.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Monday, July 28, 2014

PICHA NA TAARIFA KAMILI ZA AJALI ALIYOPATA BAHATI BUKUKU.

   
Gari waliyokuwemo Bukuku na wenzake.

Usiku , muimbaji nyota wa nyimbo za injili, Bahati Bukuku pamoja na wasaidizi wake, walipata ajali akiwa njiani kuelea Kahama kwenye huduma. paparazi ilikuripoti taarifa za awali, na hapa tunakuletea picha kamili na taarifa rasmi ya jeshi la polisi mkoani Dodoma.

Juhudi za kumhamishia Bahati Bukuku kuelekea Muhimbili kama ilivyopangwa awali zimeshindikana, kutokana na kushindwa kugeuka wala kuinuka - akiwa amelazwa. Tayari ndugu na marafiki walishafika kutoka Dar es Salaam, na watu kadhaa wa Dodoma na viunga vyake walipita kuwajulia hali na kuwafariji.

Taarifa ya Jeshi la Polisi, Dodoma.
Gari lenye namba IT 7945 Toyota Nadia likiendeshwa na EDSON MWAKABUNGU (31) mkazi wa Tabata Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na kusababisha majeraha kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari jingine linalosadikiwa kuwa Fuso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 saa tisa alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO Wilaya ya Kongwa.

Waliojeruhiwa ni EDSON MWAKABUNGU ambae analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote, BAHATI BUKUKU (40) ambae ni mwimbaji wa nyimbo za injili na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mwingine ni FRANK CHRISTOPHER (20) mwimbaji pia wa nyimbo za injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam ambapo kapata michubuko usoni na mkono wa kulia.

Wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri ambapo Kamanda Misime amesema walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la Injili.

Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.


Frank amesafishwa kichwa na anaendelea vema. Muujiza wake ni kwamba nguo aliyokuwa amevaa ilichanwa na vioo, lakini yeye mwenyewe hajachubuka kutokana na vioo hivyo.

Picha hizi zilipigwa na Alpha, ambaye alitoka bila kuwa na majeraha kwenye ajali hiyo, wakati dereva, Eddy (Edson Mwakabungu) yeye ameripotiwa kuwa mguu umevimba, kiasi cha kulazimika kutoa jeans aliyokuwa amevaa.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya. 

CHANZO:paparazihuru.com

habari kamili :: read more...

UMEANGALIA PICHA ZA MREMBO VICTORIA KIMANI ZIKO HAPA ZICHEKI.

Ametokelezea Haswa HEEEEEEEEEEEEEEEEEEE; AYA macho kwako PICHA ZA AKIWA AMEJIANIKA ZAIDI BOFYA  HAPA

  SOMA NA HII

Binti afanyiwa mchezo mchafu chooni baada ya kulewa vibaya akiwa Night Club.

AU HII 

RIHANNA AJISAHAU NA KURUHUSU ALIWE MATE LIVE ETI ANASHEREHEKEA USHINDI WA UJERUMANI.




Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

MSICHANA ABAKWA HADI KUFA huko Area C mjini Dodoma.

 Kinamama walio karibu na familia ya marehemu Isabela Andrew aliyebakwa hadi kufa wakiangua kilio baada ya kushuhudia mahali mwili wake ulipokutwa huko Area C mjini Dodoma jana.


Mwili wa msichana huyo ulikutwa ukiwa umeharibika katika moja ya pagale, lililopo Area C, Dodoma Mjini na paparazi alishuhudia ukitolewa hapo kwa machela huku polisi wakiwahoji mashuhuda wa tukio hilo.

Dodoma. Mfanyakazi wa ndani, Isabella Andrew (18), amefariki dunia na kifo chake kikidaiwa kusababishwa na kubakwa na watu wasiojulikana.

Mwili wa msichana huyo ulikutwa ukiwa umeharibika katika moja ya pagale, lililopo Area C, Dodoma Mjini na mwandishi wetu alishuhudia ukitolewa hapo kwa machela huku polisi wakiwahoji mashuhuda wa tukio hilo.


Mkazi wa Mtaa wa Kiwanja cha Ndege, Jackson Coy aliyekuwa akiishi na binti huyo alisema msichana huyo alipotea tangu Jumamosi iliyopita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema mwili huo uliokotwa jana saa mbili asubuhi na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo chake.


Mwili huo ulibainika baada ya mama mmoja, Rehema Msambile kufika katika pagale hilo alipokuwa akifuatilia nyendo za mtoto wake ambaye juzi alipigwa kwa tabia ya utoro shuleni.


“Niliamua leo (jana) kumfuatilia, nikaanza katika mapagale.


Nilipofika hapa ndipo nikaona mwili wa marehemu ikabidi nimuite jirani hapo aje aone,” alisema.


Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Henry Kandenga alisema mazingira yanaonyesha kuwa binti huyo alibakwa kwa sababu walikuta nguo za ndani zikiwa pembeni.


“Hakuna yowe iliyosikika kwamba kuna mtu anauawa ukizingatia kwamba nyumba ziko jirani na hata nyumba aliyokuwa akiishi ni jirani na mahali alipokutwa,” alisema.


Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

WANAFUNZI WA CHUO WAFANYA UCHAFU HADHARANI, JIONEE MWENYEWE HAPA

 Madenti wa chuo kimoja town wamenaswa wakijiachia live bila aibu katika kile walichokiita kujipongeza baada ya kumaliza mitihani ya chuo maarufu kama UE.

Madenti hao ambao wanachukua masomo ya uinjinia ambayo ni magumu ajabu waliponda raha katika baa moja hapa town ambapo waliandaa pati waliyoiita pen  down party.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Thursday, July 24, 2014

MAZITO 10 YAIBUKA: VIUNGO VYA BINADAMU KUNASWA DAR!.




Lile sekeseke la viungo vya binadamu kukutwa kwenye dampo jijini Dar es Salaam limechukua sura mpya huku mambo mazito 10 yakiibuliwa na gazeti makini na lenye heshima kubwa, Amani.Wingu zito lenye viulizo vingi lilitanda Bunju B, Kinondoni jijini Dar, usiku wa Julai 21, mwaka huu baada ya watu kubainika kwa mifuko maalum ya Rambo ikiwa na viungo mbalimbali vya miili ya binadamu vikiwa vimekauka.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum  ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova.

Tukio hilo lilivuta hisia za wakazi wa Bunju na maeneo mengine ya Jiji la Dar na viunga vyake hivyo kusababisha minong’ono mingi huku baadhi yao wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina!
Kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kiliingia kazini tangu usiku wa tukio na kufanikiwa kugundua mazito hayo ambayo hayapatikani mahali popote zaidi ya kwenye gazeti hili.

WAHUSIKA
Habari za uhakika zinasema kuwa, viungo vya miili hiyo vilidaiwa kutoka katika Hospitali ya IMTU iliyopo Mbezi–Beach jijini Dar es Salaam ambayo ndani yake ina chuo cha utabibu.
Ilidaiwa kwamba, viungo hivyo vilikuwa miili kamili ambayo hutumika kwa ajili ya mazoezi ya udaktari kwenye vyumba vya upasuaji.

“Ni kawaida, vyuo vyote vinavyohusiana na udaktari huwa wanakuwa na maiti ambazo huzifanyia experiment (majaribio au mazoezi) ya surgery (upasuaji). Lakini pamoja na hivyo, huwa haitakiwi kuonekana baada ya kumaliza matumizi hayo,” anaeleza mmoja wa madaktari bingwa wa hospitali moja kubwa jijini Dar kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Baadhi ya viungo vya binadamu vilivyonaswa

Suala la Hospitali ya IMTU kuwa wahusika wa viungo hivyo halina ubishi, kwani hata Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum  ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova, juzi alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alithibitisha hilo.

IDADI YA MAITI
Akifafanua zaidi, Kamanda Kova alisema mpaka sasa haijajulikana viungo hivyo vilikuwa ni maiti za watu wangapi lakini uchunguzi bado unaendelea.

Alisema, jeshi lake lilikamata mifuko 85 iliyokuwa na viungo hivyo ikiwa ni vichwa, miguu, mikono, mapafu na mifupa ya sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.



VIUNGO VINGI VYA WANAWAKE
Uchunguzi umeonesha kwamba katika viungo hivyo ingawa havikuungana, sehemu kubwa ni vya wanawake. Hilo lilithibitika baada ya kuonekana kwa vipande vingi vya matiti ya wanawake.

KWA NINI VILIKUWA VIMEKAUKA?
Kwa mujibu wa daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (jina lipo), miili inayotumika kufanyiwa mazoezi na wanafunzi wa vyuo vya tiba hukaushwa ili isioze (cadevier). Lengo ni kuifanya idumu kwa muda mrefu ili wanafunzi mbalimbali waweze kufanyia mazoezi.

Habari za ndani zilizonaswa na Amani zinasema kuwa, daktari mmoja wa hospitali hiyo (jina tunalo) alipewa jukumu la kupeleka miili (siyo viungo) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili ikachomwe kwa sababu tanuri la kuchomea kwenye hospitali hiyo liliharibika.

Gari lililobeba shehena ya viungo vya binadamu

Inadaiwa pale Muhimbili aliambiwa atoe Sh. milioni nne, akarudi kazini kwake na kuweka mezani madai hayo ambapo uongozi ulimkabidhi kiasi hicho cha fedha.

“Yule daktari akatoka na miili kwenye lori, lakini badala ya kuipeleka Muhimbili, yeye aliwapa watu kaisi cha fedha ili wakaitupe dampo na kiasi kingine akatia ndani.

“Uongozi ulijua miili imekwenda kuchomwa Muhimbili mpaka habari za kuonekana kwa viungo dampo zilipoibuka wakashangaa. Lakini wanajiuliza wao walitoa miili mbona vimekutwa viungo? Jamaa naye katimka, hajulikani alipo,” kilisema chanzo kimoja hospitalini hapo.

MAITI ZINAPATIKANAJE?
OFM ilifanikiwa kugundua kwamba, miili ya kufanyia mazoezi kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya tiba  hupatikana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo si kosa la jinai. Kuna madai huuzwa kwa bei mbaya ambayo haikutajwa.

“Vyuo vyote vya utabibu kwa hapa Dar huchukua maiti kwetu. Ni Muhimbili pekee ndiyo wenye kibali cha kutoa maiti. Ni jambo la kawaida kabisa, tatizo ni kuonekana huko mitaani ikienda kutupwa, ule si utu na hata taaluma inakataa,” alisema mmoja wa madaktari wa Muhimbili akifafanua suala hilo.

SABABU ZA MIILI KUTOLEWA
Akifafanua zaidi, daktari huyo alisema: “Hata hivyo lazima niweke sawa, maiti zinazotolewa ni zile ambazo zimekaa hapa hospitalini kwa miezi mitatu (siku 90) bila kupata ndugu. Hospitali ikijiridhisha kuwa maiti haina mwenyewe basi huweza kutolewa.”

KWA NINI BUNJU?
Habari kutoka vyanzo mbalimbali vya OFM, zinaeleza kwamba tatizo si hospitali kumiliki viungo vile, bali ni kuonekana hadharani tena vikiwa vimerundikwa kama havikuwahi kuwa na nafsi.

“Lile gari lilikuwa linakwenda kutupa porini, which is not right (jambo ambalo siyo sahihi). Baada ya wanafunzi kumaliza mazoezi, miili hutakiwa kuteketezwa kwa dawa maalum iitwayo incinerator.

Mwananchi mmoja ambaye alijitambulisha kuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha IMTU aliandika kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa iliwahi kutokea miaka ya nyuma scenario (suala) kama hiyo ambapo mwanafunzi (hakutaja chuo) aliyeonekana na mkono (wa binadamu) mtaani of which (kitu ambacho) hairuhusiwi hata kutoka na gloves (glovu) nje ya chumba. Ishu ile ilileta mtafaruku mkubwa.

STORI YENYEWE
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, uchunguzi wa awali umebaini kuwa viungo vile vilitolewa IMTU na mpaka sasa wameshawakamata watu nane wakiwemo madaktari kwa upelelezi zaidi.

WIMBI LA WATU KUPOTEA DAR
Wakati huohuo, baadhi ya wananchi waliozungumza na Amani walionesha wasiwasi kuhusu kupatikana kwa viungo hivyo na wimbi la watu, hususan watoto kupotea kwa wingi jijini Dar katika siku za hivi karibuni huku baadhi ya ndugu waliowahi kupotelewa na ndugu wakiibua vilio upya wakiamini ni miongoni mwa viungo hivyo.



Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

MIAKA 2 YA NDOA; AUNT EZEKIEL AANZA KUSAKA MTOTO

MWIGIZAJI nguli katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel (pichani) anadaiwa kuanza kusaka mtoto ikiwa ni miaka miwili tangu afunge ndoa na Sunday Dimonte.

Muigizaji nguli wa tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel akipozi.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Aunt, siku si nyingi staa huyo atakwenda kuweka makazi ya muda kwa mumewe Dubai hadi atakapopata ujauzito.

Akizungumza na Amani hivi karibuni, rafiki huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe kwa kuogopa kusutwa na ‘matarumbeta’, alisema wengi wanadai mume wa Aunt yuko jela kwa hiyo ili kuwahakikishia kuwa kitu hicho hakipo ameamua aende kuishi Dubai kwa muda hadi atakaponasa ujauzito.

Aunt Ezekiel

“Kama mipango yake itakwenda vizuri, baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kupita ataondoka na safari hii atakaa sana Dubai hadi Mungu atakapomjalia kupata mimba ndipo atarejea Bongo. Lakini baadaye ataondoka tena kwani hata kujifungua amependa akajifungulie Dubai,” alisema rafiki huyo.
Baada ya kupata nyepesinyepesi hizo, Amani lilimtafuta Aunt na kufanikiwa kukutana naye uso kwa uso alipoulizwa alisema hapendi kuweka hadharani mambo yake na mumewe lakini kuhusiana na ishu ya kwenda kuishi Dubai, muda si mrefu ataondoka.

“Nadhani unajua kuwa mke na mume Mungu akiwajalia afya njema ni muhimu ndoa ijibu kwa kupata mtoto, sasa kuhusu kwenda kuishi Dubai ndiyo mipango yangu.
“Nataka kuwakomesha wale wanaodai kuwa mume wangu amefungwa! Sitaki kuwajibu kwa maneno, nataka kuwajibu kwa vitendo,” alitamba Aunt.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

BATULI ATESWA MBAYA NA DAWA ZA KULEVYA.

 MWANADAFADA kutoka Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa anaumia kuona listi ndefu ya Wabongo wanaosubiri kunyongwa nchi mbalimbali kwa kukutwa na dawa za kulevya.


Mwanadada kutoka Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ akipozi.

Batuli alisema kinachowaponza vijana wengi ni kupenda fedha za chapuchapu, matokeo yake wanaambulia kifungo cha maisha na wengine kunyongwa katika nchi zenye misimamo mikali.

“Inashangaza sana wasichana wanaingia katika biashara hii haramu, mbaya zaidi wanapoingiza madawa ya kulevya wanaharibu kizazi kilichopo, inaniuma sana maana vizazi na vizazi vinaendelea kuangamia,’’ alisema Butuli.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Rose Ndauka ameweka wazi kwamba kinachomfanya aishi vizuri na wenzake ni kutoendekeza makundi.

WIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka ameweka wazi kwamba kinachomfanya aishi vizuri na wenzake ni kutoendekeza makundi.

Mwigizaji wa sinema z

Akipiga stori na mwandishi wa gazeti hili, Rose alisema anampenda na atampenda mtu yeyote atakayekuwa tayari kuwa na urafiki naye kwa sababu hiyo ndiyo staili yake ambayo inamfanya hata wanaomchukia katika makundi hayo wampende.

“Nampenda kila mtu na nipo tayari kuwa na urafiki na mtu yeyote atakayekuwa tayari kuwa karibu na mimi, makundi hayana maana kabisa zaidi ya majungu tu,” alisema Rose.
a Kibongo, Rose Ndauka.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Wednesday, July 23, 2014

MAJANGILI WA WANYAMA PORI WANASWA.


Majangili waliokamatwa wakiwa chini ya ulinzi.Swala aliyeuawa na majangili hao.

WIMBI la majangili limeendelea licha ya kuwepo kwa ulinzi wa kutosha, kwa mara nyingine tena kwenye hifadhi ya Serengeti ikiwa ni siku mbili tangu kuondoka kwa mmiliki wa Singita Grumeti ambaye alikuwepo kwa wiki mbili kama ilivyo utaratibu wake wa kila mwaka.

Askari wake  wameendelea kukamata majangili ambapo usiku wa kuamkia leo wamewakamata majangili watatu wakiwa na swala.
 Swala aliyeuawa na majangili hao.




Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...
 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top