Tuesday, September 30, 2014

NILISHUHUDIA NIKICHOMWA MOTO.

  MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Richard Osward (40) mkazi wa Tabata Segerea, hivi karibuni alinusurika kuuawa kwa kuchomwa moto na wananchi baada ya kuhisiwa kuwa mwizi alipokutwa alfajiri akiwa na mfuko ambao ndani yake kulikuwa na bomba, huko Segerea.

Richard Osward aliyechomwa moto na watu wenye hasira kali akidhaniwa kuwa ni mwizi.

Akizungumza kwa shida akiwa katika wodi namba 23 iliyomo ndani ya Jengo la Sewa Haji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Richard alisema tukio hilo lilimkuta akiwa ameongozana na rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Moses na kwamba walikuwa wakielekea Gerezani, Kariakoo ambako wanajishughulisha na ufundi wa magari.

Akiuguza majeraha ya moto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Nilitoka nyumbani nikiwa nimebeba bomba katika mfuko nikitaka kwenda kuliuza, tulipofika Segerea Seminari, tulisimamishwa na watu ambao walitutilia shaka wakaanza kutupekua.

“Wakasema sisi ni wezi na hivyo lazima watuadhibu. Mara akapita dereva wa bodaboda ambaye alishinikiza kuwa sisi ni wezi na kutaka wachange hela wakanunue petroli ili watuchome moto, uzuri ni kwamba kwa kuwa ilikuwa usiku,wakashindwa kupata hayo mafuta,

lakini tunashukuru dada mmoja alikuja amevaa sare za kampuni moja ya ulinzi, akatukingia kifua na kusema watupeleke polisi na ndiyo tukafikishwa Kituo cha Polisi cha Stakishari na baadaye kunileta hapa kwa matibabu, kilichoniponza ni njaa lakini mimi ni mtu safi katika jamii, mwenzangu alifanikiwa kukimbia.”

WATOTO sita, wakiwemo wawili wa kiume wenye umri wa miaka 8 hadi 14 wameharibiwa vibaya sehemu zao za siri baada ya kubakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

ASKARI JWTZ AUAWA KWA RISASI NA WATU WASIOFAHAMIKA.

 NI taharuki iliyojaa majonzi na simanzi kufuatia Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ Kikosi cha CMTU jijini Dar kuondokewa na mpiganaji wake, Sajenti Yohana  Lugendo Gweso (40) ambaye alikuwa milionea aliyepigwa risasi sita mwilini na kufariki dunia papo hapo.

Mwili wa marehemu Sajenti Yohana Lugendo Gweso (40) wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ Kikosi cha CMTU ukiwa kwenye jeneza.
Tukio hilo la kusikitisha, lilijiri saa 1:45 usiku wa Septemba 22, mwaka huu, Ukonga Babana ndani ya baa maarufu ijulikanayo kwa jina la Super Karatu.

UWAZI HATUA KWA HATUA
Kufuatia tukio hilo, Uwazi kama kawaida yake lilifuatilia kwa kina ili kubaini yaliyofichika nyuma ya pazia kama siyo sirini!

Gari kubwa la jeshi lililoandaliwa kwa ajili ya kuuchukua mwili wa marehemu Sajenti Yohana  Lugendo Gweso kwenda Bunda kwa mazishi.

Habari zilizopatikana zilidai kuwa, siku ya tukio, marehemu Gweso alipigiwa simu akiwa njiani kurudi nyumbani kwake akitokea Hospitali ya Dar Group iliyoko Tazara jijini Dar.

Ikadaiwa kuwa, baada ya kupata simu hiyo alifika kwanza nyumbani kwake Gongo la Mboto kambini.
“Alipofika alikula chakula cha mchana kisha alipumzika. Ilipofika saa 11 jioni aliondoka kwenda kwenye shughuli zake za biashara. “Alipokuwa huko inadaiwa alipigiwa simu na mtu huyo wa mwanzo na kupanga sehemu ya kukutania ambapo ilikuwa  ni hapo baa,” alisema ndugu mmoja akiomba kusitiriwa jina lake.

Wanajeshi wa JWTZ wakiupandisha mwili wa Sajenti Yohana Lugendo Gweso kwenye gari.

AONDOKA NA NDUGU
Mpiganaji huyo inadaiwa wakati anatoka katika biashara zake alikuwa na mtoto wa dada yake aliyetajwa kwa jina moja la Frank ambaye alikuwa akisimamia hesebu zote za biashara. Siku hiyo walikuwa wamekusanya kiasi cha shilingi milioni 42.

Ikadaiwa kuwa, walipofika Banana kabla ya kuingia Baa ya Super Karatu, marehemu ambaye alikuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T 855 BWK, alimshusha Frank na kumtaka atangulie  nyumbani kwani alihitaji kwenda Super Karatu kukutana na mwanamke huyo ambaye baadhi ya watu wanadai ni mweupe, mnene aliyepanda hewani (mrefu).

Mjane (mwenye kilemba cheupe) wa marehemu Sajenti Yohana  Lugendo Gweso akisaidiwa na ndugu wa karibu kuingia kwenye gari lililoandaliwa kwa ajili ya safari.

AFIKA ENEO LA MAUAJI YAKE
Habari zaidi zinasema kuwa, marehemu aliwasili kwenye baa hiyo saa 1 usiku na kutafuta  maegesho. Alishuka na kuanza kutembea, lakini ghafla kwa  nyuma aliitwa na watu wawili ambao walimuita; “Gweso tuko hapa.”

Wakati anageuka kuwafuata watu hao, watu wengine walianza kuvunja gari lake vioo hivyo alirudi mbio ili kujua nini kinaendelea.

“Kumbe wau hao walikuwa kundi moja na mashambulizi ya risasi yalianzia hapo.
“Marehemu alimiminiwa risasi sita mwilini, alipigwa kichwani, nyingine kifuani na walimchukulia fedha zote milioni 42 na bastola yake kisha wakatokomea,” aliendelea kusema ndugu huyo.

Waombolezaji wakiingia kwenye gari kuelekea kwenye mazishi, Bunda.

MWILI WAKUTWA CHINI
Baada ya tuko hilo ndugu, jamaa na marafiki walijulishwa kuhusiana na kifo cha mjeshi huyo ambapo walifika na kuuchukua  mwili wa marehemu hadi Hospitali ya Rufaa ya Lugalo jijini Dar kwa ajili ya kuuhifadhi.

UTAJIRI WA MAREHEMU
Mpaka kifo chake, marehemu Gweso alikuwa akimiliki magari manne ya kisasa, Toyota Prado (alikuwa nalo siku ya tukio), Toyota Verossa, Suzuki Vitara na VRS.
Aidha, alikuwa akimiliki biashara mbalimbali kama vile baa, duka la bia za jumla na nyumba ya kulala wageni. Vyote vipo Ukonga, Dar.

Waombolezaji wakiuchukua mwili wa Sajenti Yohana  Lugendo Gweso kwa ajili ya mazishi.

Baadhi ya waombolezaji siku ya msiba walimtaja marehemu kuwa mwanajeshi milionea aliyehakikisha anapiga hatua kwa biashara kila kukicha.

ALIANZA KUWINDWA MWAKA 2008
Habari zaidi zinadai kuwa, marehemu alianza kuwindwa mwaka 2008 ambapo watu wasiojulikana majina, sura wala nia yao, walivamia nyumbani kwake, Banana (uswahilini) na kumpiga risasi mtoto wa dada yake na kufariki dunia papo hapo.

Sajenti Yohana  Lugendo Gweso enzi za uhai wake.

Inadaiwa watu hao waliamini mtoto huyo ni Gweso mwenyewe lakni yeye hakuwepo. Kufuatia tukio hilo, marehemu aliomba kuhamia kambini kwa usalama wake hadi kifo kilipomkuta hivi karibuni.

MAZISHI YAKE
Marehemu Gweso amezikwa Septemba 27,  mwaka huu katika Makaburi ya Kijiji cha Tailo Wilaya ya Bunda Mkoani Mara. Ameacha mke mmoja na watoto wanne.


MSANII SHILOLE APOROMOSHEWA MATUSI MARA BAADA YA KUWEKA PICHA TATA KWENYE MTANDAO WA KIJAMII.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

HAYA NDIO MAGALI MAWILI ALIYOPEWA WEMA SEPETU SIKU YA BERTH DAI YAKE.

 
Miss Tanzania 2006 ambae bado analinda jina lake lisipotee midomoni mwa watu Wema Abraham Sepetu, ameshangazwa na watu wake wa karibu kwa zawadi alizopokea.

Wema alipokea gari mbili ambapo moja alipewa na Mpenzi wake Chibu Dangote "Diamond Platnumz" aina ya Nissan Murano ipo kwenye hapo chini pamoja na BMW ambayo hii wengi hawakujua imetoka kwa nani lakini baadae ukweli umetambulika kwamba imetoka kwa Kaka Manager Martin Kadinda. Martin amemkabidhi Wema gari hilo pamoja na kadi ya Gari ikiwa imeandikwa jina lake.

 Hii ndio Nissan Murano aliyopewa na Diamond

Martin Kadinda akimuonesha Wema Sepetu kadi ya gari

Wema Sepetu baada ya kutoka nje na kuona gari hiyo

MSANII SHILOLE APOROMOSHEWA MATUSI MARA BAADA YA KUWEKA PICHA TATA KWENYE MTANDAO WA KIJAMII.



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Monday, September 29, 2014

TAZAMA PICHA ZA UTAMU ZILIZOVUJA ZA MREMBO HUYU WA CHUO KIKUU .

PICHA hIZO ZIMEONEKANA KUWACHANGANYA WANAUME WENGI SASA NA KUOMBA MAWASILIANO YA MDADA HUYO KWA HARAKA;
SASA SIJUI MWENYEWE KASIKIA  SNA SIJUI ATAZITOA SIJUI

KUONA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA


WATOTO sita, wakiwemo wawili wa kiume wenye umri wa miaka 8 hadi 14 wameharibiwa vibaya sehemu zao za siri baada ya kubakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

DIAMOND PLATNUMZ AMEMPA MPENZI WAKE WEMA SEPETU ZAWADI LEO KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA..!! ICHEKI HAPA

Hiyo ndo zawadi mdau na kisha akaandika maneno haya matamu kwa mpenzi wake wema sepetu
"Nlitama nikupe vingi, wenda ingenisaidia kueleza ni kias gani napenda nikuone ukifurahi kwenye siku yako hii ya kuzaliwa...lakini tu sina uwezo huo mumy??... tafadhari pokea kidogo hichi nlichojaaliwa leo..


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

ROSE NDAUKA MCHUMBA'KE WAACHANA! WANAUME FURSA KUTUPIA.


“Hiyo ndiyo habari ya mjini, bidada karudi kwao (Kigogo, Dar) na mwanaye. Ilikuwa ni lazima ndoa isiwepo kwani licha ya kupata mtoto hakukuwa na furaha hata kidogo.”
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini na cha uhakika kimemwaga data kwamba wachumba hao ambao walivalishana pete kwa mbwembwe miaka mitatu iliyopita huku wakipika na kupakua lakini wamekuwa katika mzozo wa muda mrefu wa kifamilia, ambapo mara kadhaa wameripotiwa kuchapana wameachana.
“Unajua hawa jamaa wamekuwa na maisha ya kutoaminiana sana, nadhani wivu ndiyo sababu kubwa, lakini naona safari hii hali imekuwa mbaya zaidi kwa sababu Rose  ameamua kubeba kilicho chake na kuondoka kwa mwenzake,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

TATIZO NI NINI?
Ingawa chanzo hicho hakikuweza kuingia kwa undani kuhusu tatizo hasa lililotokea safari hii, lakini kilibainisha kwamba kabla ya tukio la sasa, mzozo mwingine mkubwa uliibuka kati yao.
“Kuna kipindi hali ilikuwa tete sana, Malick akaamua kuchukua mabegi yake na kutokomea kusikojulikana ambako alikaa kwa muda wa kama wiki mbili.

“Haikujulikana alikuwa wapi kwa muda wote huo, lakini baadaye tukamuona jamaa anarudi na maisha yao yakaendelea.

NDOTO YA NDOA YAYEYUKA
“Lakini wakati bado mambo hayajatulia, kumeibuka tatizo lingine kubwa ambalo limesababisha Rose kuamua kuondoka huku ndoto ya ndoa ikiyeyuka,” kilisema chanzo hicho.

VIPI KUHUSU MTOTO?
Katika mtafaruku huo, Malick alikataa katakata mtoto wake kuondoka na mama yake, lakini kutokana na umri wa mwaka mmoja wa kijana wao huyo, Naveen, alilazimika kuondoka na mama yake kwa vile bado ananyonya.

Rose Ndauka wakati akiwa na mpenzi wake, Malick Bandawe

Rose, mmoja kati ya waigizaji warembo wa filamu Bongo, inasemekana kwamba yupo nyumbani kwa wazazi wake, Kigogo kutoka kwa mchumba wake, anayeishi Tandale, Tanesco jijini Dar.

IJUMAA WIKIENDA MZIGONI
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilizama mzigoni ambapo stepu ya kwanza ilikuwa ni nyumbani walikokuwa wakiishi wapenzi ambapo hawakuwepo.

JIRANI ANASEMAJE?
Akizungumza na gazeti hili juu ya kuondoka kwa Rose nyumbani hapo, mmoja wa majirani zake aliyejitambulisha kwa jina moja la Sudi alikuwa na haya ya kusema:
“Rose Ndauka ana muda hatumuoni kama miezi sasa lakini ‘mista’ tunamuonaona labda kama amehama ‘but’ sina uhakika sana.”

ROSE VIPI?
Katika kutafuta ukweli alitafutwa Rose kila kona baada ya simu yake ya kiganjani kutokuwa hewani lakini jitihada ziligonga mwamba hivyo zinaendelea.

BOFYA HAPA KUMSIKIA MALICK
Mchumba mtu, Malick alipoulizwa juu ya ukweli wa sakata hilo, alikiri kutokea na kwamba baada ya jitihada zake nyingi za kulinusuru penzi lao kushindikana, amekubali matokeo.
“Nimejitahidi sana kumwelewesha Rose ili apate kunielewa, ajue namna ya maisha yalivyo, lakini imekuwa ni kama kutwanga maji kwenye kinu. Nimekubali yaishe.

“Kinachonisikitisha sana ni kuona kuwa mwanangu anakwenda kulelewa na mwanaume mwingine, inauma sana tena sana,” alisema bila kufafanua maana ya kauli hiyo.
Katika uchumba wao mrefu, Rose na Malick wamejaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Naveen.

MCHUNGAJI ASHTUA KUMUOA DOGODOGO! MCHEKI HAPA.

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Sunday, September 28, 2014

HUYU NDIYE REDD'S MISS TANZANIA TOP MODEL 2014.


Mshindi wa taji la Redd’s Miss Tanzania Top Model 2014, Jihan Dimachk (katikati) akipozi kwa picha na mshindi wa pili Doreen Robert (wapili kulia), mshindi wa tatu Evelyn Baasa ambaye pia ni Miss Tanzania Photogenic 2014 (wapili kushoto), mshindi wa nne, Lilian Timothy (kulia) na Mshindi wa tano Nasreen Abdul, mara baada ya kushinda taji hilo jana ambapo Jihan amekuwa mrembo wa pili kuingia katika nusu fainali za Miss Tanania 2014 baada ya Miss Photogenic. Shindano la Miss Tanzania Top Mode lilifanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha na kuwashirikisha warembo 30..





HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Umeona Jumba la kifahari Diamond alilomjengea mama yake??? CHeki hapa.

kupitia akaunti yake ya Instagram Diamond ametupia picha ya ile nyumba aliyosema anamjengea mama yake. Katika picha hiyo aliambatanisha na maelezo haya "Had to visit mama Chibu's Village today.." Nyumba hiyo inaonekana ya kifahari hasa ukiangalia muundo na mabati yaliyotumika kujenga nyumba huyo.



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Kim Kardashian's butt got everyone thinking...

 Kim went shopping solo for baby North West,and as she stood by the cash counter, all eyes were on her massive butt which many say isn't proportionate with her thighs.. She has sworn they are natural, even carried out a scan on their reality show. See more pics after the cut: - See more at:


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

HIKI KIVAZI CHA JOKATE MWEGELO A.K.A KIDOTI NI SHIIIIDAH.

MWANAMITINDO na mtangazaji mahiri Bongo, Jokate Mwegelo amezua utata baada ya kupiga picha akiwa ametinga suruali iliyochanika.
Jokate Mwegelo akipozi na mzungu.
Akizungumzia picha hiyo ambayo imevuja katika baadhi ya mitandao, Jokate alisema alivalia mavazi hayo hivi karibuni Afrika Kusini alipokuwa amekwenda kurekodi wimbo wake mpya (hakuutaja jina) na alivaa makusudi ili kuonesha utofauti.

“Nimeamua tu kuwa tofauti maana hata watu wengi walikuwa wakijiuliza kulikoni mimi kuvaa hivyo  lakini mimi nafikiri lazima kuna wakati tunatakiwa kuonekana tofauti na siyo mapambo muda wote ukibadilika hata unachofanya unakuwa tofauti,” alisema Jokate.



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Saturday, September 27, 2014

MCHUNGAJI ASHTUA KUMUOA DOGODOGO! MCHEKI HAPA.

 
 MCHUNGAJI Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC lililoko Mbezi ya Shamba jijini Dar, amedaiwa kuoa mke wa pili aitwaye Pamela Didas Asenga akiwa na umri wa miaka 20 tu ‘dogodogo’, Risasi Jumamosi limetonywa.

Mchungaji Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC akimuoa 'dogodogo', Pamela Didas.

Kwa mujibu wa chanzo, ndoa hiyo ilifungishwa na Askofu Innocent Lugagi wa Kanisa la White House la Durban, Afrika Kusini, Agosti 29, mwaka huu.

Mke mwingine wa mtumishi huyo wa Mungu anaitwa Zuwena (Catherine) aliyemuoa mwaka 1985. Lakini kuna madai kwamba, mke huyo amemwacha.
Chanzo chetu ndani ya kanisa hilo kilidai kwamba, mchungaji huyo aliwaambia waumini wake aliamua kumuoa Pamela kwa vile ndoa yake ya mwanzo aliifunga akiwa  Muislam na alifungishwa na shehe (hakumtaja jina).

“Alituambia Mungu amemfunulia na amempa mke mwingine mwema ambaye ni binti mbichi, watu wewee,” kilisema chanzo.

Mchungaji Peter Rashid Abubakari akiwa mke mpya.

Habari zaidi zinasema kuwa, mchungaji huyo baada ya kutua nchini, Jumapili moja akiwa kanisani kwake aliwatangazia waumini wake, hasa wanaume kwamba kama wana wake ambao walichukuana wakati wa ‘ujinga’ na wamekaa nao kwa miaka mitatu au zaidi na hawana tabia ya Kimungu, mkorofi na mchokozi na hawajafunga nao ndoa, wawaache ili Mungu awape wake wema.
Sasa baada ya picha za mtumishi huyo kusambaa hadi kwenye mitandao, Risasi Jumamosi, juzi lilifika kanisani kwake Mbezi ili kuzungumza naye lakini hakuwepo.

Mchungaji Peter Rashid Abubakari akiongoza maombi kanisani.

Baadhi ya waumini walioweza kuzungumza na Risasi Jumamosi walionesha kushtushwa na kitendo cha mchungaji wao kumuoa Pamela lakini hawakuwa tayari kusema neno!
Baadaye mwandishi wetu alimtafuta mchungaji huyo kwa njia ya simu ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Nipo Kiluvya kikazi lakini hilo lipo ila ni jambo langu binafsi siyo la kulitangaza.”
Baadaye alimtumia ujumbe  mwandishi akiwa ameuandika hivi:
“Sanchawa mimi ni Nabii wa Mungu Yehova, uliponipigia tu kila kitu Mungu akaniambia nia yako na kusudi lako.”

Mchungaji Peter Rashid Abubakari.

Pia Risasi Jumamosi lilizungumza na baadhi ya wachungaji wa makanisa ya kiroho Tanzania ili kuwasikia wanasemaje kuhusu kitendo cha mtumishi huyo kufunga ndoa nyingine.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao magazetini, baadhi ya wachungaji hao walimpongeza Mchungaji Peter kwamba, aliona alikokuwa na anakokwenda ndiyo maana aliamua kuchukua uamuzi huo.

UNYAMA ULIOKITHIRI: MWANAFUNZI WA MIAKA 14 ATEKWA NA KUBAKWA JIJINI DAR..ASHINDWA KUMALIZIA MTIHANI WA DARSA LA SABA.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Thursday, September 25, 2014

UNYAMA ULIOKITHIRI: MWANAFUNZI WA MIAKA 14 ATEKWA NA KUBAKWA JIJINI DAR..ASHINDWA KUMALIZIA MTIHANI WA DARSA LA SABA.

 HUYU NI MWANAFUNZI MWENYE UMRI WA MIAKA 14, ALISHINDWA KUFANYA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA SABA 2014 KWA SIKU YA PILI TATEHE 11 SEPTEMBA HAPA JIJINI DAR ES SALAAM BAADA YA KUTEKWA NA MWANAUME NA KUMFUNGIA NDANI KWAKE NA KUMBAKA NA KUSABABISHA MWANAFUNZI HUYO AMBAYE NI MTOTO KUTOMALIZA MTIHANI WAKE WA MWISHO.....HATA HIVYO MTUHUMIWA AMESHIKILIWA NA POLISI TANGU TAREHE 11SEPT NA HAJAFIKISHWA MAHAKAMANI....

.MWANAFUNZI HUYO ANALIA SANA

CHANZO:SAM MAHELA

Check out mother and daughter who are Lesbian Partners.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

HAWA NDIO MABINTI WA MARAIS WA AFRIKA WANAOTIKISA MITANDAO YA KIJAMII KWA PICHA ZAO KUANGALIWA ZAIDI HASA MAMEN.


SAFU hii mpya itakuwa yakutoa elimu kwa wasomaji. Wiki hii tunaanza na baadhi ya mabinti wa marais wa Afrika ambao wanatikisa sana katika mitandao mbalimbalikutokana na sifa zao tofauti

AngePaul Kagame

Ni binti wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame. Alizaliwa mwaka 1989. Kwenye mitandao amekuwa akisifiwa kuwa ni ndiye binti mrembo kuliko wengine.

Faith Sakwe Jonathan

Huyu ni mtoto wa Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan. Amefunga ndoa Aprili, mwaka huu. Naye anatajwa na mitandao kwamba ni mrembo.

Nyepudzayi Bona Mugabe

Ana miaka 24. Ni binti wa Rais wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe. Ni binti aliyetikisa mitandaoni kutokana na mambombalimbali ya kijamii. Amefunga ndoa hivi karibuni

Sifa Joseph Kabila
Amezaliwa mwaka 2001, baba yake ni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila. Anatajwa kuwa binti mtulivu na msikivu.

Ngina Uhuru Kenyatta

Mwaka huu amekamata wa 23, baba yake ni Rais wa Kenya, Uhuru Jomo Kenyatta. Mitandao inamtaja kwamba ana mvuto, pia anaongoza kwa kuwa na marafiki wengi wa kike.

Stella Mutale Sata
Baba yake ni Rais wa Zambia, Mutale Sata. Binti mwenyewe yupo poa sana kwa sasa ana miaka 20 tu.

Diana Karuguire Museven

Ni binti wa Rais wa Uganda, Joel Kaguta Museven. Amefunga ndoa. Mitandao inamtaja ni binti aliyetulia ndiyo maana akapigwa jicho na mwanaume na kufunga ndoa.

Girl aged 14 raped in school toilets after teachers' plan to 'use her as bait' backfires in US.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

DIAMOND AMTOA MACHOZI MENINAH; WEMA AMSAKA KILA KONA AMFUNDISHE ADABU.


YALE madai kuwa sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem ya kutaka kuolewa na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yamemtoa machozi mwanadada huyo.

Sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem.

Hivi karibuni Meninah na Diamond walizua na bado wanaendelea kuzua mjadala kila kukicha ambapo taarifa juu ya wawili hao kutaka kufunga ndoa ya chinichini zinaendelea kusambaa kwa fujo ambapo mwanadada huyo amelonga na Amani kwa dakika kumi.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kikizungumza kwa kujiamini, chanzo makini ambacho kiliomba hifadhi ya jina kilidai kwamba hakuna ndoa tena kati ya Diamond na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na kwamba ndoa inayopangwa kwa sasa ni ya Meninah na Diamond.

Chanzo hicho kilinyetisha kwamba wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za Kili mwaka 2014 na tangu hapo wamekuwa na ukaribu unaodaiwa unataka kuzaa ndoa.

WEMA AMWINDA
Ilisemekana kwamba baada ya Wema kuzinyaka habari hizo kuwa anataka kunyakuliwa ‘beibi’ wake mbaya zaidi wanataka kufunga ndoa, malkia huyo mkubwa wa sinema Bongo aligeuka mbogo na kuanza kuweka mikakati ya kumteketeza Meninah asiweze kufunga ndoa na Diamond.

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Kuna madai kwamba Meninah aliposikia Wema anamsaka usiku na mchana ili amshikishe adabu, msanii huyo alishtuka kwa kuwa anaujua vizuri ‘mziki’ wa staa huyo.

VIKAO VYA HARUSI VYAFANYWA
Taarifa ziliendelea kudai kwamba, vikao vya harusi vya chinichini vinaendelea kufanywa huku wahudhuriaji wakiwa ni mdogo wa Diamond ambaye pia ni mwanamuziki, Mwanahawa Abdul Juma ‘Queen Darlin’ pamoja na baadhi ya ndugu wa upande wa mama Diamond ambao wamekuwa wakifanya kila wawezalo kuhakikisha ndoa hiyo inafungwa.

POMBE NA STAREHE VYATAJWA
Sababu kubwa inayosemekana Wema kutemwa kuolewa na Diamond ni kutokana na kuendekeza pombe na starehe jambo ambalo Meninah yupo nalo kando na kwamba hivi sasa amekuwa akitimba kwa mama Diamond bila wasiwasi huku akizama jikoni kupika, kupakua na kufanya kazi ndogondogo za ndani ili kuthibitisha kuwa yeye ni mama bora.

DIAMOND AMTOA MACHOZI
Baada ya kunyaka madai hayo, Amani lilimsaka Meninah na kumhoji juu ya sakata hilo la kutaka kuolewa na Diamond ambapo alikuwa na haya ya kusema:

Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu.

“Yaani sijui hata nianzie wapi kuzungumzia hili la kutaka kufunga ndoa na Diamond, naomba niseme ukweli kwamba nashangaa, kwanza sijui chochote, nimekuwa nikiandikwa mara kwa mara lakini taarifa hizo wala hazina ukweli wowote.

“Mimi na Diamond ni tofauti kabisa, sijawahi kuwa na ukaribu naye. Kwanza naumia sana na kutokwa na machozi kuendelea kusikia taarifa hizi kuwa naolewa naye kitu ambacho hakipo kabisa, hata yeye mwenyewe akisikia hivi anaweza kumtafuta mtu ambaye anasemwa kuwa anatoka naye jambo ambalo si la kweli.”

“Wema namheshimu kama dada yangu, mtu ninayemjua kwenye tasnia ya filamu Bongo, kwanza wote tunafanya sanaa japokuwa kwa upande wake anafanya filamu na mimi muziki. Hizo taarifa juu ya kuniwinda sijui na sijazisikia. Kiukweli zimenishtua sana.”

Diamond alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo hakupatikana kwa kuwa alikuwa ziarani barani Ulaya.TUJIKUMBUSHE

Kwa wiki kadhaa sasa, Meninah na Diamond wamekuwa wakihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

16-year-old girl tells story after she got impregnated by her father.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

Tuesday, September 23, 2014

LAANA:TAZAMA PICHA ZA UTAMU ZA MWANAFUNZI HUYU WA CHUO.


PICHA ZAKE NI MBAYA SANA KIASI CHA KUSHINDWA KUKAA HAPA

KAMA UNAZITAKA BOFYAaaaaa HAPO CHINI

HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

MSANII SHILOLE APOROMOSHEWA MATUSI MARA BAADA YA KUWEKA PICHA TATA KWENYE MTANDAO WA KIJAMII.

yaani kiukweli siku ya leo ndio nimeamini kuwa staa hususan katika nchi kama hii yetu wanakazi sana leo imemtokea mwanadada shilole mara tu baada ya kupost picha yake iliyopo hapo juu kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kuporomoshewa matusi

KUONA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA

POMBE NI NOMAAAA; WAZUNGU WABAKWA BAADA YA KUFAKAMIA POMBE.

PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

habari kamili :: read more...

WAMAREKANI WAFUNGA NDOA KATIKA MLIMA KILIMANJARO.




 Kara Lee akimlisha keki mumewe Richard Miller mara baada ya kufunga ndoa katika Mlima Kilimanjaro juzi.

RAIA wa Marekani Richard Miller na Kara Lee wamefunga ndoa ya kihistoria katika Mlima Kilimanjaro juzi na kuacha watu midomo wazi.

Kara Lee akimvisha pete mumewe Richard Miller.

Wanandoa hao waliwasili nchini wiki iliyopita na kuanza safari yao ya siku saba kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia njia ya Machame Septemba 20, 2014 na kutumia usiku huo katika banda la Machame.

Kara Lee anasimulia hivi: “Katika Sikukuu ya Krismas huko Minnesota nchini Marekani tulivishana pete mimi na mchumba wangu Richard Miller na kuwekeana ahadi kuwa ndoa yetu lazima ifungwe juu ya paa
la Afrika na hiyo sehemu si nyingine zaidi ya Mlima Kilimanjaro”.

Wanandoa hao wakisaini kitabu cha maharusi.

Baada ya hapo, wawili hao walianza mipango ya kutimiza ndoto yao hiyo ya pekee na ya kihistoria kwa kukusanya fedha kwa ajili ya safari yao kuja Tanzania. Wapenzi hao waliwajulisha ndugu na jamaa juu ya uamuzi wao huo ambapo walipata baraka zote za kutimiza ahadi hiyo.

Safari yao ya kupanda mlima huo ilikuwa ikiongozwa na Kampuni ya Utalii ya Zara iliyopo mjini Moshi, Kilimanjaro ambapo Septemba 21 mwaka huu majira ya saa 6 mchana wawili hao waliwasili katika pango
la Shira wakitokea banda la Machame wakiwa pamoja na wenyeji wao tayari kwa ndoa yao hiyo iliyokuwa gumzo kwa watu waliohudhuria.

Mchungaji Aloyce Mbugi kutoka Kanisa la TAG la Victory Christian Centre lenye makazi yake jijini Arusha akiwafungisha ndoa Kara na Richard.

Siku hiyo ya Jumapili, Septemba 21, 2014 Mchungaji Aloyce Mbugi kutoka Kanisa la TAG la Victory Christian Centre lenye makazi yake jijini Arusha alianza ibada ya kuwafanya kitu kimoja Richard Miller na Kara Lee kama mume na mke.

Maharusi hao wakisimamiwa na Ansigar Mtandika na Neema Njau, walianza kula viapo vya ndoa pamoja na kuvishana pete mbele ya mchungaji huyo huku wakiahidi kuwa pamoja katika shida na raha mpaka Mwenyezi Mungu atakapowachukua.

Wanandoa hao katika pozi baada ya kufunga ndoa.

Baada ya zoezi hilo, wanandoa hao walikunywa shampeni pamoja na waalikwa waliohudhuria tukio hilo la kihistoria na kuhitimisha ndoa hiyo iliyofungwa kwa saa tatu.

Richard na Kara walianza maisha ya mke na mume katika hema na leo wameendelea na safari yao ya kuupanda mpaka kileleni Mlima Kilimanjaro ambapo wamefika kituo cha Baranco. Wanandoa hao
wanataraji kufika kilele cha mlima huo kesho Jumatano na wataanza kushuka kuelekea geti la Mweka Keshokutwa Alhamisi ya Septemba 25, 2014.

“Wana nguvu na wamepania kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro na naamini watatimiza ndoto yao nyingine hiyo," alisema Teophil Karia, mwongoza wageni kutoka Zara Tours.

WATOTO sita, wakiwemo wawili wa kiume wenye umri wa miaka 8 hadi 14 wameharibiwa vibaya sehemu zao za siri baada ya kubakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

PICHA / HABARI: KWA HISANI YA FIKRA PEVU
habari kamili :: read more...
 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top