Monday, June 30, 2014

Mme wa mtu azua timbili na kahaba baada ya kudaiwa kushindwa kulipa kiasi chote cha pesa walichopatana.

 Watu waliokuwa kwenye baa jirani na eneo mzozo ulipotokea walikuja kumnusuru jibaba huyo ambaye alifyatuka mbio misili ya farasi baada ya kuokolewa kutoka mikononi mwa Jidada hilo.

Jidada hilo likitulizwa na wasamalia wema baada ya Mzozo.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Kenyatta University warns students with bad behavior they are doing in bathrooms.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Hii hapa Profile ya Refarii Mkenya anayepuliza kipenga huko Brazili kwa sasa katika World Cup 2014.

Marwa is one of the three referees from Eastern and Central Africa region picked to officiate during the world football showpiece.
The others are Rwanda’s Felicien Kabanda and Jean-Claude Birumushahu from Burundi.
Selected after an impressive performance, Marwa, thus becomes the first Kenyan referee to be selected to officiate at the Fifa World Cup.
A teacher by profession, the 36 year old whistler won KPL’s top award in 2011 and 2013.
Marwa officiated last year’s African Champions League final between Egyptian giants, Al Ahly against South African-side Orlando Pirates.
He was a match official in both the 2012 and 2013 Africa Cup of Nations finals held in South Africa and Gabon respectively.
The Kuria-born referee also officiated in the FIFA Under 20 World Cup held in the United Arab Emirates late last year.
The Fifa Referees Committee announced on its website that it has put in place a comprehensive program to ensure referees are in peak condition before the World Cup kicks-off.
“Just as it did for the 32 participating teams, the road to the 2014 Fifa World Cup began with an initial group of 52 referees from all over the world in September 2011 when Fifa took the important decision to create a refereeing project.
“One of the key objectives was match control and consequently to prepare this group of prospective referees for the 2014 Fifa World Cup,” said a statement from Fifa.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Binti wa darasa la 7 alawitiwa na Vijana watatu huko Pwani, Mlezi wake apewa laki mbili kama kifunga Mdomo.

Denti wa kike wa darasa la saba anayesoma katika Shule ya Msingi Chanzige B iliyopo Kisarawe, Pwani aliyefanyiwa unyama wa kulawitiwa na vijana watatu.

INASIKITISHA sana! Denti mmoja wa kike wa darasa la saba anayesoma katika Shule ya Msingi Chanzige B iliyopo Kisarawe, Pwani amejikuta katika wakati mgumu baada ya kulawitiwa na kusababishiwa maumivu makali sehemu zake za siri.
Simulizi ya binti huyo inayouma sana, inaeleza kuwa denti huyo alifanyiwa unyama huo na vijana watatu ambao bado hawajafahamika majina yao mara moja lakini amekuwa akimtaja mmoja kwa jina la Musa.
Tukio hilo lenye sura ya majonzi hasa kwa wazazi na watoto, lilitokea hivi karibuni Kisarawe mkoani Pwani lakini ilifanywa siri kwa muda mrefu na mtoto huyo kukaa bila matibabu.
Chanzo chetu cha habari kinasema kuwa, shangazi wa mtoto huyo ambaye anaishi naye ndiye sababu ya kutopata tiba, kwani anadaiwa kuchukua kiasi cha shilingi 200,000 kutoka kwa Musa anayetajwa kuwa mmoja wa wahusika kama kifunga mdomo.

“Haya mambo yametokea muda tu na huyo mtoto (anamtaja jina lakini linahifadhiwa) alimwambia shangazi yake kuwa huyo Musa na wenzake wanahusika, lakini cha ajabu walikutana huko na kupeana hizo fedha ili mambo yaishe.
“Hii haikubaliki kabisa. Unajua huyo shangazi mtu anafanya hivyo kwa sababu si mwanaye, ingekuwa ni damu yake kweli asingeweza kufanya kitu cha namna hiyo,” kilipasha chanzo hicho na kuongeza:“Ilibaki kidogo mtoto ashindwe kufanya mtihani wake wa Mock kwa sababu ya tukio hilo. Kiukweli si jambo la kulifumbia macho. Huyo mama (shangazi) anatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria.”

Chanzo hicho kikazidi kusema kuwa, awali kesi hiyo ilifikishwa katika Kituo cha Polisi Kisarawe na kufunguliwa jalada lakini shangazi wa mtoto huyo aliamua kuyamaliza mambo hayo na mmoja wa watuhumiwa baada ya kupewa kiasi hicho cha fedha.
Uchunguzi wa Amani umegundua kuwa, sakata hilo liliripotiwa katika Kituo cha Polisi Kisarawe na kufunguliwa jalada nambari KIS/RB/326/2014, ambapo Fomu ya Polisi Nambari 3 (PF3) ilitolewa kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo.

Akisimulia zaidi, mama mzazi wa mwanafunzi aitwaye Mariam Said alisema, alipata taarifa za mwanaye kukumbwa na masahibu hayo ambapo aliamua kusafiri kutoka Mlandizi anapoishi hadi Kisarawe kufuatilia tukio hilo.

“Inaniuma sana mwanangu kufanyiwa unyama halafu mambo yanamalizwa kienyeji. Nilikuja hadi hapa, nikamwuliza shangazi yake na binti yangu juu ya tukio hilo, akakiri lakini akasema eti mwanangu hakuwa mkweli mapema.
“Nikaamua kwenda polisi mimi na ndugu zangu wengine. Tulipouliza hiyo kesi kituoni hapo, tukaambiwa ni kweli ilifungiliwa na nikatajiwa RB (ile iliyoandikwa hapo juu). Polisi wakatuambia, walishangaa kuona mlalamikaji harudi tena na hata PF3 waliyotoa haikurudishwa tena baada ya kuondoka,” alisema Mariam.

Binti huyo alisema alifanyiwa ukatili huo wakati akitokea shuleni na kwamba alimweleza shangazi yake kila kitu kuhusiana na tukio hilo kabla ya kwenda naye polisi kutoa taarifa.
“Baada ya hapo tulikwenda katika Hospitali ya Kisarawe lakini sikupata matibabu kwa sababu shangazi alisema hana pesa ya malipo, kukarudi nyumbani na kununua dawa kwenye maduka ya dawa,’’ alisema mtoto huyo na kuongeza:
“Pale hospitalini, shangazi alitakiwa kutoa kadi ya Bima au shilingi 10,000 ili nitibiwe. Sasa hakuwa na Bima wala hiyo pesa ndiyo maana ikashindikana.”


Gazeti hili lilifunga safari hadi Shule ya Msingi Chanzige B na kuzungumza na Mwalimu Mkuu, Issac Eliah ambaye alikiri kupokea taarifa ya mwanafunzi wake kubakwa na kulawitiwa kutoka kwa shangazi wa mtoto huyo na kutoa ruhusa kwa ajili ya matibabu.
Shangazi wa mtoto huyo alipotakiwa kuzungumzia ishu ya kuzima kesi hiyo kwa madai ya kupewa shilingi 200,000 alisema: “Mimi sitaki kuzungumzia suala hilo, nendeni polisi mkaulize siyo kuniuliza mimi.”
Chanzo:http://mdadisibongo.blogspot.com/

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

(+18)DENTI WA CHUO AVUJISHIWA PICHA ZA UTUPU, BAADA YA KUJISAHAU NA KUMPA JAMAA FLASH YENYE GROUP WORK.

denti mmoja wa chuo kimoja ambacho tusingependa kukitaja jina kwa kuhofia maadili, amejikuta akipata aibu ya mwaka baada ya picha zake za faragha kusambaa kwa kasi ya ajabu mtandaoni , denti huyo anayesoma masomo ya biashara inadaiwa alikusanya kazi ambayo waliachiwa na mwalimu wao sasa kwa bahati mbaya alisahau kuzifuta kwenye frash na ndipo zikasambaa, hapo
haijajulikana bado zimevujishwa na nani kati ya mwalimu au huyu jamaa tunayekusanya kazi kwake hili ampelekee mwalimu alizungumza rafiki wa karibu wa denti huyo,akome kwani amezoea amewahi kupiga zingine bhana unabisha?

 hivi sasa rafiki yangu. hasomi amechanganyikiwa anahofia siku baba yake atakapoziona picha hizo kwani anasema ni mkali mpaka anamuogopa, jamani ushauri tu mabintimsijiachie sana na camera zitawaponza kama huyu dada, ni hayo tu
KUZIONA PICHA CHAFU HIZO BOFYA HAPA 


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Rais wa Uruguay atukana maafisa wa FIFA kwa kuwaita "Watoto wa Mbwa" Je naye ataadhibiwa?

Rais Jose Mujica amesema maafisa wa FIFA wamuadhibu Suarez kwa unyonge wake

Rais wa Uruguay Jose Mujica amewatukana maafisa wa FIFA kwa kuwaita ''kundi la watoto wa Mbwa'' au "a bunch of old sons of bitches".

Hii ni baada ya maafisa wa shirikisho hilo kumpiga marufuku mchezaji wa nchi hiyo Luis Suarez.

Mchezaji huyo aliitaja adhabu hiyo ya marufuku ya miezi minne ikiwemo kutocheza mechi 19 za kimataifa kama adhabu ya kinazi.

Suarez alipata adhabu hiyo ambayo inasemekana kuwa kali sana kuwahi kutolewa katika hoistoria ya kombe la dunia kwa kumuua mchezaji wa Italia Giorgio Chiellini.

Rais Mujica anasifika kwa kutotafuna maneo yake pamoja na ukali wa matamshi yake.

Aliyatoa matamshi yake kupitia televishini ya taifa alipokuwa anawapokea wachezaji wa timu hiyo baada ya kubanduliwa nje ya michuano ya kombe la dunia katika awamu ya muondoano.

Rais huyo alifunika mdomo wake kwa mshutuko wa kile alichosema , lakini wandishi wa habari tayari walikuwa wamemrekodi.Pia aliwaambia kuyachapisha matamshi yake alipohojiwa ikiwa alitaka kujirekebisha.

Rais huyo alisema kuwa FIFA ilimuadhibu Suarez kwa sababu ya maisha yake ya zamani ambayo yalikuwa ya unyonge.

Pia alitaja adhabu hiyo kama aibu kubwa sana kwa historia ya FIFA.

HABRI ZAIDI JUU YA MATAMSHI HAYO BOFYA HAPA


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

18+ PATA MAUJANJA HAPA ;JINSI YA KUSHIKA MIMBA HARAKA.

1. Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, angalau siku tatu kwa wiki, ikiwezekana on alternate days.
2. Tumia ovulation prediction kit, hiki ni kifaa ambacho kitakusaidia kujua wakati hasa mwanamke ameengua yai na ndio kipindi ambacho mwanamke ana uwezo wa kushika mimba akikutana na mumewe. Ni rahisi kutumia.
3. Fanya tendo la ndoa kabla ya kuengua yai (kabla ya ovulation), huongeza uwezekano wa kushika mimba kuliko kusubiria ovulation au kufanya baada ya ovulation.
Kutaneni siku mbili au tatu kabla ya ovulation. Ukitumia ovulation test kit, mkutane kuanzia siku itakapokuwa positive kwani huwa inapredict ovulation kutokea 48 hrs after it tests positive.
4. Usitegemee njia ya kalenda kutabiri uenguaji yai, njia hii kwa kiasi fulani huweza kuwasaidia wale wenye mzunguko wa siku 28, lakini pia haina uhakika wa 100%, wengi wa wanawake hawaengui yai siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, kwa hiyo kutegemea kalenda kutakuchelewesha kupata ujauzito.
5. unapotaka kushika mimba, acha au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya.
6. unapotaka kupata mimba, tendo la ndoa liwe kitu 'enjoyable' na sio tendo 'mechanical' kwa ajili ya kutafuta mtoto.
7.Kufanya mapenzi katika mtindo (style) ambayo itafanya mbegu za kiume zikae kwa muda mrefu ukeni na hivyo nyingi kupanda kuingia kwenye kizazi na kwenda kurutubisha yai.
'missionary position' ni nzuri zaidi, ambapo mwanaume anakuwa juu, epuka positions za mwanamke kuwa juu kwani hufanya mbegu zimwagike kwa gravity. Jaribu pia kuweka mto chini ya kiuno ili kukiinua na kufanya mbegu ziingie ndani kwa urahisi zaidi.
Kumbuka kuna asilimia 10 - 25 ya couples ambazo zina matatizo ya infertility lakini vipimo havionyeshi tatizo, inaweza kuwa namna ya kufanya mapenzi ndio ikawa shida, jaribu njia hizo 7 juu.
Kama hizi njia hazijakusaidia basi utakuwa na matatizo na unaweza kumuona daktari kwa msaada wa vipimo na matibabu. Natumaini uzi huu unaweza kuwa msaada kwa watafutao watoto.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

BABY MADAHA HAISHIWAGI JIPYA SASA KAJA NA HII: SIOLEWI KWA KUFUATA MKUMBO.

 ‘Baby Madaha’ akiwa kwenye pozi.

STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amesema anaishi katika staili ya kivyake hivyo kamwe hawezi kuolewa kwa kufuata mkumbo kama ilivyo kwa wasanii wengine.

Staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’
Akipiga stori na paparazi, Baby Madaha alikiri kuwa ana mchumba ambaye ni Joh Kairuki, anampenda sana ila katika suala la kufunga ndoa bado yupoyupo sana kwa sababu haolewi kwa kufuata mkumbo kwani amejifunza kupitia kwa walioolewa na kuachika.
“Nitaolewa nitakapokuwa tayari siyo kwa kufuata mkumbo vinginevyo bora nibakie hivihivi kwa sababu pesa kwangu ndiyo kila kitu, mambo mengine yanafuata,” alisema.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius hakuwa na tatizo lolote la kiakili wakati alipomuua mpenzi wake.

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius hakuwa na tatizo lolote la kiakili wakati alipomuua mpenzi wake mwaka jana.

Haya ni matokeo ya uchunguzi wa kiakili aliofanyiwa Oscar Pistorius huku kesi yae ikianza kusikilizwa tena nchini Afrika Kusini.Ripoti hiyo iliwasilishwa baada ya uchunguzi kufanywa kuhusu hali yake ya kiakili wakati alipofanya mauaji hayo mwaka jana.

Mawakili wake walikuwa wamedai kuwa Pistorius aliukuwa anakumbwa na hali ya wasiwasi na kuzongwa na mawazo wakati wa mauaji ya Reeva Steenkamp.

Mwanariadha huyo amekana kumuua kwa maksudi mpenzi wake Reeva Steenkamp akisema kuwa alimpiga risasi kwa bahati mbaya baada ya kupatwa na wasiwasi akidhani jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.

Upande wa mashitaka pamoja na utetezi wamekubali matokeo ya uchunguzi huo.

Upande wa utetezi sasa unasikia ushahidi wake daktari aliyemkata miguu Pistorius, Gerry Versfeld, anayetoa ushahidi kuhusu athari za Pistorius kukatwa miguu.

Upande wa utetezi nao unatarajiwa kumaliza ushahidi wake katika siku chache zijazo.

Bi Steenkamp, alikuwa na umri wa miaka 29, wakati wa mauaji yake Februari mwaka jana.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Evans Elieza Aveva ashinda Uraisi wa Simba SC.


Evance Aveva akishukuru baada ya kutangazwa kuwa Rais mpya wa klabu ya Simba na kuchukua mikoba ya Ismail Aden Rage, aliyemaliza muda wake wa miaka minne.
Amin Bakhresa akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Simba SC.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe jana aliokoa jahazi baada ya kutoa Sh. milioni 20 na kuwezesha kufanyika kwa mkutano mkuu wa uchaguzi wa uliomweka madarakani Evans Aveva.

Hanspoppe alitoa fedha hizo ili kugharamia uchaguzi baada ya kampuni ya bia Tanzania (TBL), ambao ndiyo wadhamini wa klabu hiyo ambao waliahidi kugharamia mkutano huo kushindwa kufanya hivyo kwa wakati.



Habari za ndani zilidai kwamba, rais aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage alitaka uchaguzi usifanyike kutokana na wadhamini kutotoa fedha hizo.

Hata hivyo, uchaguzi huo uliohudhuriwa na wanachama 2,501 ulifanyika kama ilivyotarajiwa huku Aveva akionekana kukosa upinzani kutokana na kuenguliwa na Kamati ya Uchaguzi kwa aliyekuwa mpinzani mkubwa, Michael Wambura.

Mpinzani aliyesalia wa Aveva, Andrew Tupa hana umaarufu wa kutosha katika klabu hiyo na hivyo kumuacha Aveva katika mbio zilizoonekana za “farasi mmoja”.

Nafasi ya makamu rais ilikwenda Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliyemshinda Swedi Mkwabi na Jamhuri Kihwelu ‘Julio’.Mkutano wa uchaguzi huo ulifunguliwa kwa dua maalum saa 4:49.

Wambura alikumbana na balaa jingine baada ya kuzuiwa kuingia katika mkutano huo.Wakati huo huo, wakati kocha mkuu wa klabu ya Simba, Zdravko Logarusic, akisema hajui atarejea lini nchini, Kamati ya Usajili iko katika hatua ya mwisho kumnasa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda, Hassan Waswa.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam, Simba iko katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa Waswa ili kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji.

Chanzo kilisema kuwa leo baada ya uongozi mpya kuingia madarakani utafanya maamuzi ya mwisho ya kuona ni wachezaji wangapi watabaki kuichezea Simba katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara itakayoanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu.

“Logarusic anatua keshokutwa (leo) na yeye ndiye ataamua lini mazoezi yaanze rasmi…sisi kazi yetu ya kuimarisha timu tumeifanya kikamilifu licha ya kukutana na changamoto iliyohusicha uchaguzi mkuu,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hanspoppe Zacharia.

Hata hivyo, Loga alisema jana kuwa hajui atakuja lini nchini kwani bado hajapata taarifa zozote kutoka kwa Hanspoppe, hivyo anasubiri taarifa hizo.

Logarusic ambaye mkataba wake wa awali wa miezi sita ulimalizika Mei 31 mwaka huu anatarajiwa kuendelea kuliongoza benchi la ufundi la Wekundu wa Msimbazi akisaidiwa na nahodha wa zamani wa timu hiyo, Selemani Matola.

Simba ilimaliza msimu uliopita ikiwa katika nafasi ya nne na kukosa tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa kwa mwaka wa pili mfululizo.

 BAADA YA UCHAGUZI



Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva.

ASIYEPENDA kusikiliza maoni ya watu, akaamini anajua kuliko mtu yeyote, mara nyingi huishia kufeli, kuna mifano ya watu wengi sana.

Lakini katika kusikiliza, si lazima kila unaloambiwa ulifanyie kazi, kwa kuwa kuna maoni ambayo yanaweza kuwa si sahihi, ukisikiliza kila uliloambiwa na kuliamini, pia unaweza kufeli.

Ndiyo maana Wanasimba wakamuamini Evans Elieza Aveva na kumpa urais kwa kuwa wanajua ana uwezo wa kuikwamua klabu yao kutoka kwenye matatizo, migogoro, kashfa kibao za uuzaji wachezaji bila ya kupata fedha na mengine mengi.

Pamoja na malumbano kwa zaidi ya mwezi kuhusiana na uchaguzi mkuu, hatimaye wanachama wa Simba, jana waliamua kumpa Aveva dhamana ya kuiongoza klabu yao hiyo ambayo inahitaji mabadiliko ili kurudi kwenye maendeleo na sifa yake kwa kuwa Simba ni klabu maarufu barani Afrika na yenye mafanikio katika nyanja za kimataifa kwa hapa nyumbani.

Simba imekuwa kwenye utulivu kwa miaka mingi, kabla ya uongozi wa ‘uncle’ Ismail Aden Rage, haujaingia madarakani ambao katika miaka minne ni mwaka mmoja tu ulikuwa una mafanikio, baada ya hapo ni migogoro, uadui na matatizo lukuki.

Matatizo yaliyoondoa umoja ndiyo yaliyoifanya Simba kupoteza sifa yake ya sharubu imara na badala yake karibu kila timu, zikiwemo hata Mbeya City iliyopanda daraja, zikaanza kuisumbua, kuifunga na hata ukipenda unaweza kusema waliionea Simba.

Simba haikuwa Simba tena, ndiyo maana wakati Wanasimba wanakupa kura, wengi wao watakuwa wanataka mengi lakini mawili furaha ya moyo, yaani kuwa na timu inayoshinda na maendeleo ya klabu, vitakuwa ni vitu vya kwanza kabisa.

Vipande:

Simba imevunjika vipande, kipindi cha Rage kilikuwa cha hovyo, watu hawakuwa na upendo, hawakuelewana na mwisho kila mmoja akaishi kwa kuangalia maslahi yake na si yale ya Simba tena.
Ndiyo maana uliona Simba ilivyoyumba, kwa kuwa kila mmoja aliigeuza chukua chako mapema, hivyo una kazi ya kuzuia hilo na badala yake kila mmoja afanye kwa maslahi ya klabu.

Siri:

Inawezekana watakaosoma makala haya, wataelewa lakini siri itabaki kuwa ya kwako kwamba siku zote msemakweli, anachukiwa.
Wala usisimame, songa mbele kama utakuwa unafanya mambo kwa ajili ya maslahi ya klabu. Pia ningekushauri hata kama utakuwa unajua mambo mengi ya klabu hiyo kuliko mimi, usikubali kupendwa sana.

Nimeona viongozi wengi wanaoingia madarakani wamekuwa wakipenda sana kuonekana watu wazuri wanaotaka kumfurahisha kila mtu, ni kosa kubwa.
Kama kuna mtu au kundi la watu linaharibu, basi waeleze ukweli kwa nia na njia nzuri na mwisho lengo liwe umoja na kusaidia kuijenga Simba.
Umoja:

Kama nilivyoeleza awali, Simba ya sasa iko katika vipande. Moja ya kazi kubwa ni kuunganisha makundi makubwa ambayo chuki zao ni zile za kibinadamu na zinaiumiza Simba.
Najua hauwezi ukafanya mambo yote kwa wakati mmoja, lakini umoja ni kati ya mambo ya mwanzo kabisa kuanza kuyafanya kwa kuwa bila ya kuwa pamoja hakuna kitu kimoja kinaweza kuwa cha umoja na kushika namba moja.

Binadamu wana kawaida ya kusahau, huenda wako waliokuwa na hasira kwa kuwa walitaka kugombea wakaondolewa, wengine wana hasira kwa kugombea na kushindwa. Lakini wote hao ni Simba na wana uwezo wa kuisaidia klabu yao.

Hivyo Aveva, una kazi kubwa ya kuwaunganisha Wanasimba hata kama itakuwa ni taratibu huku ukiendelea kufanya mambo mengine ya mafanikio.
Simba ni kubwa, kwa hali iliyokuwa imefikia, haiwezi kubadilika ndani ya siku mbili na kila kitu kikaenda tofauti. Lazima muda wa kutosha unatakiwa.

Lakini hakuna mabadiliko yatakayopatikana kwa siku moja bila ya kuanza taratibu. Hivyo ni vizuri kuanza taratibu kuwaunganisha Wanasimba kwa ajili ya kujenga Simba moja imara kuliko ‘visimba’ vingi visivyokuwa na ushirikiano na mwisho ni kuiua tu nguvu ya klabu hiyo.

Najua utakuwa na kazi kubwa sana, karibu usaidie kuendeleza soka na kama kawaida, ukipatia tutakumwagia sifa za kutosha, lakini siku ukikosea, basi ukweli ndiyo ada.



Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

CHEKI HAPA PICHA ZA MUONEKANO WA NDANI WA NYUMBA YA LADY JAYDEE a.k.a. JIDE.



Shamba Boy akipa usafi.
Hapa ni jikoni.

Toa maoni yako hapo chini.
habari kamili :: read more...

WEMA, KAJALA WALA UJANA KAMA ZAMANI;HAWANA BIFU WALA NN WANAZUGA TU!.


Hatimaye! Manguli wawili wa Bongo Movies waliokuwa mahasimu wakubwa na kusababisha tafrani kubwa, Wema Isaac Sepetu ‘Beautful Onyinye’ na Kajala Masanja ‘K’ hatimaye wamekutana uso kwa uso (live) na kumaliza bifu lao saa chache kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Ijumaa Wikienda limesheheni.

Manguli wawili wa Bongo Movies waliokuwa mahasimu wakubwa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Kajala Masanja ‘K’ wakikata mauno.

>NI KWENYE VUNJA JUNGU
Tukio hilo la heshima lilijiri wikiendi iliyopita nyumbani kwa staa mwenzao wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, Mwananyamala jijini Dar ambapo baadhi ya mastaa walikuwa wakivunja jungu katika sherehe ya kumpongeza rafiki yao almaarufu kwa jina la Wise Ime aliyejifungua mtoto wa kike hivi karibuni.

...Wema na Kajala katika pozi.

KWA MARA YA KWANZA TANGU WAGOMBANE
Katika tukio hilo, mastaa wenzao walipigwa na butwaa kuwaona wawili hao wakiwa pamoja kwa mara ya kwanza tangu wagombane. miezi kadhaa iliyopita.

WALA UJANA KAMA ZAMANI
Mastaa hao walinaswa pamoja wakiwa kama kumbikumbi wakila ujana kama zamani, kitendo kilichowafurahisha marafiki zao wengine waliofika nyumbani hapo wakimpongeza Aunt kwa kuwaweka pamoja kwani tangu wapatanishwe hawakuwahi kukaa pamoja wala kula sahani moja kama walivyofanya siku hiyo.

...Wema na Kajala wakila sahani moja kwa furaha.

“Ukweli sisi tumefurahishwa na ukaribu wa hawa mashosti tuliwamisi sana kuwaona hasa kwenye shughuli kama hizi za kibao kata, leo wameshirikiana kama zamani, wamezungumza, wamecheka na kukata mauno pamoja,” alisikika mmoja wa mastaa aliyehudhuria katika shughuli hiyo.

MAUNO MWANZO-MWISHO
Kwenye shughuli hiyo kulipambwa na mauno mwanzo-mwisho yaliyoongozwa na wapiga ngoma ya Kibao Kata ambapo kila mmoja aliinuka na kuonesha ustadi wake wa kukata mauno.

Aunt Ezekiel na Vanita wakikata nyonga.

HADI MAJOGOO
Shughuli hiyo iliendelea hadi majogoo kwani baada ya Kibao Kata, mastaa hao walifunguliwa disko lililokuwa likiongozwa na madj maalum wa Pro24djs huku MC akiwa ni Maimartha  Jesse.

WEMA, KAJALA, AUNT WAPAGAWISHA
Katika shughuli hiyo, Wema, Kajala na Aunt walipagawishwa na wimbo wa mpya wa mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wa Mdogomdogo ambapo waliingia kati na kuachia mauno hadharani.

Kuna wakati Kajala na Wema waliachiwa nafasi ambapo walitoana jasho kwa kukata mauno huku wakifuatisha vizuri wimbo huo utadhani walikuwa wamefanya ‘riheso’.

ASANTE DJ
Baada ya kuserebuka kwa muda mrefu hadi wakatoka jasho, wawili hao walisikika wakisema kuwa Dj alikuwa amewakuna mno kwani kila muziki aliokuwa akiwawekea alikuwa akiwalenga na kuwafanya wachangamke zaidi hadi shughuli ilipokwisha kila mtu akarudi kwake.

NENO LA WEMA
“Sasa hivi tupo vizuri sana. Yes tupo bega kwa bega ukizingatia ndiyo tunaingia kwenye mwezi mtukufu. Nimefurahi sana kushea naiti na Kajala,” alisema Wema.

NAYE KAJALA
“Kwani kuna tatizo? Hakuna tatizo. Sisi tupo vizuri kama alivyosema Wema tumeinjoi sana,” alifunguka Kajala.

Mahasimu hao wawili wakiwa kwenye picha ya pamoja na mashosti wenzao.

TUMEFIKAJE HAPA
Miezi kadhaa Wema na Kajala waliingia kwenye gogoro kubwa na kusababisha kuibuka kwa pande mbili za Team Wema na Team Kajala zilizokuwa zinachochea ugomvi huku Kajala akitakiwa kurejesha zile Sh. Milioni 13 alizolipiwa na Wema asiende jela miaka 7.

KUTOKA IJUMAA WIKIENDA
Hongereni Wema na Kajala kwa kutambua umuhimu wa kuishi kwa amani na kumaliza tofauti zenu. Sasa ni muda wa kufanya kazi kwa bidii.
Imeandikwa na Gladness Mallya, Hamida Hassan na Musa Mateja.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

JB SASA KUWA STRAIKA No 9.

 Bonge la Bwana, Jacob Steven ‘JB’.TAMBO! Bonge la Bwana, Jacob Steven ‘JB’ amejitapa kuwa licha ya mwili wake kutoonekana wa mazoezi lakini yeye ni bonge la straika.

Akistorisha na paparazi wetu, JB ambaye anatamba na filamu ya Shikamoo Mzee, alisema mpira alianza kucheza kitambo tangu alipokuwa akiichezea timu ya JKT Mgambo na Mutukula ya Mwananyamala Dar hadi sasa kwenye Klabu ya Bongo Movie wanamtegemea.

‘JB’ akiwa mazoezini.

“Kwenye mambo ya mpira mimi ni noma, ni bonge la straika, Bongo Movie wananitegemea, watu wasinichukulie poa niko fiti sana kimazoezi,” alisema JB.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Uingereza inakabiliwa na upungufu wa Mbegu za kiume kiasi cha kuagizwa Toka nje.

Onyo hili limetolewa na shirika la kijamii la matibabu ya uzazi nchini humo BFS.

Inadaiwa kuwa baadhi ya kliniki hizo hutegemea shahawa kutoka nchi za kigeni kutokana na mahitaji yake nchini humo.

Lakini mwenyekiti wa shirika hilo Daktari Allan Pacey amesema kuwa ana wasiwasi kwamba baadhi ya vituo hivyo vya matibabu sasa vinatumia kila njia ili kupata wafadhili wa mbegu hizo.

Amesema kuwa wanawake watakabiliwa na mbinu zitakazogharimu kiasi kikubwa cha fedha iwapo mbegu duni zitatumiwa.

Inadaiwa kuwa upungufu huo unasababishwa na kuondelewa kwa sheria kwamba majina ya wanaotoa mbegu hizo sasa ni sharti yajulikane ikilinganishwa hapo awali ambapo watu wengi walipendelea kuficha majina yao.

Mahitaji ya wafadhili wa shahawa yanazidi kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu ya uzazi yanawafanya wanaume wengi kutafuta watoto wao wenyewe.

Hatahivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu za kiume bado upo.

Takwimu kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa binaadamu zinaonyesha kuwa moja kati ya mbegu nne za kiume zimetoka katika mataifa ya kigeni.

Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila mbegu kumi mnamo mwaka 2005.

CHANZO:BBC/SWAHILI

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

KALAMA:NIMEMUACHA ISABELA, SIJAWAACHA WATOTO.

 Kalama akiwa kwenye picha ya pamoja na Isabela Mpanda.
 HUYU ANAOMBA USHAURI
Vipi kaka, mimi nakuomba unipe ushauri, ninatamani kweli kutoka  kimuziki lakini sijapata soko, nifanyeje? Tedy,0752813366
KALAMA: Nenda kwa Mamuu Store waliopo Kariakoo (Dar) wanashughulika na usambazaji wa kazi za muziki watakusaidia.

MALENGO
Kalama nini malengo yako ya baadaye kuhusiana na muziki na maisha yako binafsi? Salim Liundi, Dar, 0659601205
KALAMA: Kuwa mwanamuziki wa kimataifa zaidi na kuhusu kimaisha ni kuwekeza kwenye biashara tofauti.

ETI AMEZIDIWA NA CHIPUKIZI?
Kaka mbona upo kimya sana au ndiyo changamoto za wasanii wachanga wamekuja kuwafunika kabisa? Salumu Kabunda, Iringa, 0763236597
KALAMA: Kimya kingi kina mshindo, ninajipanga bado na nyimbo mpya kibao zitakuja, kuhusu wasanii wachanga kila mtu ana nafasi yake.

DINI NI KIKWAZO?
Eti Luteni nasikia unashindwa kumuoa Isabela (Mpanda), kisa ni dini? Msomaji, 0652672805
KALAMA: Hapana, tunajipanga kwanza hatutaki kukurupuka.

HISTORIA
Kaka Kalama naomba historia yako kwa ufupi, umesoma hadi wapi, umri, kabila na tofauti na muziki unafanya kazi gani nyingine? Swaum, Dodoma, 0769429458
KALAMA: Niliacha shule nikiwa kidato cha kwanza kwa sababu ya muziki, nje ya sanaa ninafanya biashara, nina umri wa miaka 33 na kabila langu ni Mzaramo.

Kalama akiwa mzigoni.

GANGWE MOBB VIPI?
Vipi kundi lenu la Gangwe Mobb lipo na vipi mbona siku hizi umekuwa kimya? Abely Majiko, Dodoma, 0758458965
KALAMA: Kundi lipo sema kila mtu anafanya kazi zake lakini ikitokea kazi ya kufanya pamoja kama kundi huwa tunafanya.

ETI NI MSALITI?
Kalama kwa nini umeamua kuisaliti ndoa yako pamoja na familia yako na kutembea na mwanadada Isabela, huogopi michepuko? Witho Mheluka, Dar, 0755085551
KALAMA: Sijaisaliti ndoa ila tuliachana na mke wangu ndiyo nikawa na Isabela.

YEYE NA ISABELA VIPI?
Nakuona muda mwingi Kalama unaongozana na Isabela hivi ni upendo au wivu unahisi ukimpa nafasi atafanya michepuko? Fungeni ndoa hata ya bomani tu. Mrs Abuu Machale, Moro, 0653358681
KALAMA: Ni upendo wa kweli, sawa tutafunga ndoa.

MAFANIKIO
Umepata mafanikio gani katika kazi yako ya muziki? Jose, Mwanza, 0757904855
KALAMA: Yapo mengi ila siwezi kuyaweka wazi yote, kikubwa sanaa imenifanya nimefahamiana na watu wengi sana.

VIPI KUHUSU BIFU?
Kaka Kalama wewe ni wa kitambo sana, unaongeleaje ishu ya mabifu ya wasanii? Pia inakuwaje wasanii wachanga wanawafunika ninyi wakongwe yaani hatuwasikii kabisa? Rich Boy, Tabora, 0759093909

KALAMA: Nawasihi wasanii wenzangu tuachane na bifu na badala yake tufanye kazi kwa ushirikiano na tupendane. Wasanii wachanga siyo kwamba wanatufunika ila huu ni wakati wao, huwezi siku zote kuwepo wewe tu.

Luteni Kalama katika pozi.

SKENDO
Kaka Kalama unajiepushaje na skendo pia ulimpataje Miss Ruvuma, Isabela Mpanda? Rejina Musa, Arusha, 0767909535
KALAMA: Ni kujiheshimu tu, kuhusu nilivyokutana na Isabela ni historia ndefu ila tulikutana Lindi ambako tulikwenda na kundi letu la Gangwe kufanya shoo mwaka 2002, tukaanza urafiki hadi kwenye uhusiano.

KAMUACHA MKEWE?
Kalama ina maana umemuacha kabisa mkeo na watoto? Maana mimi nakujua vizuri. Vai, Tanga, 0715282806
KALAMA: Nimemuacha mke, sijawaacha watoto.

\HUYU ANAMFAHAMU SANA
Kalama nakujua vizuri, tumemaliza darasa moja Shule ya Msingi ya Tandale-Magharibi (Dar) na ulikuwa unakaa Uwanja wa Fisi (Manzese), babu yako alikuwa na mashine ya kusaga nafaka. 0758828014
KARAMA: Ni kweli.

YEYE NA MALIPO NI NDUGU?
Kwanza napenda kazi yako, naomba kuuliza eti wewe na Malipo ni ndugu? Fatuma Juma, Dar, 0657892533
KALAMA: Ni mdogo wangu nikitoka mimi anafuata yeye.

VIPI HUDUMA KWA WATOTO?
Wewe Kalama watoto wako unawahudumia vipi na wako wapi? Mama Elvis, Dar, 0656334307
KALAMA: Wako shule Bukoba huwa nawatumia fedha, wakati wa likizo huwa naenda kuwaona au wanakuja Dar.

BIFU NA INSPEKTA VIPI?
Nafarijika sana kukuona ukiwa bado unakaza buti kwenye gemu, nini chanzo cha mtafaruku kati yako na Inspekta Haroun? Assanary, Mwanza, 0757212099
KALAMA: Hatuna mtafaruku wowote na hatujawahi kugombana.

YEYE NA LINAH VIPI?
Uliwahi kutoka kimalovee na Linah (Estalina Sanga) kabla ya kukutana na Isabela? Joseph, Dar, 0713221774
KALAMA: Hapana sijawahi.

HUYU ANATAKA KUJUA?
Kaka Luteni wewe ni mwenyeji wa wapi? Asha Sadiki, Tanga, 0655954760
KALAMA: Mimi ni mwenyeji wa Dar.

OA SASA
Luteni Kalama mimi nakukubali ila unatakiwa uoe, acha uwaluwalu. Neema, Arusha, 0754086622
KALAMA: Sawa nitaoa.

HUYU ANAHOJI
Kwa nini wasanii wengi hawaoi, Luteni Karama nakupongeza kuwa na watoto wawili, mastaa wengi hawana watoto wanapenda kuishi bachela. Nofedy Mtete, Iringa, 0787104390
KARAMA: Sijui kwa nini, asante kwa pongezi.
CREDIT:GPL

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Binti abakwa na Baba yake na kuambukizwa UKIMWI.

Binti anayedaiwa kubakwa na baba yake, kupewa ujauzito na kuambukizwa Ukimwi. Picha na Florence Focus.
“Amini usiamini hizi ni zama za mwisho mwanangu, mimi hili suala bado haliniingii akilini kabisa, kwani nilizoea kusikia kama hadithi kuwa mzazi ana uhusiano wa mapenzi na mwanawe, lakini leo hii yamenikuta ya kunikuta,” haya ni maneno ya Bhoke Mwita (siyo jina halisi), mama mzazi wa binti anayedaiwa kubakwa na baba yake mzazi kwa miaka minne.
Bhoke anasema kibaya zaidi mwanaye  amefanyiwa unyama huo na baba yake mzazi, huku akimwachia doa ambalo haliwezi kufutika milele ambao ni ugonjwa wa Ukimwi.
Tukio hilo linamsababisha Wanjara kunyamaza kwanza kabla ya mahojiano, baadaye anadai binti yake kapewa ujauzito na maambukizi ya Ukimwi na baba yake, ingawa alikuwa hajitambua kuwa ni mgonjwa hatua ambayo imemuumiza na kumtia aibu kwenye jamii.

Mkazi huyo wa Mtaa wa Kigera Kibini, Kata ya Kigera, Manispaa ya Musoma mkoani Mara, anasimlia historia ya maisha yake hadi kuzaa mtoto huyo wa mwisho nje ya ndoa baada ya mumewe kufariki, lakini hatima imekuwa kugeuzwa mke mwenza.
Mwita anasita kuendelea na simlizi kabla binti yake aliyefanyiwa unyama na baba yake, hajasimulia masaibu yake: “Matatizo niliyonayo ni mengi, Mungu pekee ndiye anayefahamu, bado naongezewa msalaba mzito kama huu.”
Ghafla anapaza sauti anaita jina la binti yake aliyefanyiwa ukatili, aliyekuwa chumba kingine na kumtaka aeleze yote yaliyomsibu ili ulimwengu utambue.
Simulizi za binti
Anatokea binti mrembo ila sura yake inaonyesha unyonge, mrefu, mwembamba  anasalimia kwa sauti ya upole huku akielekea kwenye kiti kuketi, afya yake siyo ya kuridhisha.
Bila kupoteza muda, binti huyo anadai alianza kuishi na baba yake mwaka 2002  akiwa anaingia darasa la tatu, baada ya mama yake kupata kibarua kwenye  nyumba ya watawa.
Anasema baba yake alikuwa akiishi na kaka zake wawili wakubwa ambao walikuwa wamemaliza shule na wakati huo walikuwa wakijihusisha na kazi za vibarua.
Anasimulia kuwa alipofika darasa la tano, baba yake alikuwa akimfuata chumbani kabla ya kaka zake hawajarudi nyumbani na kumtaka afanye naye ngono.  Binti huyo anasema kwamba wakati huo alikuwa hafahamu chochote kuhusu mapenzi.
 “Nilipoona baba ananipiga kila siku, nilikubali, akawa anakuja chumbani kwangu na wakati mwingine ananiita kwake, tukishamaliza ananiambia niende kwangu kulala, hivyo nikaona kama jambo la kawaida,” anasimulia binti huyo.
Anaendelea kusema kuwa baada ya kumaliza shule ya msingi mwaka 2009, alibaki na jukumu la kumhudumia baba yake kama mume wake, jambo ambalo anadai  lilikuwa likimuumiza, hivyo akaamua kuwa wazi ili apate msaada.


    “Mwaka 2010 nilikuwa tu nyumbani, kazi yangu ilikuwa kumhudumia baba, kupika na kuchota maji, marafiki zangu hawakuruhusiwa kufika nyumbani, pia sikutakiwa kutoka, nikizungumza na jirani baba anakuwa mkali kama mbogo, nikaamua kumshirikisha dada yangu (anamtaja) ili anisaidie, japo alikuwa akiniuliza kuhusu jambo hilo namkatalia,” anadai.

Baada ya kumweleza dada yake, alimpa mbinu za kutoroka ili amsaidie kumfikisha kwa mama yao aliyekuwa amehamia Kijiji cha Kabasa, Wilaya ya Bunda.

Mama mzazi anena
Bhoke anasema baada ya mumewe wa ndoa kufariki mwaka 1989, alianza uhusiano na mwanamume huyo (anamtaja) alipata mimba na kujifungua binti huyo Septemba 3, 1994.
“Nilipojifungua mwanamume huyo alinitunza vizuri, alimpenda mwanawe hivyo sikuhangaika kumlea ingawa alikuwa mume wa mtu, kwa sababu alikuwa na familia yake,” anasimlia Bhoke.
Anasema kuwa mwaka 2003 alipata kibarua cha upishi nyumba ya watawa wa Shirika la Utawa mjini hapa, huku akitakiwa kuishi kwenye nyumba hiyo hivyo ilimlazimu kumtafutia mtoto wake sehemu ya kuishi kutokana na nyumbani kwake kutokuwapo mtu.
Mama huyo anadai baada ya mwanamume kupata taarifa kuwa mtoto amepelekwa kuishi kwa babu yake, alimfuata na kumwomba ampe mwanaee akamlee.
“Sikuwa na sababu za kumnyima mtoto, kwani ni wake, hivyo nilimkabidhi. Hata hivyo, nyumbani kwake hapakuwa mbali na nilipokuwa naishi,” anasema Bhoke na kuongeza:
“Kipindi anamchukua alikuwa anaingia darasa la tatu, hivyo alikuwa na akili ya kutambua zuri na baya, niliamini kama ataona anateseka atarudi hapa kwa dada zake.”
Anasema yeye aliendelea kufanya kazi nyumba ya watawa kwa miaka miwili, kisha akarejea nyumbani na  kuamua  kwenda kijijini kulima.
Bhoke anadai kabla hajaenda kijijini alikuwa akisikia maneno kwa majirani kuwa, mzazi mwenzike ana uhusiano wa kimapenzi na binti yake, lakini hakuamini, huku akimtaka binti yake mmoja kufuatilia ukweli wa tetesi hizo.
Anadai mwaka 2007, binti yake alianza kutaja maovu ya baba yake kwa dada yake, lakini akimtaka asimweleze mama yake, ingawa alimwambia licha ya kusema kuwa baba yake akimtaka kimapenzi, hakutamka iwapo wanajamiiana.
“Baada ya kupata taarifa hizo nilianza kuhisi kitu ila sikuwa na la kufanya, kwa sababu mtoto mwenyewe hana ushirikiano wa kutosha,” anadai Bhoke.
Mwaka 2007, binti alimaliza elimu yake ya msingi Shule ya Kamnyonge lakini alishindwa kuendelea na sekondari.
Anadai baada kushindwa, baba yake alimpeleka Shule ya Msingi Nyasho kurudia  darasa la sita, hivyo alimaliza tena darasa la saba mwaka 2009 lakini hakufaulu.

Taarifa zilivyojulikana
Dada yake binti huyo anadai baada ya mdogo wake kukiri baba yake anajamiiana naye kwa lazima, alimhurumia na kumsihi atoroke na kwamba atampa nauli aende kwa mama yake kijijini. Anasema alipofika kwa mama yake alitafutiwa shule akarudia darasa la saba Shule ya Msingi Kung’ombe, Wilaya ya Bunda mwaka 2011, alifaulu na kujiunga na Sekondari ya Wariku mwaka 2012.
Anadai baada ya kufunga shule Juni akiwa kidato cha pili, alimlazimisha mama yake ampe nauli ili aende Musoma kumsalimia baba yake. Anadai alipofika kwa baba yake hakurejea tena Bunda, zaidi ya baba yake kumpigia simu mama yake kuwa mtoto wake anateseka hivyo anamchukulia uhamisho asomee Musoma Mjini.
Anadai mdogo wake alihamia Sekondari ya Nyasho mjini hapa, ambako alisoma miezi miwili na kuachishwa na baba yake na kumpeleka Kijiji cha Sirorisimba, wilayani Serengeti kufanya kazi za hotelini.
Hata hivyo, anadai siri ilifichuka baadaye kwamba mdogo wake alitoroshwa  kutokana na ujauzito, hivyo baada ya mimba kukua alishindwa kuendelea na kazi ili apate nauli ya kurejea kwa mama yake Bunda.
Baada ya kufika kwa mama yake, alimpeleka kupima ingawa binti huyo alikataa kuwa siyo mjamzito lakini vipimo vilionyesha ana ujauzito.
Mama yake alimpa nauli ya kurudi kwa baba yake kwa sababu alimchukua kwa madai ya kumsomesha, hivyo hakuona umuhimu wa kumpokea akiwa na hali hiyo.

Dada yake anaendelea kusema, siku moja alikwenda kumsalimia mdogo wake na kumkuta akiwa na hali mbaya, hatua iliyomshtua na kumpigia simu mama yao  na ndugu zake wengine ili kumpa msaada wa kumpeleka hospitali.
“Nilimkuta mdogo wangu akiwa na hali ambayo siyo nzuri kwa kweli, alikuwa kavimba mwili mzima, halafu amejisaidia haja kubwa na ndogo hapohapo kitandani hakuna msaada, niliumia sana!”
Baada ya kumpeleka hospitali vipimo vilionyesha ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi, walimpa ushauri nasaha na kumwanzishia dawa za kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto.
Anasema binti alikaa nyumbani wiki moja tu na kujifungua mtoto akiwa amekufa, kufuatia hali hiyo taarifa zililifikia Dawati la Jinsia la Polisi na kumtia mbaroni mtuhumiwa.

Msaada wa kisheria
Awali, binti huyo alikuwa akipewa msaada na Shirika lisilo la Serikali  la Watoto Wapinge Ukimwi (WWU) mjini hapa kama mtoto anayeishi katika mazingira magumu, walimsaidia akiwa darasa la kwanza hadi la saba, baada kuhitimu elimu ya msingi hawakuendelea naye.
Mkurugenzi wa shirika hilo, Sista Marion Haqhes anasema hawezi kumzungumzia mtoto huyo kwa sababu shirika lake na sheria ya mtoto haimruhusu ingawa tukio hilo ni kweli.

Polisi wanena
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Paul Kasabago anathibitisha kuwapo taarifa za ubakaji na kwamba, mtuhumiwa amekuwa akimbaka binti yake muda mrefu.
Kasabango anasema licha ya mtuhumiwa kumbaka binti yake mara kwa mara, amemsababishia ujauzito aliojifungua mtoto aliyekufa na vipimo vimeonyesha amemwambukiza Ukimwi.
Anasema kwa sasa mtuhumiwa yupo rumande kwa mahojiano zaidi na kwamba, atafikishwa mahakamani muda wowote.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Kajala masanja katika pozi za kimitego.

 Wanasema chembe na kidevu lazima ukae anakata zaidi ya wembe usomjua usimshangae huyo ni kajala masanja ambaye yuko mguu ndani mguu nje kuihama bongo kwani anakerwa na lawama zinazomwandama kiasi cha kutojisikia furaha maishani mwake.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Alichokisema Diamond baada ya kukosa tena tuzo za BET 2014.

 Dakika kadhaa baada ya mshindi wa tuzo ya BET 2014 kwa wasanii wa Afrika kutangazwa kuwa Davido wa Nigeria, staa kutoka Tanzania Diamond Platnumz aliekua anawania pia tuzo hiyo ameandika ya moyoni kwa watu wake.

‘Tusipopenda kukubali matokeo na ushindi wa wenzetu basi daima hatutaweza kuwa washindani, muhimu ni kujua wapi tulipotoka na wapi tulipo leo, katika nchi zaidi ya 20 zenye wasanii zaidi ya milioni 40 kuchaguliwa Tanzania ni fursa, heshima na hatua kubwa, cha muhimu ni kuitumia vyema fursa hii na kuhakikisha mwakani tunapiga hatua, asante sana kwa wote wanaozidi kunisupport’
KIPO HAPO CHII ALICHOKIANIKA.


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Sunday, June 29, 2014

Jionee Picha kali ya Masogange inayowadatisha wanaume wa south.



Bonyeza like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

habari kamili :: read more...

Friday, June 27, 2014

MZEE WA KANISA AAIBIKA BAADA YA JARIBIO LAKE LA KUVUNJA AMRI YA SITA KUUMBULIWA!


Mzee wa kanisa la kiroho aliyetajwa kwa jina la Luca Pesa,akitembezwa mtaani.
HABARI KAMILI
Tukio hilo ambalo kamwe Luca hawezi kulisahahu maishani mwake, lilijiri kwenye gesti hiyo iliyopo karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Segerea, Dar, Jumanne iliyopita huku mzee huyo akishushiwa tuhuma nzito ya rushwa ya ngono kwa vibinti chini ya miaka 18.

Katika tukio hilo, mzee huyo wa kanisa na msanii huyo wa Kundi la Maigizo la Vivif lenye maskani yake maeneo hayo walikuwa wamejichimbia kwenye gesti hiyo katika chumba ambacho mlangoni kilikuwa kimeandikwa Rombo kabla ya kuchomolewa na kufikishwa kanisani kisha polisi.

TUHUMA NZITO
Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, ikiwa kwenye mingo zake, ilipokea simu kutoka kwa dada aliyejitambulisha kwa jina moja la Diana na kujieleza kuwa anatoka kundi la sanaa za maigizo la Vivif lililopo Segerea jijini Dar.

OFM: Ndiyo hujakosea unazungumza na
OFM, tukusaidie nini?
Diana: Kuna mzee wa kanisa la kiroho la (anataja jina la kanisa hilo) lililopo maeneo ya Segerea, aliomba kuwa mfadhili wa kundi letu.

Akiwa kwenye geti la kanisa.

Tulimkubalia na baada ya muda alianza kutumia fedha zake vibaya kwa kufanya vitendo visivyofaa.
OFM: Vitendo gani visivyofaa?
Diana: Anawarubuni mabinti wadogo anawaweka kambini na kula nao tunda tamtam eti ndiyo tiketi ya kuchezeshwa kwenye maigizo.
OFM: Tiririka!

Diana: Yaani hadi muda huu ninapozungumza na ninyi mzee huyo wa kanisa anachati na msanii mwingine wa kundi hilo. Anaitwa Debora anataka waende kwenye gesti fulani wakanogeshane, wahini tayari mtego umewekwa utafyatuka muda wowote.

UDHALILISHWAJI?
Diana alisema baada ya Debora kuombwa ‘mambo’ ndipo akawataarifu wasanii wenzake na kuwataka wote kwa pamoja waungane kuikomesha tabia hiyo chafu ya Luca anayelichafua kanisa la kiroho na kulidhalilisha kundi lao la sanaa.

OFM MZIGONI
Baada ya kuseti kila kitu, Diana aliiomba OFM iambatane nao kwani muda huo tayari Debora alishatangulia kwenye gesti hiyo kumfuata mzee huyo wa kanisa ambaye alishachukua chumba.

.....akitaitiwa.

Taarifa hiyo ilipokelewa kwa mikono miwili na kiongozi wa OFM ambaye aliwaagiza vijana wake makini ambao walisitisha kazi nyingine za kiintelijensia kisha kuelekeza nguvu zao eneo la tukio.
Vijana hao walitumia pikipiki zao ziendazo kasi ambapo baada ya muda usiozidi dakika ishirini walikuwa wamefika kwenye gesti hiyo.

ENEO LA TUKIO
OFM walipofika eneo la tukio, walikuta kundi la wasanii hao wakimchomoa gesti mzee huyo wa kanisa ambaye aliruka ukuta na kudondokea kwenye matuta ya viazi.

Akiwa anajizoazoa kwenye matuta hayo, kundi la wasanii hao lilimuunganishia ambapo kabla ya kumnasa aliingia kwenye chumba cha nyumba iliyopo jirani na gesti hiyo ili kujisalimisha.
Hata hivyo, zoezi lake lilifeli baada ya wasanii hao kumtahadhalisha mwenye nyumba hiyo kuwa wanamtaka mtuhumiwa wao la sivyo wangeichoma moto.

Baada ya kuzingirwa na wasanii hao huku akihatarisha maisha yake kwa kuwa wasanii hao walikuwa na hasira, aliona yasiwe makuu akaamua kuwaruhusu wamtoe mtuhumiwa wao wakamalizane naye kanisani.

KABANG!
Alipotiwa mikononi, mzee huyo wa kanisa aliomba apelekwe kanisani ambapo hapakuwa mbali na eneo la tukio ili akahifadhi vitu vyake muhimu pamoja na kuomba ushauri.

APELEKWA MSOBEMSOBE KANISANI
Kundi hilo la wasanii lilimpeleka kanisani msobemsobe ambapo baada ya hatua kadhaa polisi walitokea na kuwadhibiti wananchi wenye hasira na wasanii waliotaka kumdhuru mzee huyo wa kanisa wakati akipelekwa kanisani.
MTAANI WERAAA!
Wakiwa mitaani, njiani mabinti walikuwa wakipiga kelele ‘weraaa…ukomeee…’ huku wakifurahia kufunga mitaa kwa madai kwamba mzee huyo wa kanisa alizidi.
Katika sekeseke hilo, polisi hao walimtia pingu mzee huyo wa kanisa na kuongoza safari ya kuelekea kanisani.

Wakiwa kanisani hapo polisi walijitambulisha na kuwauliza wachungaji pamoja na waumini wa kanisa hilo kama walimfahamu mzee huyo wa kanisa.

BREKI YA KWANZA POLISI
Kundi la wazee pamoja na vijana wa kanisa hilo walikiri kuwa Luca ni mmoja wa wazee wa kanisa hilo ndipo polisi hao wakamruhusu kuwakabidhi baadhi ya vitu vyake ikiwemo simu na fedha kisha breki ya kwanza ikawa Kituo cha Polisi cha Tabata-Shule ambapo alifunguliwa jalada la kesi namba RB/3843/2014 -RUSHWA YA NGONO, KUWAWEKA KAMBI KINYUME CHA SHERIA WASICHANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 NA KUWADHALILISHA KIJINSIA.

Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

Hadi OFM wanaanua jamvi kituoni hapo kanisa lilikuwa likihaha kumchomoa kwa dhamana akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
habari kamili :: read more...

MKE WA TYSON ATAKA MALI ZAKE!


Mke wa marehemu George Otieno ‘Tyson’, Beatrice Shayo.

Wakati hata siku arobaini hazijatimia, mke wa marehemu George Otieno ‘Tyson’, Beatrice Shayo juzi alicharukia mali zake baada ya kuamua kutinga nyumbani kwa marehemu, Mbezi Makonde jijini Dar kwa lengo la kuchukua kila kinachomhusu.

Mdada huyo aliyefunga ndoa na Tyson Agosti 9, 2012 nchini Kenya na kujaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Eugene, alishuhudiwa na gazeti hili Juni 24, mwaka huu saa sita usiku akiwa na ndugu zake na kuanza kugonga geti la nyumba hiyo.

Katika kujua kilichokuwa kikiendelea, mmoja wa mapaparazi wetu aliwasogelea na kuzungumza na Beatrice ambaye alieleza kuwa, lengo lake lilikuwa ni kuchukua mali zake zilizomo mle ndani.
“Ulidhani mimi nataka kuingia kwenye nyumba hii nikae, la hasha! Nimefuata mali zangu tu basi,” alisema Beatrice huku akiendelea kugonga geti hilo.

Mke wa Tyson (kulia) na ndugu zake wakisubili getini.

Wakati Beatrice na nduguze wakionekana kukata tamaa ya kufunguliwa, mara alitokea mwanamke anayedaiwa alikuwa akiishi na marehemu mpaka kifo kilipomkuta na kuuliza aliyegonga geti ni nani, alipotajiwa jina la Beatrice alisema: “Eee, Beatrice, usiku huu umekuja kutafuta nini?”
Beatrice: Nina shida, naomba ufungue tuongee.

Mwanamke: Hatuwezi kuongea usiku huu, uje kesho asubuhi.
Beatrice: Nakuomba ufungue tu, nimekuja kuchukua mali zangu nilizoacha humo ndani na nimekuja na gari kabisa la kubebea.

Mwanamke: Mali gani, humu hamna chako na kama una kitu chako humu, fuata taratibu.
Beatrice: Nimefuata taratibu, nipo na mjumbe hapa.

George Otieno ‘Tyson’,enzi za uhai wake.

Mwanamke: Ndiyo nasema mje kesho asubuhi na mapema mtanikuta.
Baada ya mwanamke huyo kugoma kufungua, mjumbe wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la Sabina Mawanda aliwashauri waondoke na kurudi tena asubuhi lakini inadaiwa walipofanya hivyo walikuta nyumba imefungwa na hakukuwa na mtu.

Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

habari kamili :: read more...

Thursday, June 26, 2014

Breaking: Luis Suarez kutoshiriki shuguli za mpira kwa miezi minne na kutocheza mechi za kimataifa 9.

Mshambuliaji wa Uruguay na clabu ya Liverpool Luis Suarez amepewa adhabu NA shirikisho la soka Duniani yaani FIFA ya kutoshiriki shuguli zozote za mpira kwa mda wa miezi minne na  kuto cheza match 9 za kimataifa kufuatia kumng'ata meno beki wa Italy Giorgio Chiellini.

Uruguay and Liverpool striker Luis Suarez has been banned for four months after being found guilty of biting Italy defender Giorgio Chiellini during Tuesday's World Cup game between the sides.

Toa maoni yako hapo chni kama hii adhabu itamfaa


Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

habari kamili :: read more...

Picha za Mashabiki wa Yanga wakimlaki Marcio Maximo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.


Kocha mpya wa Yanga SC, Marcio Maximo baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar.

Polisi akidumisha ulinzi wakati wa mapokezi ya Maximo.

Maximo akiwanyooshea mkono mashabiki wa Yanga.

Mashabiki waliofika kumpokea Maximo.

Mashabiki wa Yanga wakipozi na kocha wao mpya.

Kocha Marcio Maximo ametua jijini Dar muda mfupi uliopita kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa kuanza kuifundisha timu ya Yanga. Maximo amepokelewa kwa shangwe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na mashabiki wa Yanga.

Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

habari kamili :: read more...

Jionee sura ya Corazon kabla ya Make-up na baada ya kufanyiwa.

Kwa staili kweli ............................ Toa maoni yako hapo chini.

Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza Like hapo juu

habari kamili :: read more...
 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top