Wednesday, April 30, 2014

ALIYEPIGWA NA CHID BENZ YU MAHUTUTI HOSPITALINI.


MREMBO Mwanaisha Kiboye, mkazi wa Ilala, Dar anayedaiwa kupigwa na mwanamuziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, hali imekuwa mbaya kwani yu mahututi.

Mwanaisha Kiboye, akiwa hoi hospitali baada ya kipigo kutoka kwa msanii Chid Benz.

Juzi Jumatatu, wakati staa huyo akipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar kwa kesi hiyo, Mwanaisha alikuwa akipumua kwa tabu kwenye chumba maalum katika Hospitali iitwayo Aviation iliyopo maeneo hayo ya Ilala.

MAMA MDOGO ANASEMAJE?
Kwa mujibu wa mama mdogo wa Mwanaisha aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha, hali ya mgonjwa imekuwa tete kwani kwa siku moja amekuwa akizimia zaidi ya mara tano.

Mtuhumiwa Chid Benz.

AZIMIA MARA TANO
“Mwanangu hali yake ni mbaya anazimia zaidi ya mara tano kwa siku halafu watu wananiambia nitoe kesi mahakamani si nitaonekana chizi jamani?” alisema mama huyo huku akilengwalengwa na machozi.
Alisema hali ya mgonjwa imekuwa ikibadilika hasa suala la presha kupanda na kushuka huku mapigo ya moyo yakiwa chini hivyo kuwatia hofu ndugu, jamaa na marafiki.

KIPIMO CHA KICHWA
Aliongeza kuwa siku hiyo (Jumatatu) madaktari na wauguzi walikuwa katika harakati za kumpeleka kwenye kipimo kiitwacho CT Scanning kuangalia madhara yaliyompata kichwani na kusababisha hali kuzidi kuwa mbaya.

Mwanaisha Kiboye akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Aviation, IIala.

Mwanahabari wetu alifanikiwa kuingia wodini ambapo katika kipindi cha saa kadhaa Mwanaisha hakugeuka wala kuamka kutoka usingizini.

TURUDI KWENYE KESI
Juzi (Jumatatu) Chid alitakiwa kupandishwa kizimbani Mahakama ya Mwanzo, Wilaya ya Ilala, Dar kwa ajili ya kesi hiyo lakini hakutokea kortini badala yake alimtuma mdhamini wake amuombee udhuru kuwa alikuwa akiumwa.

CHEMBA KIDOGO
Karani wa mahakama hiyo, Nusura Seleman alipoita kesi hiyo, mdhamini huyo na ndugu wa Chid Benz na ndugu wa Mwanaisha, walijongea kwenye ‘chemba kidogo’ mbele ya Hakimu Leonia Muta.

HAIWEZEKANI
Katika kesi hiyo ambayo mwanahabari wetu aliifuatilia hatua kwa hatua, hakimu Muta aliwaita wenye kesi hiyo lakini wote hawakuwepo ndipo hakimu huyo akasema hawezi kuendelea na kesi hiyo bila wenye kesi wote kuwepo. Shauri hilo liliahirishwa hadi Mei 5, mwaka huu.

MAMA CHID ATOLEWA NDUKI
Akizungumza nje ya mahakama hiyo, kaka wa Mwanaisha aliyejitambulisha kwa jina la Swedy alisema:
“Hali ya ndugu yetu ni mbaya namna ile halafu wanatuambia tukayamalize nyumbani, hilo si jambo la kushangaza jamani?

Mama yake Chid Benz alikuja nyumbani kutaka kumuona mgonjwa tukamtoa nduki.
“Hali ya ndugu yetu ni mbaya hivyo asijekudhurika na jambo lolote akiwa nyumbani kwetu ikaonekana tumemfanyia kusudi.

CHID NAYE ATOLEWA BARU
“Hata Chid Benz mwenyewe naye juzi (Jumamosi iliyopita) alikuja na kutupigia magoti naye tukamtoa baru, asitulee zake kwanza hii siyo mara ya kwanza kumpiga dada yangu kuna kipindi alimpiga kesi ilikuwa Kituo cha Polisi cha Kilwa Road.”

BADO HALI TETE
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni Jumatatu jioni, bado hali ya Mwanaisha bado ilikuwa ni tete.
Chid Benz alidaiwa kumpiga Mwanaisha Siku ya Pasaka Aprili 20 mwaka huu maeneo ya Ilala, Dar.
habari kamili :: read more...

Tuesday, April 29, 2014

Sketi fupi na ya kubana yamtia mashakani Officer wa polisi Kenya.

Afisaa mmoja wa polisi mwanamke nchini Kenya amepewa onyo kali kwa kuvalia sketi iliyokuwa imembana kiasi cha kuonyesha umbo lake.

Wakuu wake walichukua hatua ya kumuonya polisi huyo baada ya picha yake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kupigiwa gumzo kubwa.

Alipigwa picha akiwa amevalia sketi yake fupi na yenye kumbana akiwa anashika doria katika eneo ambako mashindano ya magari yalikuwa yanafanyika eneo la Kati mwa Kenya.

Afisaa huyo kwa jina Linda Okello, alitakiwa kufika mbele ya mkuu wake James Mugeria na kuonywa vikali dhidi ya kuvalia hivyo kwa mara nyingine, kitendo ambacho alifahamishwa kuwa ni utovu wa nidhamu kwa kuvalia nguo isiyo ya heshima kwa polisi

Maafisa mjini Kiambu walisema kuwa kupewa onyo kwa afisa Linda na kuonywa dhidi ya kuvalia sketi yake iliyokuwa imembana sana ni jambo la kawaida na kwamba ameruhusiwa kuendelea na majukumu yake.

Waliongeza kuwa afisa huyo ameamrishwa kuanza kuvalia kiheshima.

Alipigwa picha na mwanahabari mmoja wa gazeti moja maarufu nchini Kenya akiwa na wenzake kazini mjini Kiambu. Lakini punde si punde picha hiyo ikaanza kusambazwa kwa mitandano ya kijamii na baadhi wakiikejeli.

Taarifa ya polisi huyo kuonywa ilizua hasira kwenye mitandao ya kijamii baadhi wakihoji ikiwa ni makosa kwa afisaa wa polisi kuvalia sketi ya kumbana. Nini Kauli yako?
habari kamili :: read more...

MATESO : ANGALIA SHUGULI YA KUCHORA TATTOO


ujue kuna vitu vingine huwa tunavifanya tu ili kuiga sasa kama kuwekewa tattoo inauma kiasi hicho kwa nini alienda si angeacha tu
habari kamili :: read more...

LOL!! NIKILALA NA MWANAUME ASIYE NA PESA SIRIDHIKI NA WALA SIFIKI KILELENI.

Wapendwa naomba msaada maana naona napotea , yaani boy wangu alisafiri kikazi karibia mwaka mzima sasa huku mimi sababu ya upweke nikaanza kuchepuka na Boss wangu , kila week end ananipeleka nje ya Mji kama Bagamoyo ama Kigamboni tunalala huko na kufanya starehe za kila aina , Baada nikawa natoka na Wengine pia wenye pesa , sasa cha ajabu nikitoka na mtu ambae hana pesa za kunipeleka mbali ya mjini na kunipa starehe mbali mbali si enjoy hata tukifanya sifiki kileleni , Sasa kibaya boywangu amerudi nashangaa simfeel hata kidogo kama zamani kwani yeye si mtu wa sterehe....yaani sometimes ili nienjoy inabidi nichepuke kwa wale mapedeshee wenye kujua starehe ni nini ....Nifanyaje?
habari kamili :: read more...

HUYU NDIYE BINTI ANAYEDAI KUTEKWA NA KUFANYIWA KITU MBAYA NA NEY WA MITEGO..!! PICHA ZOTE HAPA

Katika sakata linaloendelea sasa ni Ney wa mitego kumteka dada huyu, kama hukusoma hapoa awali ilikuwaje basi fungua post za numa utaiona post ya mdai hayo.
habari kamili :: read more...

Mdada apewa kichapo na maza ake baada ya kupost picha chafu fb, Mcheki hapa.

Binti alipost picha yake ambayo imeelezwa kuwa ni ya nusu uchi kwenye page yake ya facebook na kama kawaida ya internet ikasambaa ghafla.
Mama wa binti huyo baada ya kusikia hizo habari hakuweza kujizuia na kumpa kichapo kikali kwa kuchapa na mkanda binti yake huyo mwenye umri wa miaka 12.
Baada ya video hii kusambaa mama huyo raia wa Trinidad and Tobago amesema hajilaumu kumchapa mwanae na wala haogopi kwenda jela kwasababu alikuwa anamuonyesha mwanae njia nzuri ya kuishi.
habari kamili :: read more...

Dent wa Chuo afia ndani ya Gheto la Mshikaji wake huko Kibaha.


MSICHANA Atu Gabriel mwenye umri wa miaka 20,  mwanafunzi wa Chuo cha Eden Hill kilichopo Kwamfipa wilayani Kibaha mkoani Pwani, amekutwa amekufa chumbani kwa mtu anayetajwa kuwa ni hawara yake, Hafidh Mohammed
Tukio hilo lilitokea April 26, mwaka huu na kukusanya umati huku mwanaume aliyelala na binti huyo akitokomea kusikojulikana.Marehemu anadaiwa kuwa mwenyeji wa Makambako mkoani Njombe.

Akizungumza na waandishi wetu juzi Kibaha, mama wa Hafidh ambaye pia ni mjumbe wa eneo hilo, Zainabu Saidi alisema mwanaye alimweleza kutokea kwa tukio hilo asubuhi kulipokucha na kabla ya hapo, hakuwa akifahamu kama alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana huyo kwa vile aliyekuwa akimfahamu ni mwanamke mwingine ambaye alizaa naye.

“Mimi kwa kweli sikuwa na taarifa yoyote juu ya uhusiano wao na huyu  mwanafunzi, nimeletewa taarifa asubuhi na kijana wangu huku akionekana kuchanganyikiwa, nimejaribu kumsihi asikimbie lakini imeshindikana,” alisema mama huyo.

Mwili wa Atu ukiingizwa kwenye gari la polisi.

ALIVYOAGA CHUONI
Wanafunzi wa chuo hicho kinachofundisha masomo ya biashara na habari ambao walikataa kutaja majina yao waliliambia gazeti hili kuwa, marehemu Atu aliwaaga anakwenda jijini Dar es Salaam kumuuguza wifi yake aliyelazwa katika Hospitali ya Amana, Aprili 23, mwaka huu.

Hata hivyo, walisema uondokaji wake uliwapa maswali mengi kwani tofauti na walivyotegemea kuwa angebeba mfuko mkubwa wenye nguo za kubadili, yeye aliondoka akiwa na mkoba wake wa mkononi pekee hali iliyoonesha hakuwa akienda mbali.

Walisema siku tatu baadaye walipatwa na mshtuko mkubwa baada ya mlinzi wa hosteli yao kuwaletea taarifa za kifo cha mwenzao kilichotokea katika chumba cha mvulana huyo anayeishi jirani.

MAJIRANI NAO WANENA
Majirani waliozungumza na gazeti hili walisema kwao haikuwa mara ya kwanza kumuona msichana huyo, kwani mara kwa mara alikuwa akifika pale ingawa akishaingia ndani hakuwa akitoka nje.

Walisema mara zote hizo, mwanaume huyo mwenyeji ndiye alikuwa akitoka nje na kwenda kumnunulia chakula.

Wananchi na wanausalama wakiwa eneo la tukio.

POLISI WAUPELEKA MWILI HOSPITALI YA TUMBI
Jeshi la polisi liliwasili eneo la tukio na kuukuta mwili huo ukiwa umelala kitandani ukiwa hauna jeraha, lakini pembeni yake kulikutwa vidonge ambavyo havikufahamika ni vya aina gani ambavyo pia vilichukuliwa pamoja na mkoba wake hadi kituonis.

Minong’ono kutoka kwa majirani kuhusiana na vidonge hivyo ilitofautiana,  baadhi yao walisema huenda vilitumika katika jaribio la kutoa mimba, wengine walisema inawezekana msichana huyo alipata ugonjwa wa ghafla usiku na mwanaume huyo alikwenda kumchukulia vidonge hivyo ambavyo havikuweza kumsaidia marehemu kupata nafuu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,  SACP Ulrrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema juhudi za kumtafuta mwanaume huyo zinaendelea huku madaktari nao wakiendelea na uchunguzi wao ili kubaini chanzo cha kifo hicho.
habari kamili :: read more...

Monday, April 28, 2014

Morgan Tsvangirai atimuliwa na chama chake cha MDC kwa utovu wa nidhamu.

Chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change MDC kimesema kimemsimamisha kazi kiongozi wake Morgan Tsvangirai kwa kukiuka kanuni za kidemokrasia.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa MDC Tendai Biti kufuatia mkutano wa chama hicho uliofanyika katika mji Mkuu Harare.

Tangu mwaka 2009 hadi 2013 Bwana Tsvangirai alitumikia taifa la Zimbabwe katika nafasi ya Waziri Mkuu katika serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa kwa pamoja na Rais wa sasa Robert Mugabe.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilifikia kikomo mwezi julai mwaka 2013 baada ya Rais Mugabe kushinda kwa wingi wa kura katika uchaguzi wa rais na Tsvangirai kususia uchaguzi kwa madai ya udanganyifu.

Kushindwa kwake kulipunguza nguvu yake kama kiongozi ambaye alikuwa mshindani mkuu wa Rais Mugabe.

Waangalizi wanasema ndani ya MDC kumekuwa na mgogoro wa kiuongozi kwa miezi kadhaa.

Viongozi wengine wa ngazi za juu wameripotiwa kusimamishwa katika mkutano huo uliofanyika siku ya jumamosi na wanachama wengine wa chama hicho watachukua nafasi zao.
habari kamili :: read more...

Angalia picha za mshikaji aiyenaswa akimla udenda mdada ndani ya DCM la Gungulamboto lilojaa kupindukia.

Watu hawana hata aibu kwani kubabanana mno kulisababishwa jamaa na manz mmoja ndani ya DCM linalofanya safari zake kati ya Ubungo na Gungulamboto kulambana LIVE wakiaamini kwa vile ilikuwa usiku na watu walijaa kiasi cha kukosa hata nafasi ya kugeuka ili watu wa jinsia Tofauti wasitazamane kushindikana Ndipo wawili hao walifanya Tukio hilo lililomshitua Mother mmoja mtu mzima aliewajia juu na kuleta Zogo ndani ya gari hilo.

Baada ya Zogo kuwa kubwa walijisikia aibu sana hali iliyowalazimu kuteremka maeno ya Tazara wakati safari yao ya GungulaMboto ilikuwa Bado.

Sijui nn kiliendelea manake Mpiga wetu aliyeripot taarifa anasema yeye aliendelea na Safari ya Gungula Mboto.
habari kamili :: read more...

Hivi ndivyo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ alivyomchefua Mbongo-Fleva Juma Kasim ‘Juma Nature’.


 PASUA jipu! Mastaa wawili wenye majina makubwa Bongo, mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Juma Kasim ‘Juma Nature’ wanadaiwa kuacha mshangao kwa wasanii wenzao baada ya kutifuana, Ijumaa Wikienda limeng’atwa sikio.


Mkali wa Bongo Fleva, Juma Kasim ‘Juma Nature’.

Pamoja na kwamba Nature amekuwa akizuga kutomaindi lakini habari za kushangaza zilidai kwamba mkali huyo wa Temeke amekuwa akimtuhumu mwanadada huyo kuwa amemuibia wazo lake la biashara ya ndala au kandambili.

Kabla ya madai haya mapya, Nature aliwahi kunukuliwa redioni wakati akitambulisha wimbo wake mpya wa Chuma Ulete kuwa yupo mbioni kuingiza bidhaa hiyo sokoni.
Madai ya sasa yanaeleza kwamba Nature amekuwa akilalamika kuwa Jokate ‘amekopi’ na ‘kupesti’ wazo lake la biashara.

Mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.

Pia ilisemekana kwamba Nature amekuwa akimtafuta Jokate ili kuweka suala hilo sawa bila mafanikio.
“Nature amekuwa akimpigia simu Jokate lakini haipokelewi,” kilidai chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa popote hata kwa mtutu wa bastola.

Kwa mujibu wa Nature bado hajabahatika kuziona kandambili za Jokate lakini amekuwa akiambiwa na watu wake kuwa mrembo huyo kamuibia.

NATURE AFUNGUKA
Alifunguka: “Hadi sasa hivi sijabahatika kuziona hizo ndala ila nishaambiwa na watu wangu wengi tu kuwa Jokate ameniibia wazo langu.

“Mimi nasema ni wizi wa ajabu ambao sikutegemea kama Jokate angenifanyia kitu mbaya.
“Kweli sikutegemea kama ishu kama hiyo ingefanywa na mtu kama yeye (Jokate) ila hata kama ametoa mimi wazo langu liko palepale.“Nitakuja kuzitoa tu hizo kandambili zenye picha na jina langu.”

Kandambili zilizosababisha mtifuano.

BOFYA HAPA KUMSIKIA JOKATE
Baada ya kusikia upande mmoja wa Juma Nature, kama ilivyo ada kupata mzani wa habari, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Jokate na kumsomea mashitaka yake hayo ya kuiba wazo la biashara la Juma Nature.
Bila kupepesa macho wala kuchezesha masikio, Jokate alifunguka kwamba kwa upande wake anasikitishwa na mtu kama Nature kumtuhumu kwani ni kati ya watu anaowaheshimu.

Jokate alikwenda mbele zaidi na kueleza kuwa mbali na kumheshimu pia ni kaka yake.
“Wewe siyo wa kwanza kusikia tuhuma hizo kutoka kwa Nature, niliamini baada ya mimi kutoa hizo ndala, atanisapoti kwani mimi niko katika kuendeleza na kutoa ajira kwa vijana wenzangu ili kulisukuma gurudumu letu la maisha.

MASIKITIKO
“Kweli Nature amenisikitisha sana kwa kitendo chake cha kunitangazia ubaya.
“Hata hivyo, siwezi nikaacha kutoa bidhaa zangu, nitaendelea kutoa ‘so’ itabidi tu anisamehe. Kama vipi na yeye atoe za kwake,” alisema Jokate, mmiliki wa lebo ya mavazi ya Kidoti.

MASTAA WANASEMAJE KUHUSU SAKATA HILO?
Wanahabari wetu walizungumza na baadhi ya mastaa ambao walionesha kushangazwa na sakata hilo huku wakihoji kulikoni Jokate na Nature kuhitilafiana wakati kazi zao zinategemeana.
“Unajua msanii kwa msanii kutofautiana kupo tu lakini kwa Nature na Jokate unajua ni watu ambao muda wowote wanaweza kukutana kwa ajili ya kufanya kazi,” alisema mmoja wa wanamuziki wakubwa wa Bongo Fleva.

NATURE KAMGEUKA JOKATE?
Kwa mujibu wa mastaa hao, awali Nature aliposikia Jokate ana ‘aidia’ kama hiyo alinukuliwa akisema freshi tu kwani ni msanii mwenzake hivyo kipato atakachopata kitamsaidia maishani lakini kumbe inawezekana kimoyomoyo ilimuuma ndiyo maana ameendelea kumtuhumu Jokate.

KUTOKA IJUMAA WIKIENDA
Ni vyema Jokate na Nature wakakaa na kukubaliana waifanye biashara hiyo kwa pamoja kwani itawaingizia kipato kikubwa zaidi, ni kiasi cha kuona fursa na kuitumia.

Kupata mapicha zaidi kuhusu mchefuo huo bofya hapa
habari kamili :: read more...

Huyu ndie msanii wa Bongo Movie aliyekubali kuigiza picha za NUSU UTUPU.

 MWANADAFADA mkali wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa kwa sasa yupo tayari kuigiza nusu utupu kwa sinema za nje ya nchi.

Mwanadafada mkali wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.

Akipiga stori mbili-tatu na kona hii, Batuli alisema kuwa muvi nyingi Bongo huwa zinafungiwa kwa kukosa maadili na kwamba kama ikitokea nafasi akaitwa nje ya nchi kuigiza sini hizo, atakuwa tayari.

“Zamani nilikuwa nikiogopa kuigiza nusu utupu. Wenzetu Nigeria wameendelea na ndiyo maana wanaigiza hata nusu utupu, kama itatokea nafasi ya kuigiza huko (nje ya Bongo) nusu utupu, nipo tayari,” alisema Batuli.
habari kamili :: read more...

Papa John Paul II na Papa John XXIII watangazwa kuwa ni watakatifu.

 
Umati mkubwa wa watu wamekusanyika mjini Vatican kushuhudia tukio la kihistoria ambapo viongozi wawili wa zamani wa Kanisa Katoliki,

Ibada iliyoendeshwa kwa pamoja kati ya Papa Francis na mtangulizi wake Papa Benedict XVI imeangaliwa na karibu mahujaji milioni moja na wengine mamilioni ya watu kupitia matangazo ya televisheni na redio.

Raisi wa Zimbabwe Robert Mugabe na Mkeo.

Karibu ujumbe wa wageni 100 wamehudhuria sherehe hiyo, wakiwemo kutoka koo za kifalme na wakuu wa nchi na serikali.

Hii ni mara ya kwanza kwa papa wawili kutangazwa kwa wakati mmoja kuwa watakatifu.

Waandishi wa habari wanasema hatua hii inachukuliwa kama njia ya kuziunganisha kambi mbili za wapenda mageuzi na wasiotaka mabadiliko ya sheria katika Kanisa Katoliki.

Papa John Paul II na Papa John XXIII wametangazwa watakatifu.

habari kamili :: read more...

Mashabiki wa Liverpool waanza maombi maalumu ili Everton iwafunge Man city.

 
Alikuwa ni Demba Ba aliyeanza kupeleka kilio kwa majogoo wa Liverpool pale alipounasa mpira kufuatia nahodha wa Liverpool Steven Gerrard kuteleza na Ba kupata mwanya wa kumfunga kirahisi Mignolet.

Liverpool hawakukubali kusalimu amri kwa wageni,kwani waliendelea kupeleka mashumbulizi ya hatari langoni mwa wapinzani wao wakiishia kwa kosa kosa. Liverpool wanapigania ubingwa wa ligi kuu ya England kwa mara ya kwanza katika miaka 24 iliyopita.Joe Allen na Luis Suarez walizidisha mashambulizi katika lango la Chelsea, kabla ya Willian aliyeingia kipindi cha pili kufunga bao la pili kwa timu yake ya Chelsea baada ya Fernando Torres bila uchoyo akiwa katika nafasi ya kufunga alimpasia Willian na kuwaachia kilio wenyeji wao Liverpool.

Chelsea katika mchezo huo ilikuwa ikipewa nafasi finyu ya kuibuka washindi. Lakini ni Jose Mourinho aliyeibuka na kicheko, huku Brendan Rodgers akiugulia kipigo cha kwanza kwa timu yake tangu kuanza kwa mwaka huu.

Kwa ushindi huo sasa, Chelsea inaachwa pointi mbili nyuma ya Liverpool ambayo inaoongoza ikiwa na pointi 80, baada ya michezo 36. Msimamo wa timu hizo ni Liverpool pointi 80, Chelsea 78, Manchester City 77, Arsenal ikichukua nafasi ya nne ikiwa na pointi 70.

Mashabiki wanaomba Man City aliyebakiza game 3 afungwe au atoke sare game moja kwani hali isipokuwa hivyo basi ndoto za Ubingwa kwa Liverpool hazitakamilika kwani Man city wanamzidi Liver kwa GD kubwa sana na point zitakuwa sawa kama wote watashinda mechi zao za mwisho.
habari kamili :: read more...

Sunday, April 27, 2014

DEREVA WA KAMPUNI AFUMWA AKINGONOKA NA KIKAHABA NDANI YA GARI HUKO MBAGALA.

Yelewiii!  Dereva ‘suka’ wa kampuni moja binafsi yenye makao yake makuu Kurasini jijini Dar (jina halikupatikana) Jumapili iliyopita alinaswa akifanya mapenzi na changudoa  ndani ya gari la kampuni hiyo, kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kilishuhudia tukio hilo laivu.

‘suka’ baada ya kunaswa akiwa na changu (kulia).
Dereva huyo akiwa na mwenzake walifika maeneo ya Mbagala Zakhem saa 7 usiku wa Februari 16, mwaka huu bila kujua kama OFM ilikuwa katika maeneo hayo kwa ajili ya kufanya oparesheni tokomeza machangudoa.

OFM ilimshuhudia dereva huyo na mwenzake wakishuka ndani ya gari aina ya Toyota Hilux (isiyokuwa na ‘pleti namba upande wa  mbele) mali ya kampuni  hiyo, wakiingia kwa fujo katika moja ya madanguro maarufu na kupaki gari  kisha wakashuka kuelekea kwenye danguro la machangudoa.

Baada ya muda, mmoja wao alirejea akiwa na changudoa maarufu kwa jina la Waluwalu na kujifungia ndani ya gari hilo.
Kama kawaida yake OFM iliwataarifu askari wa Kituo cha Kizuiani waliokuwa doria katika eneo hilo ambao kwa pamoja walilivamia gari na kumuamuru dereva  ashuke.

Hata hivyo, suka huyo alikuwa mbishi akaamua kufunga milango na kupandisha vioo ili asiweze kubughudhiwa na kile alichokuwa akikifanya ndani ya gari.
Askari waliokuwa na silaha wakalizunguka gari hilo na dereva huyo alipoona mambo yamekuwa magumu alifungua mlango na kutimua mbio lakini hakufika mbali kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi sambamba na changudoa aliyekuwa naye.
Akizungumza kwa hofu dereva huyo alisema, yeye na mwenzake ni madereva wa kampuni... (jina tunalo) na walikuwa maeneo hayo kwa bahati mbaya na si kama walifika kuwanunua machangu hao.
Dereva huyo alipotakiwa atoe sababu za kujifungia ndani ya gari hilo na changudoa kisha kutoa pleti namba ya mbele ya gari, alijitetea kwa kusema kuwa pleti namba ilidondoka barabarani tangu mchana, hivyo walikuwa wakimtafuta fundi ili awatengenezee.na Changu wakiwa na watuhumiwa wengine walionaswa katika operesheni tokomeza uchangudoa.

Alipohojiwa changudoa waliyekuwa naye, hakuwa na lolote la kusema zaidi ya kuangua kilio na kuomba aachiwe huku akilaumu ukali wa maisha kama sababu ya kujiingiza katika biashara ya kujiuza.
Wahusika hao walifikishwa Kituo cha Polisi cha Kizuiani kabla ya kesho yake (Jumatatu) kupelekwa Mahakama ya Jiji kusomewa makosa yanayowakabili
habari kamili :: read more...

HUYU NDIE DEMU WA KIBONGO ALIYENASWA AKIFANYA NG0NO LIVE HUKO UINGEREZA.

Imefahamika kwamba Shilla msichana wa kibongo aliyeko Rumande huko London/UK kwa makosa ya kufanya mapenzi in the public kumbe ni By-Sexual yaani ni msichana anayependa kufanya mapenzi na wanawake wenziwe na wanaume pia.

Habari hizo kutoka huko jela zinasema kwamba msichana huyu wa kibongo ambaye ameishi huko kwa muda wa Takribani Miaka zaidi ya 10 alianza kujifunza tabia hizo akiwa huko na mpaka kufikia sasa ambapo ni gwiji kabisa wa vitendo hivyo ambavyo nchini Uganda adhabu yake ni Kifungo cha maisha.
 Hatma ya msichana huyo mpaka leo bado kujulikana lakini inasemekana kuna uwezekano mkubwa wa kurudishwa bongo na Serikali hiyo. Stay tuned!!
habari kamili :: read more...

SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO ZAFANA JIJINI DAR ES SALAAM.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.

 Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa mwendo wa aina yake wakati wa sherehe za miaka 50 ya Muungano.

 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.


 Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.

 
Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka kutoka futi 4500 kwenye uwanja wa Uhuru kwenye kilele cha miaka 50.
Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais katika maonyesho ya Ndege yaliofanyika kwenye Kilele cha  Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.

 Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja matofali kwa kutumia kichwa na mikono.



  Baadhi ya silaha zakijeshi zikipitishwa mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa wa jeshi letu.
habari kamili :: read more...

Saturday, April 26, 2014

Tuwaenzi waasisi wa muungano.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameshikilia picha ya  Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage huku Rais wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar  Dk.Ali Mohamed Shein akiwa ameshikilia picha ya  Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume baada ya kuzipokea kutoka kwa vijana waliofanya matembezi ya Uzalendo.
habari kamili :: read more...

Kijiji cha ukahaba chafumuliwa mbagala.


watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi wa wananchi
SIKU  chache baada ya kuibua danguro la vigogo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na wahusika kutiwa mbaroni na polisi, mwishoni mwa wiki waandishi wetu wamekifumua kijiji cha ufuska.
  Kijiji hicho kilichogunduliwa Mbagala Zakhem, jijini Dar, wasichana na wavulana walinaswa wakifanya vitendo vya ngono kwenye moja ya mabanda ambayo yametengenezwa maalumu kwa shughuli hiyo.
Awali, waandishi wetu walipata taarifa kutoka kwa wasamaria za kuwepo kijiji hicho pembezoni mwa barabara ya kwenda Kiburugwa, hivyo kuamua kufuatilia.

Operesheni hiyo ilifanywa na waandishi wetu kwa kushirikiana na jeshi la polisi Jumamosi iliyopita usiku ambapo ilifanikiwa kuwanasa baadhi ya vijana akiwemo mwanamke mmoja aliyekutwa akifanya ngono na wanaume wawili (walio pichani).

Hata hivyo, kundi la watu kama wanane wakiwa na nguo mikononi walitimua mbio baada ya kuona polisi wamevamia chumba kimoja kilichotengenezwa kwa uzio wa vipande vya magunia chakavu na makaratasi walichokuwa wakikitumia kufanyia ngono.

 Aidha, wana usalama walifanikiwa kuwakamata watu watatu, wanaume wawili pamoja na mwanamke aliyejitambulisha kwa jina moja la Semeni waliyekuwa wakifanya naye mapenzi.
Baada ya kuwatia mbaroni watu hao na kuwafanyia upekuzi, walikutwa na kondomo na vipisi vya bangi.

 Gesti bubu inayotumika
Maafande walipomhoji Semeni alisema vijana hao walimlipa shilingi 5,000 kila mmoja na mmiliki wa eneo hilo aliyemtaja kwa jina moja la Babu walimlipa shilingi 2,000.
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo, aliwapongeza polisi kwa kufanikiwa kuwakamata baadhi ya vijana hao.

 “Kwa kweli sehemu hii ni kama kijiji cha ngono maana hata wanafunzi huchukuliwa
  na kuingizwa kwenye vibanda hivi kwa ajili ya kufanya ufuska, tunashukuru kwa kuamua kukisambatisha,” alisema jamaa huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
habari kamili :: read more...
 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top