Monday, April 28, 2014

Papa John Paul II na Papa John XXIII watangazwa kuwa ni watakatifu.

 
Umati mkubwa wa watu wamekusanyika mjini Vatican kushuhudia tukio la kihistoria ambapo viongozi wawili wa zamani wa Kanisa Katoliki,

Ibada iliyoendeshwa kwa pamoja kati ya Papa Francis na mtangulizi wake Papa Benedict XVI imeangaliwa na karibu mahujaji milioni moja na wengine mamilioni ya watu kupitia matangazo ya televisheni na redio.

Raisi wa Zimbabwe Robert Mugabe na Mkeo.

Karibu ujumbe wa wageni 100 wamehudhuria sherehe hiyo, wakiwemo kutoka koo za kifalme na wakuu wa nchi na serikali.

Hii ni mara ya kwanza kwa papa wawili kutangazwa kwa wakati mmoja kuwa watakatifu.

Waandishi wa habari wanasema hatua hii inachukuliwa kama njia ya kuziunganisha kambi mbili za wapenda mageuzi na wasiotaka mabadiliko ya sheria katika Kanisa Katoliki.

Papa John Paul II na Papa John XXIII wametangazwa watakatifu.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top