Monday, April 28, 2014

Mashabiki wa Liverpool waanza maombi maalumu ili Everton iwafunge Man city.

 
Alikuwa ni Demba Ba aliyeanza kupeleka kilio kwa majogoo wa Liverpool pale alipounasa mpira kufuatia nahodha wa Liverpool Steven Gerrard kuteleza na Ba kupata mwanya wa kumfunga kirahisi Mignolet.

Liverpool hawakukubali kusalimu amri kwa wageni,kwani waliendelea kupeleka mashumbulizi ya hatari langoni mwa wapinzani wao wakiishia kwa kosa kosa. Liverpool wanapigania ubingwa wa ligi kuu ya England kwa mara ya kwanza katika miaka 24 iliyopita.Joe Allen na Luis Suarez walizidisha mashambulizi katika lango la Chelsea, kabla ya Willian aliyeingia kipindi cha pili kufunga bao la pili kwa timu yake ya Chelsea baada ya Fernando Torres bila uchoyo akiwa katika nafasi ya kufunga alimpasia Willian na kuwaachia kilio wenyeji wao Liverpool.

Chelsea katika mchezo huo ilikuwa ikipewa nafasi finyu ya kuibuka washindi. Lakini ni Jose Mourinho aliyeibuka na kicheko, huku Brendan Rodgers akiugulia kipigo cha kwanza kwa timu yake tangu kuanza kwa mwaka huu.

Kwa ushindi huo sasa, Chelsea inaachwa pointi mbili nyuma ya Liverpool ambayo inaoongoza ikiwa na pointi 80, baada ya michezo 36. Msimamo wa timu hizo ni Liverpool pointi 80, Chelsea 78, Manchester City 77, Arsenal ikichukua nafasi ya nne ikiwa na pointi 70.

Mashabiki wanaomba Man City aliyebakiza game 3 afungwe au atoke sare game moja kwani hali isipokuwa hivyo basi ndoto za Ubingwa kwa Liverpool hazitakamilika kwani Man city wanamzidi Liver kwa GD kubwa sana na point zitakuwa sawa kama wote watashinda mechi zao za mwisho.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top