Tuesday, July 29, 2014

ALEX MASSAWE AFANYA KUFURU YA FEDHA SAUZI.



WAKATI akisakwa kwa udi na uvumba na serikali ya Tanzania ili kuunganishwa katika kesi ya mauaji jijini Dar es Salaam, mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe anadaiwa kufanya jeuri ye fedha nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’.

Mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe akiwa ndani ya gari.

Katika video iliyowekwa katika mtandao mmoja wa internet na kurushiwa kwenye gazeti hili juzi, inamuonesha mtu anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara huyo akiwa na afya njema, akiwa na kijana mmoja aliyekuwa akimsifia mzee huyo kwa kumiliki fedha nyingi na gari la kifahari la kutembelea aina ya Toyota Lexus.

Kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Floyd akitamba kuwa jina lake lingine la utani ni ATM Mashine, anasikika akimpamba mfanyabiashara huyo kuwa hana shida na fedha, kwani gari alilokuwa akiliendesha pekee lina thamani ya Dola za Marekani 120,000 (karibu shilingi milioni 200 za Tanzania).

SIKIA MAELEZO YA KIJANA
Huku wakiwa ndani ya gari moja, kijana huyo anasikika akisema: “Hi guys, huyu hapa ni Mr. Alex Massawe, anaendesha gari lenye thamani ya dola 120,000 za Marekani na hapa ana pesa anazokwenda kufanya ‘shopping’ pale Mike Ranger Mall. Ni fedha ndogo sana kwake.

Akionyesha jeuri ya pesa

Ni za kununulia nguo na viatu tu,” anasema kijana huyo mdogo huku video ikimuonesha mfanyabiashara huyo aliyewahi kutangazwa kuwa ni bilionea, akitoa burungutu la dola katika mfuko wa koti.

MWONEKANO WAKE
Katika video hiyo, mtu huyo anaonekana  akiwa amevaa suti nyeusi, kofia nyeusi, miwani, pete kwenye vidole vya mkono wa kushoto na akiashiria kujiamini kupita kiasi.

NJIANI KUPONDA RAHA
Aidha, kijana anayemsifia ambaye pia amejitambulisha kwa jina la Half a Billionaire Man, aliendelea kusema kuwa walikuwa njiani kuelekea kuponda raha, hasa kwa vile siku hiyo ilikuwa ni Jumapili.
Mkononi kijana huyo akaonekana ameshika dola alizopewa na mtu huyo na akasema ni 15,000 (kama shilingi milioni 25).

“Hatuna shida na fedha, tunazo na tunatumia bila wasiwasi, tunaendesha magari mazuri kama hili unaloliona, Lexus na Guchi,” aliendelea kutamba kijana huyo huku mtu huyo akiwa anaendesha gari lake kwa utulivu bila kusema neno.

Mfano wa gari analomiliki

WADAU WASEMA NI DHARAU
Baadhi ya wadau katika maoni yao walisema kama kweli mtu huyo ni Alex Massawe ni dharau kwa mamlaka zinazohusika nchini kwa vile mtu huyo anaonekana hana hofu yoyote huku serikali ya Tanzania ikimsaka na ni vigumu kumkamata  .“Kama kweli inamsaka, mbona anatanua bila wasiwasi wowote ule jamani?” alihoji mdau mmoja.

AMETENGENEZWA?
Baadhi ya watu walitilia shaka kuwa, huenda video hiyo ilitengenezwa lakini Uwazi iliipeleka kwa wataalam wa kompyuta IT ambao walipoiangalia walisema hakuna kilichotengenezwa, ni halisia. Uwazi lilichukua picha za video hiyo na nyingine kwa kuziweka pamoja zikaonesha kushabihiana kwa sehemu kubwa.

RPC KINONDONI AZUNGUMZA NA UWAZI
Baada ya kuinyaka video hiyo, Uwazi lilizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura ambaye anasimamia upelelezi wa tukio la mauaji ya mfanyabiashara aliyeuawa katika mkoa wake.

Mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe.

Yeye alisema: “Hilo suala lipo kwa Polisi wa Kimataifa (Interpol), wao wanamfuatilia kwa karibu sana. Atapatikana tu.”

KAMANDA KOVA NAYE
Baada ya hapo, Uwazi likamtafuta Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova ambaye alisema:

“Alex Massawe anaendelea kusakwa, Interpol inamfuatilia kila kukicha. Atanaswa tu.”
Aidha, Kamanda Kova alitaka kujua jinsi inavyopatikana hiyo video ambapo alielekezwa na mwandishi wetu.

DCI AONGEA
Uwazi likamsaka Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Tanzania DCI, Isaya Mngulu na kumuuliza anasemaje kuhusu mtu huyo kudaiwa ni Alex Massawe kutanua Afrika Kusini ambapo alisema:
“Kwanza niko nje ya nchi. Lakini Massawe anafuatiliwa kwa karibu na Polisi wa Kimataifa (Interpol). Kwanza tayari yuko kwenye mazingira mazuri ya kumkamata, tena muda si mrefu.”

MASSAWE AMEFIKAJE HAPA?
Massawe na mfanyabiashara mwenzake, Abubakar Marijani ’Papa Msofe’ na mtu anayejulikana kwa jina la Makongoro Nyerere (si wa hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere) wanadaiwa kuhusika na kifo cha mfanyabiashara Onesphory Kituly mwaka 2012 nyumbani kwake, Magomeni Mapipa jijini Dar.

Papa Msofe na Makongoro wapo Gereza la Keko, Dar kwa kesi hiyo huku Massawe akiwa anaendelea kusakwa aunganishwe na watuhumiwa wenzake hao.

Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

Share this article

1 comments:

  1. Huu ni lazima ushuhudia usomaji na kila mtu, nipo hapa kuruhusu ulimwengu wote kujua kuhusu mtu aliyeokoa uhusiano wangu na mtu huyu mkuu anaitwa Dr IZOYA. Hakika alifanya kazi nzuri kwangu kwa kumrudisha mpenzi wangu wa zamani ambaye aliniacha na kuahidi kamwe kurudi kwangu tena. Kwa hili, nimekuja kutambua kuwa kutoa maelezo ya Dk IZOYA kwa ulimwengu utafanya mengi mazuri kwa wale walio na nyumba zilizovunja au uhusiano kwa ajili yake ili kukusaidia kurekebisha uhusiano huo uliovunjika au ndoa yako. Unaweza kumfikia kupitia barua pepe yake: drizayaomosolution@gmail.com. Kuwasiliana naye na kuona jinsi tatizo lako litatatuliwa ndani ya 24hours. Pia mtaalamu katika mambo yafuatayo ...
    (1) Unataka kurudi nyuma yako.
    (2) Unataka kukuzwa katika ofisi yako.
    (3) Unataka wanaume / wanawake kukufuate.
    (4) Unataka mtoto.
    (5) Wewe ni mjasiriamali na unataka kushinda mikataba
    (6) Unataka mume wako awe wako milele
    (7) Unahitaji msaada wa kiroho.
    (8) Umeshambuliwa na unataka kupona fedha zilizopotea.
    (9) Weka talaka
    (10) Kualika kwa mila ya fedha
    (11) Chagua uchaguzi

    ReplyDelete

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top