Wednesday, June 11, 2014

Kamati ya Rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemrejeha Mgombea wa Urais wa Simba SC, Michael Richard Wambura.


Mgombea wa nafasi ya urais klabuni hapo, Michael Wambura.

RASMI Kamati ya Rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemrejeha Mgombea wa Urais wa Simba SC, Michael Richard Wambura kwenye mbio za kuwania uongozi wa Wekundu wa Msimbazi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Julius Lugaziya amewaambia Waandishi wa Habari mchana wa leo ofisi za TFF katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kwamba Wambura amerejeshwa baada ya kikao chao kilichodumu kwa siku mbili.

Baada ya mlolongo mrefu tangu juzi Saa 5:00 asubuhi hoteli ya Courtyad, Upanga, Dar es Salaam hadi jioni ya jana, Wajumbe wa Kamati hiyo waliamua kupiga kura kuamua na Wambura akapata kura tatu kati ya tano za kumkubalia aendelee na mbio za Urais Simba SC.

Ikumbukwe Wambura alikata rufaa TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kumuengua katika kinyang’anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC chini ya Mwenyekiti Wakili Dk. Damas Ndumbaro ilimuengua Wambura kwa sababu alikiuka Katiba ya klabu hiyo, TFF na FIFA kwa kuipeleka klabu hiyo mahakamani.

Tafadhali bofya like hapo juu kama bado hujabofya upate habari mpya haraka

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top