Tuesday, July 7, 2015

Ramadhani Singano "MESSI wa Bongo" huru kusajiliwa na Timu yoyote.

HATIMAYE Shirikisho la soka Tanzania limethibitisha kuwa mchezaji Ramadhani Singano ‘Messi’ kuwa yupo huru na anaweza kusajiliwa na timu yeyote itakayo muhitaji baada ya klabu yake aliyokuwa akiichezea siku za nyuma Simba kushindwa kutekeleza baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye mkataba.


Singano ameiambia Goal kuwa anafurahi haki yake kupatikana na baada ya muda mfupi ataweka wa zi timu ambayo ataichezea kuanzia msimu ujao lakini haitakuwa Simba kwa sababu nitimu ambayo haikupenda mafanikio yake.

“TFF imenitendea haki kwakweli hii ilikuwa haki yangu na ilikuwa wazi ila muda ulikuwa haujafika na washukuru viongozi wangu wa SPTANZA kwa kunisimamia na kuipata haki hii niliyoitafuta kwa siku nyingi,”amesema Messi.

Mchezaji huyo anatajwa kujiunga na Azam FC, baada ya kuonekana mara kadhaa akiwa na viongozi wa timu hiyo na pia uongozi wa timu hiyo umewahi kukiri kwamba unamuhitaji mchezaji huyo na kilichokuwa kikwazo kwao ilikuwa ni malumbano hayo ya kimkataba ambayo leo jioni yamefikia tamati kwa TFF kumuamuru mchezaji huyo yupo huru.

Tatizo kubwa lililokuwa linasumbua kati ya pande hizo mbili ni mkataba ambapo Messi alikuwa anasema mkataba wake umeisha baada ya msimu uliopita kumalizika wakati viongozi wa Simba walidai kuwa mkataba wa Messi ulikuwa unaishi msimu unaokuja wa 2015/16 na baadaye waliitwa na Secretarieti ya TFF Juni 9 na kutakiwa kukaa pamoja na kulimaliza tatizo hilo ikiwemo kuana upya mazungumzo ya kuingia mkataba mpya baada ya ile ya awali kuwa na mapungufu.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top