Monday, December 30, 2013

Vijana wazieni kazi mkiwaza kuwaridhisha wake zenu hamtafanikiwa.

Mzee mmoja (jina lake na mkoa anaotoka tunahifadhi)amewaasa vijana wasilimbuke na ngono na badala yake waelekeze nguvu zao katika ubunifu wa kujitafutia kipato.

Yeye ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 93 anasema shida za kutoaminiana ziko toka enzi hizo wala hazijaanza jana hivyo vijana wakibweteka kudhani eti kusalitiana kunatokana na kutoridhishana sio kweli kwani mwanamke ni mwanamke tu hata ungefanyeje.


Ushauri wake kwa vijana wote wachape kazi inayowaingizia kipato kitakachoweza kumudu maisha yao na ya jamii inayowahusu na sio kupoteza mda kufikiria kuridhishana.

Alisema "tendo la ndoa lina maliza nguvu nyingi sana sasa wako wanawake walevi wa ngono wanaweza kukufanya usiende kazini mshinde mkidu na hatma ya hilo ni umasikini".

Na ikumbukwe kwamba wako watu wengi wanaoishi duniani bila kufanya tendo la ndoa na hawapati shida zozote wakiwemo makasisi wa baadhi ya madhehebu.

Alisisitiza watu wafanye mapenzi kiafya sio kuoverdose eti kisa nimridhishe kumbe unajimaliza mwenyewe na baadae ukichoka atakuwa anatoka na watu wengine we si umemzoesha.

Akazidi kusema kuwa zamani watu waliishi miaka mingi kwa kufanya mapenzi kiafya yaani alitolea mfano kwa wiki mara moja tu ndo maana watu wakaishi hadi miaka 100 au zaidi lakini siku hizi mambo yamebadilika watu wanazingizia mabadiliko ya hali ya hewa kumbe wanajimaliza wenyewe.

Alisema kama baada ya kazi umechoka fuata burudani kama muziki au ngoma ambazo siku hizi hazipo sana na sio kuwahi nyumbani eti mkewe akakuburudishe ndo kwanza unazidisha shida.

Amewaomba vijana watumie asilimia 80% ya akili kufikiri juu ya ubunifu na mbinu mpya za kukabiliana na maisha na sio mapenzi kwani yapo tu na watayaacha.

Je Babu yuko sahihi?toa maoni yako
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top