Tuesday, December 31, 2013

Hivi ndivyo Police wa China walivyomnasa Jack Patrick na Heroin

Mambo yaliyochangia kunaswa kwake ni uso wa uchovu, kuanza kuwa na hali mbaya ya mwili,
kushindwa kujibu maswali vizuri na hati yake ya kusafiria (passport) yake kuonesha kugongwa mihuri ya kuingia nchini humo kila mara.

Habari zinasema ndipo maafisa wa uwanja huo walipomweka pembeni na baadaye kumpeleka kwenye chombo cha kukagua kwa undani mwili wa binadamu,
 walipojiridhisha ana ‘mzigo’ wakampa polisi mwanamke (WP) kwa ajili ya kwenda kusimamia utoaji wa kete hizo chooni kwa njia ya haja kubwa.


Baada ya kutoka chooni, ikafuata hatua nyingine. Jack aliwekwa mbele ya mapaparazi akiwa amevalishwa maski nyeusi usoni ili asionekane sura kisha akapigwa picha za kumwaga.

AVALISHWA MASKI, AWEKWA MBELE YA MAPAPARAZI




Sheria za Macau, mtuhumiwa huvalishwa maski usoni ili watu wasiione sura yake. Kete alizozitoa ziliwekwa juu ya meza, pia simu zake mbili, Iphone na Samsung nyeupe zilikuwa pembeni. Baadhi ya watu Bongo walizitambua simu hizo kwamba ni zake.

AINA YA MADAWA

Jack ambaye ni Miss Ilala Namba 3, 2005, alikamatwa na madawa aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 kwa kuhifadhiwa ndani ya kete 57.

 ATANYONGWA?

Kwa sheria za Beijing, China mtu akithibitika kubeba unga hukumu yake ni kunyongwa tu lakini waandishi wetu walipozungumza na wataalam mbalimbali wa sheria za kimataifa ili kujua ni adhabu gani inaweza kutolewa kwa mrembo huyo endapo atakutwa na hatia, walisema Beijing si Macau, ni vigumu kula kitanzi lakini kwenda jela miaka mitatu, minne au nane inaweza ikamhusu.

NANI YUKO NYUMA YA JACK?

Watu wengi (tukiwemo sisi) wana hamu kubwa ya kujua ni nani hasa anahusika na mzigo ambao msanii huyo anatuhumiwa kukamatwa nao. Katika pitapita ya waandishi wetu kupeleleza kwa undani suala hili, lilibahatika kuzungumza na baadhi ya watu ambao walihoji na kutaka kujua ni kigogo yupi yuko nyuma ya ishu nzima.

“Lazima kutakuwa na mtu nyuma yake, si bure nyie fuatilieni sana,” alisema mdau mmoja ambaye hakupenda jina lake litajwe mahali popote.

Aliongeza kuwa, mtu anayekutwa na kete za unga tumboni maana yake katumwa (punda) na bosi wake, kwa hiyo suala kubwa kwa sasa ni kumsaka bosi huyo ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.


Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top