Tuesday, December 31, 2013

Kijana ataka kujirusha katika mnara wa simu Ubungo Dar.Askari Zimamoto na Uokoaji wamdhibiti.


Askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji wamefanikiwa kuzima jaribio la kujirusha la kijana mmoja aliyetaka kujirusha maeneo ya ubungo Dar kama hataonanan na rais kisa kesi aliyebambikizwa na polisi.


 
Askari wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji Wakiwa wamepanda juu ya Mnara wa Simu Uliopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam mda mfupi uliopita kwaajili ya kumuokoa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Hassan.

Kijana huyo alipanda juu ya mnara huo kwa lengo la kufikisha Ujumbe wa kutaka kuonana na Raisi Kikwete  ili aweze kumwelezea kwa kile anachodai kuwa jeshi la polisi lilimbambikia kesi na
 hatimaye kuhukumiwa kifungo cha Miaka 6 kwenda jela.


 Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea na zoezi la kumuokoa Kijana Hassan na sasa wamemweka begani kushuka nae mdogo mdogo.

Kijana enaeleza nini kilimfanya achukue maamuzi hayo.

Wananchi wakihairisha shuguli zao kushuhudia tukio hilo.

Mwishowe gari la Polisi likiondoka na Kijana Hassan.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top