Tuesday, December 16, 2014

Wema Sepetu Alisusa Gari Aina ya Murano Alilopewa Kama zawadi na Diamond Platnumz.


LILE ndinga aina ya Nissan Murano alilozawadiwa supastaa Wema Sepetu na aliyekuwa mchumba wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’, limeanza kumchefua mrembo huyo kiasi cha kulisusa.

Tukio hilo lilijidhihirisha wazi mbele ya paparazi wetu juzikati nyumbani kwa staa huyo, Kijitonyama jijini Dar, ambapo Wema alitamka hadharani kuwa kwa sasa analichukia kupita maelezo gari hilo alilozawadiwa na Diamond kwenye sherehe yake ya kuzaliwa.

“Bwana acha nitumie hili gari lingine kwenda airport hilo Murano sitaki hata kulisikia, sijui najisikiaje hata nikiliona,” alisikika Wema.Paparazi wetu baada ya kusikia Wema akionesha wazi kuwa analichukia gari hilo, alimuuliza sababu inayomfanya alichukie ambapo alisema hajui ni kwa nini analichukia ingawa ni mali yake.

“Siku hizi sipendi kutumia hili Murano tena nalichukia kweli, inafikia kipindi nakosa raha nikiliona lakini ukiniuliza sababu ya kulichukia kiasi hicho hata sina sijui nimezoea sana kutumia BMW, ndiyo maana najikuta nalichukia gari hili,” alisema Wema.

Kwenye bethidei yake iliyofanyika Septemba, mwaka huu, Wema alizawadiwa magari mawili. La kwanza lilikuwa ni BMW 545i (Sh. Milioni 56) ambalo liliibua utata juu ya mtu aliyemzawadia na la pili ni Nissan Murano (Sh. milioni 36) alilopewa na Diamond

Inasemekana Beyonce na Jay Z wameiba wimbo wao wa ‘Drunk in Love’.



UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top