Sunday, October 26, 2014

Mbunge Shy-rose Bhanji azua timbwili ndani ya ndege.

Mbunge kijana anayewakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Shyrose Bhanji, anadaiwa kuwa chanzo cha kuvunjika kwa vikao vya bunge hilo vilivyokuwa vikifanyika Kigali nchini Rwanda.

Gazeti la New Times la Rwanda limeandika kuwa Bi Shyrose aliporomosha matusi mazito na maneno ya kashfa dhidi ya wabunge wenzake na viongozi wa mataifa kadhaa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hilo ndilo linalodaiwa kusababisha kuvunjika kwa vikao ambapo wabunge wenzio walimtaka Spika wa EALA, Bi Margret Nantongo Zziwa, amchukulie hatua Shyrose lakini hawakufanikiwa.

Kando na hilo kumekuwa na ujumbe unaosambazwa katika Whatsapp ukidai kwamba mbunge huyo alianzisha ugomvi ndani ya ndege wakati yeye na wabunge wenzake wakisafiri kwenda Ubelgiji hivi karibuni kwa shughuli za kikazi. Inaelezwa alikuwa kaambatana na wabunge wengine kutoka Tanzania, Adam Kimbisa na Angela Kizigha.

Hata hivyo Taarifa News haikufanikiwa kumpata Shyrose kujieleza kuhusu tuhuma hizo nzito na ambazo kama atapatikana na hatia kupitia taratibu za EALA anaweza kufukuzwa kutoka bunge hilo.

MGOMBEA 2015 ANASWA NA DENTI DOGO DOGO KABISA AKIMNANILII GESTI; PICHA LIVE ZA TUKIO HIZI HAPA.



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top