Thursday, June 12, 2014

Ukatili kwa wanawake bado unaendelea India, Mwanamke mwingine abakwa na kuning’inizwa juu ya mti.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 19 amekutwa amening’inizwa juu ya mti katika kijiji kimoja Kaskazini mwa India, likiwa ni tukio la tatu kutokea ndani ya wiki moja katika Jimbo la Uttar Pradesh.

Mwili wa mwanamke huyo umekutwa katika eneo la Moradabad ambapo familia yake imewaambia polisi kuwa alibakwa huku uchunguzi wa madaktari ukiendelea kufanyika.

Mwanamke mwingine alikutwa amening’inizwa juu ya mti katika Jimbo la Uttar Pradesh siku ya Jumatano.

Mwezi uliopita mabinti wawili wadogo walibakwa na kundi la watu katika mazingira kama hayo na kuibua maandamano ya hisia kali nchini India.

indiateen

Siku ya Jumatano, mwanamke mwenye umri wa miaka 44 nae alikutwa amening’inizwa juu ya mti katika eneo la Bahraich.

Polisi wamesema kuwa alikuwa akipatiwa vitisho na wanakijiji kwa kuuza pombe katika eneo hilo na familia yake ilifungulia kesi watu watano kuhusiana na kifo hicho.

Tafadhali bofya like hapo juu kama bado hujabofya upate habari mpya haraka

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top