Nilihangaika sana namna ya kumpata lakin nilikuwa naogopa kutongoza kipindi hicho. Ikabidi nimweleze kaka mmoja ambaye ni mkubwa kwangu kumbe naye domo zege akanishauri niende kwa mganga ili anipe dawa ya mapenzi.
Kipindi hicho hata hela sina sikuwa na uwezo wa kupata ikabidi nikaenda kweli kwa mganga. Yule mganga akaniambia dawa ipo lakin nmpe shilingi elfu 2.
Nikaumiza kichwa namna ya kuipata nikaona ngoja nimdanganye baba kuwa nmepoteza kitabu cha mwalim,nilipomweleza baba akanipa hyo hela nikaenda kumpa yule mganga naye akanipa dawa nikarudi nyumban.
Nikaanza kila asubuhi napaka ile dawa nikiwa naenda shule na namsubir huyo Rusi tunaongozana huku nikisubiri yeye ndiyo aanze kuniambia ananipenda kwasababu nilijua ile dawa itamvuta na anipende.
Nikaona wiki inakatika Rusi hana mpango hata wa kunitamkia kuwa ananipenda nikazidi kujisiliba hayo mafuta ya dawa lakin kimya. Nikaona acha nibadili dini nimfuate anakosali yeye huku nikizidi kupaka ile dawa lakin hakuna hata siku moja aliyoweza hata kunichekea. Nikaishiwa nguvu baada ya kuona dawa inaisha bila hata kuona tabasam la Rusi pamoja na jitihada zote. Tangu siku hyo simwamini mganga yoyote nyamaafu
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment