Thursday, June 12, 2014

Mapigano makali yamezuka kati ya Majeshi ya DRC na Rwanda huko Kivu.

Maafisa wakuu katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo wanasema kuwa makabiliano makali yalizuka mapema leo kati ya wanajeshi wa DRC na wanajeshi wa Rwanda.

Waziri wa mawasiliano, Lambert Mende, anasema kuwa makabiliano hayo yaliendelea kwa muda na kuendelea kwa saa kadhaa katika eneo la mpakani kati ya nchi hizo mbili.Alisema makabiliano yalianza wakati wanajeshi wa Rwanda walipovuka na kuingia katika mkoa wa Kivu na kumkamata mwanajeshi wa Rwanda.

Hadi sasa hapajakuwa na tamko lolote kutoka kwa upande wa Rwanda.

Serikali ya Rwanda imetuhumiwa na Umoja wa Mataifa kwa kuhusika na mzozo unaotokota katika mashariki ya Jamhuri ya Congo.

Rwanda imekanusha adai hayo.

Tafadhali bofya like hapo juu kama bado hujabofya upate habari mpya haraka

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top