Friday, June 13, 2014

Lulu akiri kuwa Nando aliwahi kumtokea na alimkubalia awe ‘my baby’ wake lakini baada alimpotezea.

 Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibuka na kufunguka kuwa amekerwa na kitendo cha mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa (BBA) 2013, Amir Khan Nando kujinadi kuwa aliwahi kuwa ‘mtu’ wake kitu ambacho si cha kweli.

Akizungumza na Ijumaa kwa juzikati, Lulu alikiri kuwa Nando aliwahi kumtokea na alimkubalia awe ‘my baby’ wake lakini baada ya kumshtukia kuwa hana nia nzuri, alimpotezea kabla hawajazama kwenye dimbwi la mahaba.

“Nahisi Nando alikuwa kwanza anataka kiki kupitia mimi na ndiyo maana kila alipotaka kupiga picha na mimi, nilimkatalia coz nilishamgundua nia yake, nimemshangaa kweli alipotangaza kuwa niliwahi kuwa mpenzi wake labda alivyonitokea na kumkubalia lakini sikufanya naye chochote kinachohusu mapenzi ndiyo akaona aseme hivyo,” alisema Lulu.

Tafadhali bofya like hapo juu kama bado hujabofya upate habari mpya haraka


Amir Khan Nando akiwa kwenye mahojiano na Global TV Online ndani ya ofisi za Global Publishers

Juzikati, Nando alifanya mahojiano na Global TV Online ambapo awali alidai ‘kutembea’ na Lulu lakini alipobanwa zaidi aliumauma maneno na kudai anampenda na yuko tayari kumuoa kwa sababu ana sifa za kuwa mke (wife material).
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top