Thursday, June 12, 2014

Breaking;MABANDA YA WAMACHINGA ENEO LA KARUME YAMETEKETEA KWA MOTO USIKU KUAMKIA LEO.

Moto ukiwa unaendelea kuwaka katika soko la Karume 'Mchikichini' ukiendelea kuteketeza mabanda.
Hali ilikuwa tete usiku wa kuamkia leo katika mabanda ya Wamachinga eneo la Soko Karume 'Mchikichini', Ilala jijini Dar, baada ya kutokea moto mkuwa na kuteketeza mabanda ya wafanyabiashara eneo hilo. Fire walifika katika eneo la tukio na kuondoka baada ya kukubali kushindwa kuzima moto huo hakuna walichoweza kuokoa.

Nguzo za umeme zimeungua pia Vilio vinaendelea eneo hilo!
Chanzo kinadaiwa kuwa ni sehemu ya Mama ntilie ambao inasemekana huchemsha maharage na kuyaacha usiku ili yaive vizuri.

Tafadhali bofya like hapo juu kama bado hujabofya upate habari mpya haraka

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top