Friday, May 30, 2014

Wasichana watatu wabakwa na kuning'inizwa kwenye mt huko India.

Takribani wanaume watatu akiwemo afisa mmoja wa polisi tayari wamekamatwa kuhusiana na tukio la kubakwa kwa wasichana wawili wadogo na kundi la watu na kuning’inizwa juu ya mti huko nchini India.

Mamlaka katika Jimbo la Utter Pradesh limesema kuwa bado linamsaka mtu mmoja ambaye anatuhumiwa kuwepo katika kundi hilo lililohusika kufanya tukio hilo la kusikitisha.

Familia za wahanga wa tukio hilo zimesema kuwa mara ya kwanza polisi walikataa kuwasaidia katika kuwatafuta watoto hao baada ya kupotea ambapo matukio ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake nchini India bado yameendelea kuwa tatizo kubwa.

Wanakijiji walikuta miili ya wasichaa hao wenye umri wa miaka 14 na 15 ikiwa inaning’inia juu ya mti wa maembe saa chache baada ya kupotea nyumbani katika kijiji cha Katra kilichopo kwenye jimbo la Utter Pradesh.
Wasichana hao walikuwa wamekwenda vichakani kuoga kutokana na kutokuwa na vyoo nyumbani kwao ambapo mamia ya wanakijiji wenye hasira walikusanyika katika eneo hilo la mti kwa siku nzima wakiandamana kushinikiza polisi kukabiliana na vitendo hivyo.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top