Monday, March 31, 2014

Wanaharakati wamuunga Kikwete kwa kuzindua Kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo).


Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr. George Nangale, akizindua rasmi kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kwa niaba ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kama jitihada za kumuunga mkono Rais Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini. Kushoto ni Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi, Wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, na Kulia ni Dr. Herry Muhando kutoka International Evangelist.

Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi, akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kupitia Taasisi yake kama jitihada za kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini. Wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, Wa pili kulia ni Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr. George Nangale (kwa niaba ya Rais Kikwete) na Kulia ni Dr. Herry Muhando kutoka International Evangelist.



Meneja Biashara wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Basel Haydar (kushoto) pamoja na Meneja Mauzo wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Emmanuel Okware.

Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza akisisitiza jambo ambapo ametoa rai kwa wadau mbalimbali pamoja na mataifa mengine kuunga mkono jitihadi hizi kuhakikisha ujangili unatokomezwa.
Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania imezindua kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kama jitihada za kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini.

Mratibu wa taasisi hiyo, Robert Zangi, amesema wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwamba wameamua kumuunga mkono Rais Kikwete kutokana na kukithiri kwa matukio ya ujangili wa wanyamapori miaka ya hivi karibuni.

Aliongeza kwamba kampeni hiyo itawalenga zaidi watu ambao wanaishi jirani na mbuga za wanyama.

“Watu wanaoishi jirani na mbuga za wanyama ni rahisi kufahamu nani ni jangili na nani ni raia mwema miongoni mwao,” alisema.

Aliongeza kusema kwamba kampeni hiyo itawafikia watu wanaoishi jirani na mbuga za wanyama kwa lengo la kuwaelimisha umuhimu wa kupambana na jangili dhidi ya wanyamapori.

Kampeni hiyo ina mpango wa miaka mitano ambao kwa kuanzia kutakuwa na matukio matatu makubwa mwaka huu kati ya sasa hivi na mwezi Mei.

Tukio la kwanza, alisema, ni la uzinduzi wa kampeni hiyo na la pili ni kuwasilisha ujumbe wa kampeni kwenye Umoja wa Mataifa nchini Marekani tarehe 9 mwezi Aprili na la tatu litakuwa ni semina juu ya kupambana na mauaji ya Tembo, Vifaru na wanyamapori wengine.

Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr George Nangale, amesema kwamba wanaunga mkono kampeni hiyo kwani mauaji ya wanyamapori ni majanga na kwamba watu wanaoishi jirani ya mbuga za wanyama wanaweza kusaidia sana kwenye mapambano dhidi ya ujangili.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top