Wednesday, March 12, 2014

Taarifa kamili kuhusu ile ajali ya basi la HOOD iliyotokea jana huko Same - Mwanga.

 Basi la Hood linalofanya safari zake kutoka Arusha kwenda Mbeya, namba za usajili T.488 AXV aiana ya Scania ilipata ajali mbaya jana  majira ya saa 3 asubuhi na kusababisha kifo cha Mtu mmoja na kujeruhi wengine 16.

Ajali hiyo imetokea katika, barabara ya Same - Mwanga, Kijiji cha Kiverenge wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro ambapo taarifa za awali zinasema  kuwa chanzo chake ni kupasuka kwa tairi ya mbele.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema katika ajali hiyo alifariki Abiria mmoja aliyemtaja kwa jina la Joshua Likumbia, Raia wa Kenya, ambaye alikuwa akisafiri kuelekea jijini Mbeya.
Kamanda Boaz amesema majeruhi katika ajali hiyo ambao ni 16, akiwemo dereva wa Basi, Fadhili Hashim wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Same na Hospitali ya Rufaa mkoani Kilimanjaro, KCMC.


Kamanda Boaz ameendelea kufafanua kuwa majeruhi hao nane wamelazwa Same huku wengine 8 wakikimbizwa mjini Moshi katika hospitali ya KCMC kutokana na hali zao kuwa mbaya ambapo watatu kati yao wakia wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top