Mchungaji Mtikila aliyasema hayo juzi katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma kutokana na mwenendo usioridhisha wa Bunge hilo.
Alisema Bunge hilo ni kwa ajili ya kupoteza fedha za walipakodi zinazotumika katika kuwalipa posho wajumbe ambao hawana kazi ya kufanya.
Alisema wajumbe wa Bunge hilo wanapoteza muda wao kwa kupingana na misimamo ya CCM na matokeo yake ni malumbano yasiyokuwa na tija.
“Kila siku nimekuwa nasema kuwa kinachoendelea hapa ni usanii mtupu, kama kweli sisi ni watu wa kumwogopa Mungu, basi tukubali kuziacha posho zetu na turudi nyumbani,” alisema Mchungaji Mtikila.
Alisema CCM kupitia wajumbe wake, kinataka kulazimisha mchakato wa Katiba, jambo ambalo alisema ni kutengeneza bomu kubwa kwa Taifa.
Hata hivyo, alisisitiza msimamo wake wa kwenda mahakamani kabla ya kumalizika kwa Bunge na kwamba safari hii hakuna atakayechomoka kwa sababu ana ushahidi wa kutosha.
“Posho hizi walizonilipa, nitazitumia katika kutafuta haki na uhuru kamili wa Watanganyika, najua kabisa kuwa kwa uzembe walionao, hata kama nikiwakuta majaji wabovu mahakamani, kesi hii nashinda tena kwa urahisi,” alisema Mchungaji Mtikila.
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment