Wednesday, March 12, 2014

Mjamzito aliwa uroda gesti na mshikaji hadi kupata uchungu na kujifungua huko Moro.

 MJAMZITO wa miezi saba Bi. Mwanaidi Athumani mkazi wa Chamwino Morogoro hivi karibuni alifanya mchepuko wa kutoka nje ya ndoa na kujikuta akijifungua mtoto wa kiume ndani ya gesti iliyopo maeneo ya Mafisa mjini hapa, Risasi Mchanganyiko lina data za kutosha.

Habari zinasema kuwa mwanamke huyo alifanya mchepuko huo baada ya mumewe kusafiri kwenda kutafuta fedha za maandalizi ya kujifungua kwake.

Bila ya kujali kama ana mimba ya miezi saba, Mwanaidi aliingia katika gesti moja (jina tunalo) akiwa na mwanaume anayedaiwa kufanya kazi ya kupiga debe katika stendi ya Msamvu na mambo yalipomwendea kombo, mwanaume huyo akatimua mbio.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, Mwanaidi na mpiga debe wake walipanga katika chumba namba 3 na baada ya kufanya mambo yao, Mwanaidi akaanza kupiga kelele kutokana na kushikwa na uchungu. Ilimbidi mhudumu wa gesti hiyo, Bi. Moshi Eliya afike kumsaidia Mwanaidi aweze kujifungua salama pamoja na kwamba hakuwa na ‘gloves’ wala kitu chochote cha kulinda afya yake.

Chanzo chetu ambacho nacho kilikuwa ni mpangaji ndani ya gesti hiyo kilisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 8 usiku na Mwanaidi alipiga kelele huku akizozana na mpiga debe wake. Kiliposikia tukio hilo, chanzo hicho kikapiga simu kwa paparazi wetu aliyetinga katika nyumba hiyo ya wageni kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo.

Baada ya kujifungua salama, paparazi wetu alimuuliza Mwanaidi kilichotokea ndipo mwanamke huyo akafunguka kuwa alikuwa amechepuka nje ya ndoa baada ya kukumbwa na shetani.


“Nina mume na tuna watoto watatu huyu ni wanne, mume wangu amesafari kwa ajili ya kutafuta fedha za maandalizi ya ujuo wa mwanetu akijua nina mimba ya miezi saba,” alisema mwanaidi. Pamoja na kutaka kugoma, lakini mwandishi wetu alimchukua mwanamke huyo na kichanga chake na kuwapeleka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako wamelazwa kwa uchunguzi zaidi.

Mhudumu wa gesti hiyo, Bi. Moshi Eliya ambaye alikuwa mkunga wa Mwanaidi alisema kuwa alishindwa kutumia ‘gloves’ wakati wa kumzalisha mzazi huyo kwa kuwa alikumkuta mtoto ameshaanza kutoka. “Mtoto aliashaanza kutoka, hata hivyo kwa usiku ule tungepata wapi hizo gloves?” alihoji.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top