Saturday, March 29, 2014

Kitale adaiwa kula michango ya kumbukumbu za Sharo Milionea.

 Msanii wa vichekesho Musa Kitale.
Makubwa! Mama mzazi wa aliyekuwa nyota wa filamu na muziki, marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ amemtuhumu msanii wa vichekesho ambaye alikuwa rafiki wa mwanaye, Musa Kitale kuwa alikula michango ya kumbukumbu ya kifo cha mwanaye, mwaka jana.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Mama Sharo amekuwa akimlalamikia Kitale kwa watu kwamba alikula fedha za mchango wa mwanaye hivyo kupigwa marufuku kwamba kitu chochote kinachomhusu Sharo asipewe.

Mama yake na marehemu Hussein Mkieti  aka ‘Sharo Milionea’ .

Ilidaiwa kwamba, chanzo cha mama Sharo kutaka Kitale asipewe kitu chochote kinachomhusu marehemu ni baada ya hivi karibuni Klabu ya Bongo Movie Unity kutangaza kuwa litatoa Tuzo kwa Sharo Milionea kama kumbukumbu kwani alikuwa ni mwenzao katika tasnia ya filamu.

Ilisemekana kuwa mama huyo alielezwa kwamba tuzo hiyo itapokelewa na Kitale ndipo alipokataa na kusema hataki kabisa kitu chochote kipitie kwa msanii huyo kwa sababu huwa hamfikishii.

“Mama Sharo amekuwa akilalamika kwa muda mrefu sana kwamba Kitale anatumia vitu vya mwanaye, eti alichangisha michango ya kumbukumbu hakumfikishia hivyo kwa sasa ameamua kupiga marufuku asikabidhiwe kitu chochote,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupata habari hizo, wanahabari wetu walimtafuta Kitale ambapo kabla hata ya kujibu tuhuma hizo, alinyanyua simu na kumpigia mama Sharo kumuuliza kama kweli amezungumza madai hayo.

Mama Sharo alikiri kuwa ni kweli alizungumza akidai alifikia uamuzi huo baada ya kutonywa na watu kuwa Kitale amekuwa ‘akichikichia’ fedha za marehemu mwanaye.

Kitale, baada ya kujiridhisha, alitoa ufafanuzi kuwa madai hayo hayana ukweli na kudadavua kwamba wakati wa kumbukumbu ya Sharo mwaka mmoja (Novemba) tangu alipofariki dunia, hakuna michango yoyote iliyotolewa.

“Inaniuma sana kwa sababu enzi za uhai wa Sharo hatukuwahi kugombana hata siku moja na mama Sharo alikuwa analitambua hilo, tuliishi kama ndugu na mimi ndiye niliyemsaidia mpaka akapata umaarufu lakini sasa namshangaa huyu mama kunishutumu vitu vya uongo,” alisema Kitale kwa huzuni huku jasho likimtiririka.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top