Saturday, March 29, 2014

Breaking news:: Ajali mbaya ya Toyota Pick Up kugongana na lori imetokea Same na kuua watu 12 .


Watu 12 waliokuwa wanasafi kuelekea kwenye msiba kwa kutumia gari aina ya Toyota Pick Up kwenda katika msiba wa jaama yao kumuhani msiba ulikuwa katika kijiji cha Kongei, Kata ya Hedaru, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro wamekufa papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya gari lao kugongwa na malori mawili ya mizigo.


Ajali hiyo ambayo ilitokea katika muda wa usiku katika barabara kuu ya Moshi, Chalinze katika eneo la hedaru ilisabababisha magari matatu ambayo ni Fuso lenye namba za usajili T 299 ANM likitokea Moshi kwenda Dar es Salaam na Scania namba T 737 AKW lenye tela namba T 776 CCN ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Moshi Kwa mujibu wa Kamanda Boaz.Aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Stella John (45), Salma  Kizoka (33), Marry Senzige (49), Neema Daniel (52), Rehema George (29), Sophia Mbike (51), Mama Ritta Kallani (55), Mama Kallan Stephano
(55), Kolina Mmasa (55), Bahati Daudi (25), Farida Kiondo (24) na Maria John (33) wote wakazi wa Kongei,Kata ya Hedaru,Tarafa ya Chome-Suji. Hata hivyo, miili ya marehemu hao
imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top