Wednesday, March 12, 2014

Inahuzunisha sanaa!! Mtoto aliyekatwa koromea na Baba yake afariki Dunia.

Mtoto Said Siraji akiwa amelazwa hospitalini baada ya kukatwa shingo na Baba yake
Mtoto Said Siraji(13), mkazi Majengo Kaskazini wilayani Kahama mkoani Shinyanga aliyedaiwa kukakatwa shingo na baba yake usiku wa kuamkia Machi nne mwaka huu, amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando mjini Mwanza.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo Kaskazin Noel Makula Mseven amesema Marehemu Siraji aliyekuwa anasoma darasa la tatu katika Shule ya Msingiya Majengo amefariki akiwa Bugando alikokuwa amelazwa kwa matibabu zaidi mara baada ya hali yake kuwa mbaya katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
Kwa mujibu wa mama mzazi wa Siraji Mariamu Idd awali alieleza, siku ya tukio Marehemu Siraji alichukuliwa na baba yake mzazi anayeitwa Siraji Salvatory(45) kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa wazazi hao walikwishaachana siku nyingi
Alfajiri ya Machi nne Salvatory ambaye kwa sasa yuko Rumande alimchukua Siraji na kumpeleka kwenye makaburi ya majengo kwa nia ya kumchinja lakini hakufanikiwa kumuua huku akimwachia jeraha likimwaga damu nyingi kabla hajaokotwa na wasamaria na kupelekwa hospitalini.
Museven amesema Julai mwaka jana Salvatory alitaka kumchinja mke wake Mariam lakini akaokolewa na Mseven kitu kilichomuuzi salvatory na kutaka kumchinja mwenyekiti huo wa kitongoji tuhuma iliyompeleka gerzani kwa kipindi cha miaka miwili..
Hata hivyo mseven amesema siku amemwokoa mariam Salvatory alitaka kumchinja mtoto wa jirani ili kutimiza azma yake ikashidikana hali inayodhaniwa sasa imekamilika baada ya kumchinja mtoto wake Marehem Siraj

Habari ambazo hazijathibitishwa na idara ya upelelezi wilayani humo zimesema, Salvatory amewaeleza maafisa wa polisi kwamba kitendo hicho amekifanya kwa lengo la kulipa mchango wa Freemason na kwamba alitaka kuchangia damu ya mtoto mdogo akakataliwa.
Mauaji haya yametokea kwa wakati jamii ya wana kahama inakabiliwa na balaa la kuamini vitu na mambo yasiyo na msingi kama lile la kubaini wachawi na imani ya Freemason ambayo haijulikani hata ilikotoka wala msingi wake.
CHANZO : MDOSOAJI
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online