Friday, February 14, 2014

Wassira na January Makamba wamehojiwa leo na Kamati ndogo ya maadili CCM Dodoma.

WASSIRA: HAKUNA TUHUMA DHIDI YANGU


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu ) Ndugu Stephen Wassira akitoka nje ya ukumbi wa White House baada ya kumaliza mahojiano na Kamati Ndogo ya Maadili.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu ) Ndugu Stephen Wassira akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi,Wassira aliwaeleza waandishi kuwa hakukuwa na tuhuma juu yake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu ) Ndugu Stephen Wassiraakifurahia jambo na Kada Maarufu wa CCM Ndugu Adam Soud mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandishi wa habari leo mjini Dodoma.


JANUARY MAKAMBA BAADA YA KUHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI LEO MJINI DODOMA


Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu January Makamba akizungumza na waandishi wa habari nje ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi baada ya kuhojiwa zaidi ya saa moja na nusu na Kamati Ndogo ya Maadili.


Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu January Makamba akiondoka nje ya ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi baada ya kumaliza kuhojiwa kwa  zaidi ya saa moja na nusu na Kamati Ndogo ya Maadili.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top