Wednesday, January 29, 2014

Picha za Jengo la JMC lilivyonusurika kuungua na moto leo:





 Wafanyakazi kutoka Kampuni ya Ultimate Security wakiwa eneo hilo kuongeza nguvu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (kulia) akipata maelezo ya awali kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi.


Maofisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi wakiwa eneo la tukio.
JENGO la JMC linalomilikiwa na Zhihir Shivji lililopo eneo la Kamata mtaa wa Kasanga, Kiriakoo jijini Dar es Salaam leo majira ya saa nane mchana lilinusurika kuteketea kwa moto ulioanzia ghorofa ya saba.
Chanzo cha moto huo na mali zilizoteketea mpaka sasa bado havijafahamika.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alifika eneo la tukio na kuagiza wamiliki wa majengo kuweka vyombo vya kutambua hitilafu mbalimbali kwenye majengo yao.
Katika tukio hilo hakuna majeruhi yeyote aliyeripotiwa.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top