Mmiliki
wa kampuni ya Microsoft Bill Gates amekunywa maji yaliotengenezwa
kutokana na kinyesi cha binaadamu kama maonyesho ya teknolojia mpya
itakayoweza kutoa maji safi katika mataifa yanayoendelea.
Mwanzilishi
huyo wa Microsoft amesema kuwa ataisambaza mitambo ya teknolojia hiyo
mpya kote duniani baada ya kuifanyia majaribio mwishoni mwa mwaka
huu.Teknolojia hiyo imeungwa mkono na shirika la WaterAid ambalo
limesema kuwa itasaidia sana katika maeneo ya miji.
Kulingana
na shirika hilo la hisani takriban watu millioni 748 hawana maji safi
ya kunywa.katika kanda ya video iliyowekwa katika blogu yake,Bwana Bill
Gates alishuhudia kinyesi cha Binaadamu kikiingizwa katika mtambo huo
kabla ya kunywa maji yaliokuwa yakitoka kutoka kwa kikombe.
''Maji
hayo ni mazuri sana ikilinganishwa na maji yoyote yale niliokunywa,na
baada ya kusomea teknolojia hii nitayanywa kila siku.Maji haya ni salama
kabisa'',aliandika katika blogu yake.Kulingana na mtengenezaji wa
mtambo huo Peter Janicki,maji taka hayo huchemshwa kabla ya mvuke wa
maji hayo kutengwa na taka ngumu.
Taka
hizo ngumu baadaye huwekwa katika moto na kutoa mvuke unaoendesha
mashine zinazotoa nguvu za umeme kwa mtambo huo na pia kwa wakazi wa
eneo hilo.Maji hayo baadaye hutiwa ndani ya mtambo wa kusafisha maji ili
kutoa maji safi ya kunywa.
''lakini
kwa nini mtu awe na wazo la kubadilisha uchafu kuwa maji ya kunywa na
umeme'',aliuliza Gates.Jibu aliloandika ni kwamba kwa sababu magonjwa
yanayosababishwa na mazingira machafu huwaua watoto 700,000 kila mwaka
na huwakinga wengine wengi dhidi ya kuathirika kiakili na kimwili.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment