Saturday, January 10, 2015

MIMBA YAMTIBUA AUNT EZEKIEL.

MAMBO si mambo! Tayari mimba ya muigizaji Aunt Ezekiel imeanza kumtibua baada ya nyota huyo kushindwa kufanya baadhi ya kazi ambazo alikuwa akizifanya mwenyewe.

Mose Iyobo akimsaidia kuvaa kiatu muigizaji maarufu Bongo, Aunt Ezekiel.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, kutokana na tumbo kuwa kubwa, Aunt kwa sasa hawezi kufunga viatu vyake, kufua, kuosha vyombo na hata akitaka kwenda toileti inabidi apewe kampani na mtu.

“Mh! Jamani Aunt hata kuinama ni mtihani sasa sijui kama ni kujidekeza au nini maana anapokuwa karibu na bebi wake ndiyo usiseme ni full kudeka anasema akiinama anaumia jamani?“Eti sasa hivi shosti wake Wema Sepetu na bebi wake Mose Iyobo ndiyo wamekuwa wakifanya kazi ya ziada kumsaidia kila kazi nyingi anazoshindwa,” kilisema chanzo hicho.

Aunt Ezekiel akiwa kwenye pozi na Mose Iyobo.

Baada ya chanzo hicho kupenyeza habari,  paparazi wetu alimsaka Aunt na kufanikiwa kumnasa kwa nyakati tofauti akiwa anasaidiwa kufungwa viatu na Wema pamoja na Iyobo.Alipoulizwa Aunt kama anashindwa kweli kufanya kazi mwenyewe au anadeka, alifunguka:

“Jamani hivi niiname nimkunje mtoto wangu bila sababu za msingi na watu wapo ambao wanaweza kunisaidia kwa nini nijiumize, acheni nisaidiwe,” alisema Aunt.Kwa upande wake, Mose ambaye inaaminika kuwa ndiye mhusika wa mimba hiyo ya Aunt alipozungumza na mwanahabari wetu, alijisifu na kusema anafurahi kuwa baba bora wa Aunt.

“Sioni tatizo kutamka, mimi ndiye mhusika mwenyewe, baba bora mimi, watakaochukia wachukie,” alisema Iyobo.Kabla ya kuanzisha uhusiano na Iyobo, Aunt aliolewa na mfanyabiashara, Sunday Demonte anayedaiwa kufungwa nchini China kwa msala wa madawa ya kulevya.



JAMAA AKIFANYIZIWA LIVE

UNGANA NAMI KATIKA FACEBOOK KWA KUBOFYA Like HAPO JUU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top