Wednesday, October 29, 2014

Northumberland, Uingereza John Cummings amesimamishwa kwa kipindi cha miezi 4kosa la kumwambia mwamuzi wa kike kuwa sehemu anayopaswa kuwapo mwanamke ni jikoni na sio katika uwanja wa mpira wa miguu.

Makamu wa Rais wa shirikisho la mpira wa miguu kaunti ya Northumberland, Uingereza John Cummings amesimamishwa kwa kipindi cha miezi 4 kwa kosa la kumwambia mwamuzi wa kike kuwa sehemu anayopaswa kuwapo mwanamke ni jikoni na sio katika uwanja wa mpira wa miguu.

Cummings amemtolea kauli hiyo mwamuzi Lucy May, kwamba hawezi kuhimili kazi ya kuwa mwamuzi, na kuongeza kuwa katika maisha yake yote hakuwahi kuona mwanamke akichezesha mpira wa miguu.

Tume huru ya uratibu wa shirikisho la mpira wa miguu imesema kuwa Cumming amekiuka kanuni za mpira wa miguu za shirikisho hilo kwa kutumia lugha ya kukashifu na ubaguzi wa kijinsia.

Makamu huyo wa rais amekiri kuwa hakuwa anamaanisha kwenye kile alichokizungumza bali ilikuwa ni utani ambao huenda May hajauchukulia hivyo, japo chama hicho kimesema nafasi ipo wazi kwa refarii huyo kukata rufaa juu ya hukumu hiyo.

Hukumu aliyopewa refa huyo inaambata na adhabu ya faini ya paundi 250 na pia adhabu ya kuhudhuria mafunzo.

Mkurugenzi wa chama cha soka Northumberland, Clive Oliver amekemea kitendo hicho na kusema mpira wa miguu unajumuisha watu wote na hakuna ubaguzi wowote unaopaswa kuvumiliwa.

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YAKE RASMI YA SIKU MBILI VIETNAM‏.


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top