Tuesday, October 28, 2014

KAMANDA NZOWA ATUMIWA PAKA 3 OFISINI KWAKE; PAKA HAO WAMZONGA YEYE TU! NA KUWAACHA WATU WENGINE.

MAAJABU! Paka watatu wenye macho mekundu walimshangaza Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa pale alipowakuta katika mlango wa ofisi yake na kumng’ang’ania miguuni.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa akiwa ofisini kwake.

Sakata hilo lilitokea wiki iliyopita wakati Kamanda Nzowa akitoka ofisini na mgeni wake aliwakuta paka hao mlangoni.Kufuatia hali hiyo, wageni na baadhi ya askari anaofanya nao kazi walionekana kushangazwa na tukio hilo huku wakijiuliza kwa nini paka hao wamzingire kamanda huyo na kuwaacha watu wengine?

Hata hivyo, baadhi ya wageni waliokwepo walihisi kuwa huenda paka hao walitumwa kishirikina na watu anaopambana nao kwa kuwakamata kutokana na kupatikana na madawa ya kulevya kwani ameweza kwa kiasi kikubwa kudhibiti biashara hiyo haramu hapa nchini.

Akizungumza na Uwazi, askari mmoja alisema Kamanda Nzowa amekuwa akipata vitisho na majaribu ya kila aina ikiwemo rushwa lakini kwa kuwa ni mcha Mungu mzuri anashinda.

Hadi wageni hao wanaondoka paka hao bado walikuwa wamemng’ang’ania kamanda huyo.
 Hata hivyo, kamanda huyo alirudi nyuma na kufunga mlango na kuwaacha paka hao wakiwa wamesimama nje ya mlango wa ofisi yake.

Mwandishi wetu alipomuuliza Nzowa kutokana na hali hiyo alisema ni mambo ya kawaida kwake na kinachomsaidia ni Mungu kwani kila mara amekuwa akisali.

BINTI ATEKWA NA WACHUNA NGOZI NA KUNUSURIKA


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHIN

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top