Monday, October 6, 2014

PICHA ZA HALIMA MDEE NA WENZAKE WALIOANDAMANA KUELEKEA IKULU NA KUISHIA MIKONONI MWA POLISI.


 Halima mdee akizozana  na polisi mara baada ya kuingizwa kwenye gari

Jana mchana taarifa za kukamatwa kwa M/kiti mpya wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) Mh Halima Mdee ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Kawe zimesambaa kila kona ya mitandao na vyombo vingine vya habari....

 Polisi  wakimpandisha Halima mdee kwenye gari la polisi leo

Wamekamatwa kwa kufanya maandamano ya Amani ya kuelekea Ikulu kumwomba Mh Rais asipokee rasimu iliyochakachuliwa...

naimani unafahamu fika jinsi rasimu hiyo imekuwa na utata na mpaka mwisho mambo mengi muhimu na ya msingi ya Kitaifa yameondolewa na wabunge wa Bunge maalumu la Katiba....

Sasa nauliza, kosa la Halima na wafuasi wake (Bawacha) ni nini? Kupeleka kilio chao kwa Rais? Je maandamano si haki ya kikatiba? Kuna nini nyuma ya huu mtindo wa polisi kupiga raia badala ya kuhakikisha usalama wa raia???

Mfuasi wa chadema akishikiliwa na polisi na kupelekwa katika gari la polisi
 
Halima Mdee akiwa ndani ya gari la polisi pamoja na wafuasi wa chadema wakipelekwa katika kituo cha polisi cha Osterbay.

Wafuasi wa chadema wakimueleza polisi madai yao wakiwa nje ya kituo cha polisi cha Osterbay wakidai kwenda kwa wanaohusika kutuoni hapo kwa ajili ya kumtoa mwenyekiti wao Halima Mndee
 
Wakina mama wa chadema wakifika katika eneo la polisi Osterbay

Viongozi wa chadema wakiomba kuruhusiwa kupita polisi ya Osterbay


ZITTO KABWE ATWAA TUZO YA MTETEZI WA HAKI YA HIFADHI YA JAMII.



HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top