Kadina amesema kuwa yeye na Wema hawana mkataba wa kulipana bali wapo kishkaji zaidi.

Martin Kadinda ambaye ni meneja wa Wema Sepetu ameibuka na kusema kuwa Wema Sepetu ambaye ni meneja wa Wema Sepetu ameibuka na kusema kuwa Wema Sepetu aliyekuwa akimwaga pesa vilivyo kwasasa hana pesa ya kumlipa bali yeye Martin anahangaika kwa issue zake binafsi ili wasilale njaa
"Kikubwa ninachofanya ni kutafuta dili za kazi nyingi ili tuweze kupeana pasu kwa pasu lakini si mshahara, nafanya kazi na bosi wangu Wema kishikaji na kwa kweli nafurahia sana utaratibu huu"
Martin alisema kuwa kama angekuwa na mkataba na Wema kumlipa kila mwezi asingemudu na kusema yupo na Wema kwasababu anajua ni mtu wa aina gani na anafanya kazi zake kwa uhuru bila kubanwa.
Wakati Wema yupo kimapenzi na yule kigogo aliyejulikana kwa jina la Clement(CK), Wema alidaiwa kumwaga pesa kila kona na wapambe kibao wa kula bata nao huku akiwa na magari kadhaa lakini kwasasa anadaiwa kushuka kiuchumi na kubaki na gari moja pekee huku wapambe aliokuwa nao wakitimua na waliobaki kulalamika hawali bata kama zamani.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment