Friday, August 29, 2014

AJALI MBAYA KABISA YAUA 10 NA KUJERUHI 7 MBALIZI MKOANI MBEYA LEO.

Daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace baada ya kuparamia lori.

Lori lenye namba za usajili T 158 CSV lililoparamiwa na daladala.

 
Askari wa usalama wa barabarani akiwa anatazama na kuchunguza zaidi ajali hiyo.




Baadhi ya majeruhi wakitolewa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea Hospitali ya Rufaa Mbeya. 
WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu kama daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace  na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa lori lililokuwa likiingia barabarani.
Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi ingawa pia walimtupia lawama dereva wa lori ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali Teule ya Ifisi, Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.

Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huku wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.
Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na wanawake wanne na wanaume wanne.
Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo dereva wa lori alitokomea mara baada ya tukio.

R.I.P All na pole sana kwa familia


HATA KUBONYEZA KA Like Tu Hapo JUU HUTAKI; BONYEZA BASI MPEDWA
PIA ISOME NA HII HAPA CHINI INAKUHUSU

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top