Monday, July 7, 2014

NJEMBA ALIYE MNASA BABA MWENYE NYUMBA NA MKE WAKE AHAMA NYUMBA.


Bw. Huruma Bernard ambaye alidai kumfumania baba mwenye nyumba wake, Lugali akihama na mkewe kutoka nyumba waliyopanga.

JAMBO limezua jambo! Yule jamaa aliyefahamika kwa jina la Huruma Bernard ambaye alidai kumfumania baba mwenye nyumba wake, Lugali akitaka kuvunja amri ya sita na mkewe, hatimaye ameamua kuhama nyumba.Fumanizi hilo liliripotiwa  wiki iliyopita  ambapo Huruma alimfumania baba mwenye nyumba huyo kwenye gesti moja iliyopo Buguruni, Dar.

Katika tukio la kuhama, Ijumaa iliyopita, wanahabari wetu walitonywa na chanzo chao kuwa Huruma alikuwa anahama katika nyumba aliyokuwa anaishi maeneo ya Ukonga, Dar baada ya kupewa notisi na baba mwenye nyumba huyo ili kuondoa fedheha ya kumfumania gesti na mkewe.

...Mke na mume walifunga virago vyote tayari kwa kuhama.

Wanahabari wetu walipofika eneo hilo walimkuta Huruma na mkewe wakibeba vitu ambapo jamaa huyo alisema kuwa amekubali kuondoka kwenye nyumba hiyo baada ya kuona hakutakuwa na maelewano tena.

...Mke na mume wakiwa nje ya nyumba waliyopanga.

“Nimekubali kuhama kwani maelewano na baba mwenye nyumba hayakuwa mazuri tena baada ya kumfumania na mke wangu,” alisema Huruma.

...Mke na mume hao wakiondoka.

Alisema kwamba mkataba wake katika nyumba hiyo ulikuwa unatakiwa umalizike Machi Mosi, mwakani lakini baada ya kumfumania wamekuwa na bifu kubwa kiasi cha kukaribia kutwangana kila wanapopishana.

Binti anayejinadi kuwa yeye ni mzuri kuliko wote tz atupia tena picha chafu ZIONA HAPA


Shauri lao bado lipo kwenye Kituo cha Polisi cha Buguruni likiwa na faili la kesi namba BUG/RB/6182/ 2014- UTEKAJI kwani baada ya fumanizi jamaa huyo alidai alitekwa


Bonyeza Like hapo juu uwe wa kwanza kupata habari mpya.

Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top