Thursday, June 12, 2014

Mtoto wa R Kelly amebadilisha jinsia kutoka kuwa mwanamke na sasa ni mwanaume.

Mtoto wa miaka 14 wa mwanamuziki mkongwe wa R&B wa nchini Marekani R Kelly ametangaza kubadilisha jinsia yake kupitia mitandao ya kijamii.

Mtoto huyo aitwaye Jaya alizaliwa mwanamke lakini akachukua uamuzi mgumu na kuwaambia mashabiki zake kuwa sasa hivi yeye ni mwanaume akiitwa Jay kwakuwa amebadilisha jinsia yake.
Lakini wakati mama yake Andrea Kelly akimuunga mkono mtoto wake kutokana na hatua hiyo, baba yake R Kelly bado hajazungumza chochote.

Jaya ambaye sasa anaitwa Jay amesema mama yake alifurahishwa sana kwa kitendo chake hicho na kusema anampenda mtoto wake vyovyote vile alivyo ambapo anamshukuru mama yake kwa kukubali yeye kubadili jinsia yake na kuwa mwanaume.



Tafadhali bofya like hapo juu kama bado hujabofya upate habari mpya haraka

Ameongeza kuwa anaamini yeye sasa ni mwanaume na anataka upasuaji zaidi na tiba ya kumsaidia kuwa vile alivyotakiwa.
Jay amesema akiwa na umri wa miaka sita alijigundua kuwa anavutiwa sana na wasichana lakini hataki mahusiano kwanza.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top