Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka alidai hayo jana mbele ya Hakimu Aloyce Katemana wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Hakimu Katemana alisema kesi hiyo itatajwa tena Julai 8 mwaka huu kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi umekamilika. Washitakiwa wataendelea kuwa nje kwa dhamana.
Hivi karibuni Rwakatare kupitia kwa Wakili wake Peter Kibatala aliomba upande wa jamhuri kumpa simu zake zilizochukuliwa alipokamatwa kwa ajili ya kukamilisha upelelezi, hata hivyo upande wa Jamhuri ulidai utawasiliana na polisi apewe simu hizo.
Rwakatare na mwenzake, Joseph wanakabiliwa na mashitaka ya kula njama ya kudhuru kwa sumu.
Wanadaiwa Desemba 28, mwaka juzi katika eneo la King’ongo wilayani Kinondoni, walikula njama ya kutumia sumu kumdhuru Dennis Msacky wakati huo akiwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment