MSANII
wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ambaye kwa sasa yuko Kenya amesema kuwa, haamini kama kweli wasanii wa filamu Recho Haule na Adam Kuambiana wamefariki dunia mpaka siku atakapoyaona makaburi yao.
Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya simu, Madaha alisema ameshitushwa na vifo hivyo na vimemfanya akose amani kutokana na namna walivyoondoka duniani ghafla.
“Nilitamani sana kuwepo lakini niko mpakani mwa Kenya na Uganda kuna ziara maalum ya kikazi naifanya.Yaani bado siamini kama kweli wamefariki, mpaka nije nione walipozikwa,” alisema Baby Madaha.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment