Saturday, May 31, 2014

JOHARI AMTUPIA CHUCHU VIJEMBE MSIBANI.


STAA wa Bongowood, Blandina Chagula ‘Johari’ anadaiwa kumtupia vijembe kiaina msanii mwenzake, Chuchu Hans ambaye ‘anabanjuka kimalovee’ na mkurugenzi mwenza wa Kampuni ya RJ, Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’.

Staa wa Bongowood, Blandina Chagula ‘Johari’.

Tukio hilo lilichukua nafasi kwenye msiba wa mwigizaji Sheila Haule ‘Recho’ Sinza-Palestina, Dar, hivi karibuni ambapo vijembe viliibuka baada Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ kumuuliza kwa lugha ya utani Chuchu kuwa RJ itachangia nini msibani hapo, Johari akadakia:

“Kampuni yangu si ya uchochoroni au ya chumbani, nina TIN namba kabisa siyo kama hiyo nyingine, iweje umuulize asiyehusika...”

Baada ya Johari kutamka maneno hayo, waombolezaji waliokuwepo msibani hapo walipigwa na butwaa na kuhoji kulikoni?

Johari amekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano na Ray kipindi cha nyuma huku kukiwa na taarifa kuwa Chuchu ana kampuni iitwayo Chura ikimaanisha Chuchu na Ray hivyo ilitafsiriwa kuwa alikuwa akiipiga kijembe kwa madai kuwa haiwezi kufikia levo za RJ.

Alipofuatwa na mwanahabari wetu ili kupata ufafanuzi juu ya ishu hiyo, Johari hakuwa tayari kwani alisema ana majonzi ya kuondokewa na kipenzi chake Recho hivyo hakutaka malumbano na watu katika kipindi hiki kigumu.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top