Wednesday, February 12, 2014

Moto mkubwa wazuka katika stoo ya chuo cha taaluma ya Polisi Moshi

Wanafunzi wa chuo cha taaluma ya polisi Moshi wakijaribu kuzima moto na kuokoa mali zilizokuwa zikiungua katika moja ya stoo ya kuhifadhia vitu mbalimbali zikiwemo nguo baada ya kuzuka kwa moto katika jengo hilo. Hakuna mtu aliyeripotiwa kudhurika na Mkuu wa Chuo hicho Kamishana Msaidizi wa Polisi Matanga Mbushi ameahidi kutoa taarifa kamili baadaye. 






Baadhi ya vitu vikiokolewa kutoka katika jengo lililowaka moto.





 Juhudi za kuondoa vifaa vilivyookolewa kabla ya kuteketea kwa moto
 Moja ya kifaa kilichopo chuoni hapo ambacho pia kilikuwa kikitumika kwa shughuli za kuzima moto katika jengo hilo .Mkuu wa chuo hicho Matanga Mbushi amesema taarifa kamili ya moto huo itatolewa baadae.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akiwa na mkuu wa Chuo cha taaluma ya Polisi kamishana msaidizi wa polisi Matanga Mbushi wakishuhudia zoezi la uzimaji moto katika jengo hilo.




Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top