Thursday, February 13, 2014

Miss Tanzania 2011, Salha Israel akiri kutembea na kibunda cha kondom kwenye pochi yake.

MISS Tanzania 2011, Salha Israel akiongea na mapaparazi wa GPL (hawapo pichani).

MISS Tanzania 2011, Salha Israel ameweka bayana bila ya woga wowote kuwa, kwenye pochi yake hakaukiwi na mipira ya kiume ‘kondom’, Amani linakupa kila kitu kinagaubaga.
Salha alisema hayo, juzi Jumanne katika mahojiano maalum, chumba cha habari cha Magazeti Pendwa Bongo, Global Publishers, Bamaga – Mwenge jijini Dar es Salaam.

HABARI KAMILI
Katika mahojiano hayo, Salha aliwekwa mtu kati ambapo alifafanua ishu hiyo pamoja na mambo mengine ndani na nje ya urembo, bila kusahau tasnia ya sinema ambayo kwa sasa ameingia kwa miguu miwili.

Swali la msingi lililozaa jibu hilo ni pale alipoulizwa kama aliwahi kutoa mimba tangu alipoanza kuelea kwenye bahari ya mapenzi, ambapo alikana kisha akafafanua: “Mimba! Weeeee.... hapana. Sijawahi kupata wala kutoa mimba.”
Akaongeza: “Mimi natumia kondom bwana, mimba itaingia wapi hapa!”
AMANI: Kama ukienda kwa jamaa na akawa hana kondom unafanyaje?
SALHA: Na kwa nini asiwe nayo? Lakini siyo tatizo sana, ndiyo maana mimi huwa nakuwa nazo kwenye pochi muda wote. Nikijua nakwenda kwa jamaa, basi zinakuwa tayari.

Sitaki kisingizio, kama atakuwa nazo fine (sawa) but (lakini) akiwa hana natoa zangu. Unajua mimi ndiye nitakayeingia kwenye matatizo ndiyo maana nakuwa makini mwenyewe.

AMANI: Kwa hiyo hata sasa hivi hapo unazo kondom kwenye pochi yako?
SALHA: (Anacheka) Hapana, hapana... kwa sasa sina na hii ni kwa sababu sina mtu muda huu ila nikiwa naye huwa siachi kuzibeba muda wote.
Share this article

0 comments:

ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA

Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko Pamoja

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top