Kikizungumza na paparazi wetu kutoka London, Uingereza, wikiendi iliyopita, chanzo hicho makini kilisema mwanaume ambaye hivi karibuni Shilole alijinadi kuwa ni bwana’ke siyo kwani huko London baadhi ya watu wanamfahamu kama mwanaume tata kijinsia.
“Yule jamaa anapenda sana kukaa na wanawake, sijawahi kumuona na wanaume wenzake, kazi kukata tu mauno na wanawake. Nilishangaa sana Shilole kusema eti ni mchumba’ke wakati hapa London (Uingereza) ni maarufu sana kwa kushiriki pati za wanawake.
WAPENZI: Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na 'mchumba wake', Ankar.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, Paparazi wetu alimtafuta Shilole ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Jamani imeniuma sana kwani nilikuwa sijui, nimeligundua hilo baada ya kuambiwa na watu, nilipigiwa simu kutoka Uingereza kwamba yule mwanaume siyo hivyo sina mpango naye tena kwa kweli,” alisema Shilole anayetamba na kideo cha Nakomaa na Jiji.
SOURCE:GPL
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment