Hapa anaonesha picha za X-Ray .
Mchungaji Mtikila alikumbwa na mkasa huo Ijumaa wiki iliyopita
baada ya kufika katika eneo hilo kwa nia ya kutaka kuwaondoa watu hao wa
familia tatu tofauti ambao wanaishi katika eneo hilo.
Kipigo hicho ambacho kimemsababishia majeraha ya
kisogoni na hata kushonwa nyuzi tatu kichwani, kuvimba usoni na maumivu
makali mwilini yalitokana na kipigo kutoka kwa familia mbili tofauti
zinazoishi katika eneo hilo ambao wanapinga kuhama.
Mtikila alisema, mara baada ya kufika eneo hilo, alikwenda
katika nyumba ya kwanza na kuwakuta walinzi ambao walikubali na
kuondoka katika eneo hilo kwani tayari notisi walikuwa nayo na walikuwa
wanatambua kuwa wanatakiwa kuondoka.Alisema baadaye walikwenda katika
nyumba ya pili ambayo anaishi mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Rubein
Sanga ambaye hata hivyo vitu vyake vingi akuwa amekwisha vihamisha.
Alisema wakiwa mbele ya nyumba hiyo gari la polisi
lilifika na wakiwa hawana hili wala lile vijana ambao anawataja kuwa ni
wa Sanga walianza kuwashambulia kwa kutumia nondo na kila aina ya
silaha za jadi.
“Walinipiga sana hadi nikapoteza fahamu na wakawa
wanasema huyo Mtikila bebeni na mumchome moto, walitaka kuniua kwani
walinikwida tai hadi ikakatika,” alisema.
Pia katika sakata hilo, Mtikila anadai kupoteza simu mbili, pesa
taslimu Sh400,000 na Dola za Marekani 2,000 na siku ya tukio na alifika
hapo akiwa ameongozana na watendaji wa Dawati la Msaada wa Kisheria
katika taasisi yake ya Liberty Fund International.
Kamanda wa Polisi Temeke, Engbert Kiondo alikiri
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wanalifanyia uchunguzi na taarifa
kamili itatolewa kesho Jumanne.
Chanzo:Mwananchi.
Chanzo:Mwananchi.
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment