Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, waziri mkuu
aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa hajawahi kutoa tamko lolote juu ya
kugombea urais mwakani lakini shutuma kwamba anautaka zimekuwa zikiibuka
kila kukicha.Hali hiyo inatafsiriwa na wengi kuwa, Lowassa ni tishio kwani wote waliowahi kumshambulia wanaambulia kutokwa jasho huku wakijibiwa hoja zao na watu wengine.
Hivi karibuni Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda aliibuka na kudai Lowassa anakivuruga chama kwa kuanza mbio za urais kabla ya muda wake.
Naye Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela aliunga mkono hoja ya Makonda na kumtupia lawama mwanachama mwenzake huyo kwamba amechapisha fulana zilizoandikwa ‘Friends of Lowassa’ (marafiki wa Lowassa), akadai hazina nia nzuri ndani ya chama hicho.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja,
Jumamosi iliyopita aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar kuwa,
Makonda na mzee Malecela wawaombe radhi viongozi wa dini kwa kudai
kwamba wanapokea mamilioni ya fedha kutoka kwa kiongozi huyo ambaye ni
Mbunge wa Monduli.
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela.
Mgeja alisema anashangaa kuona panya akimfukuza paka huku taarifa
hizo zikimpa uzito Lowassa ambaye licha ya kwamba hajawahi kutoa tamko
la kugombea urais mwaka 2015 lakini jina lake liko vinywani mwa
wanasiasa kila kukicha.Naye Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula wiki iliyopita alisema anafurahishwa kuona wanachama wake wakionesha ukomavu wa demokrasia ndani ya chama huku akiwataka wazingatie taratibu, kanuni na misingi waliyojiwekea.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.
“Tunafurahi kuona wanachama wetu wakionesha ukomavu wa demokrasia
ndani ya chama lakini tuzingatie misingi, kanuni na taratibu
tulizojiwekea kulinda chama chetu,” alisema Mangula.






0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment