Friday, January 10, 2014

DUUUU!!! Kashifa ya ngono yamkumba raisi wa Uransa François Hollande na mwanamke muigizaji.

Umemcheki vizuri huyiu sh anayedaiwa kuwa na mahusiano hayo.
Rais wa Ufaransa François Hollande, ametishia kuwachukulia hatua za kisheria wahariri wa jarida moja nchini humo lililochapisha taarifa za uvumi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mmoja muigizaji Julie Gayet.


Hollande hakukanusha madai hayo lakini alisema kuwa jarida hilo limekwenda kinyume na maadili ya vyombo vya habari kwa kuingilia maisha yake binafsi.

Jarida hilo, Closer,limechapisha picha kadhaa ambazo linasema zinathibitisha madai kuwa Hollande ana uhusiano wa karibu sana na Bi Gayet.


Bi Gayet mwenye umri wa miaka 41 ni muigizaji msifika wa vipindi vya televisheni.

Duru zinasema kuwa ufichuzi huu umetokea wakati ambapo Hollande anakabiliwa na changamoto kadhaa katika utawala wake, ikiwemo kudorora kwa uchumi jambo ambalo wananchi wanamtarajia kulishuhughulikia.

Inajulikana wazi kuwa bwana Hollande ana mpenzi mmoja tu ambaye ni mwanahabari Valérie Trierweiler.

Hollande pia aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanasiasa mwenzake wa chama cha kisosholidti, Ségolène Royal.

Mwezi Machi mwaka jana aliwasilisha malalamiko yake kwa kiongozi wa mashitaka Jijini Paris, dhidi ya wanablogu na wenye Mitandao ya kijamii kuwa wanaeneza uvumi.

Chanzo: BBC

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Moto umeteketeza bohari ya madawa.




Tutazidi kukujulisha kinachoendelea kwani waandishi wetu ndo wanaelekea eneo la tukio

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Lulu amfanyia surprise mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba


Mama wa mpenzi wa zamani wa Lulu, Steven Kanumba amefanyiwa Surprize na Elizabeth Michael yaani Lulu baada ya kumlisha keki juzi ambapo ni siku ya birth day ya mama huyo.

“Yaani mama Kanumba alikuwa hajui kuwa Lulu anajua siku yake ya kuzaliwa, Lulu akatumia nafasi hiyo kumfanyia ‘sapraizi’,” alisema rafiki wa karibu wa Lulu aliyeomba hifadhi ya jina lake.
 

Niliamua kumfurahisha kwa sababu ni siku yake ya kuzaliwa na sikufanya kwa sababu mwanaye hayupo, hata angekuwepo ningemfanyia tu.

 Hapa ni mama Kanumba Na mama Lulu nao wakilishana vipande vya keki hiyo.
source:GPL

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Msajili wa Vyama Vya siaisa atoa onyo kali kwa CHADEMA na Viongozi wake.

 
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujiepusha na vurugu na uvunjifu wa amani kinapotatua mgogoro wake na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe.

Akizungumza kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam, Jaji Mutungi alisema vitendo hivyo vinakiuka sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992.
“Ninawaasa viongozi wa Chadema na Zitto Kabwe kuwazuia wafuasi wao kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani wa aina yoyote wakati wote ambao mgogoro baina yao unaendelea,” alisema Jaji Mutungi na kuongeza.
 
“Mojawapo ya majukumu ya Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa ni kusimamia utekelezaji wa Sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 na kanuni za maadili ya vyama vya siasa ya mwaka 2007 zinazokataza vyama hivyo kuruhusu wanachama au mashabiki wake kujihusisha na vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani.”
Amewaasa pia waandishi wa habari kujiepusha kushabikia migogoro hiyo kwani ina athari kubwa katika jamii.
“Napenda pia kusisitiza kwamba ni vyema viongozi na wanachama wa vyama vya siasa waonyeshe ukomavu wa siasa kwa kushughulikia tofauti zao na migogoro baina yao kwa ustaarabu, utulivu na amani huku wakizingatia sheria zote za nchi. Hiyo ndiyo demokrasia ya kweli.”

Onyo la Msajili limekuja kutokana na vurugu zilizozuka hivi karibuni baina ya wafuasi wa Chadema na wale wa Zitto wakati wa kesi baina ya pande hizo iliyokuwa inasikilizwa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Breaking:Watu wawili wapigwa na kuchomwa moto kwa kudaiwa kuiba boda boda eneo la mlima Nyoka Mbeya; Samahani picha zinatisha


Habari zilizoyujia hivi punde zimethibitisha kutokea kwa tukio hilo maeneo ya mlima nyoka ambapo watu wenye hasira walichukua sheria mkoni kwa kuwafunga, kupiga na kisha kuwachoma moto hadi mauti yalipowakuta watu wawili kwa madai ya kuiba boda boda.

 Miili ya Marehemu ikiwa imetelekezwa katika mlima nyoka.


  
Baadhi ya mashuhuda akiwemo mwenyekiti wa Bajaji wa pili kushoto na watatu mwenye begi mgongoni mwenyekiti wa Bodaboda wakiwa eneo la tukio Mlima Nyoka


Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Thursday, January 9, 2014

Yule mdada aliyeshikwa na madawa ya kulevya juzi alidanganya kameza 61 wakati sasa katoa 72 kwa haja kubwa na anazidi kuzifurumusha.


Mwanamke aliyekamatwa juzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, anaendelea kutoa pipi za heroin kupitia njia ya haja kubwa ikiwa ni zaidi ya idadi aliyoisema mwanzoni kazimeza. Pia mdada huyo amekataa kuwataja watu waliomtuma licha ya kubanwa.

Kamishna wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey ameliambia gazeti la Mwananchi kuwa Yude dada aliyedakwa juzi“Anaendelea kutoa kete zaidi na ndiyo maana hatukuweza kusema idadi kamili ya mzigo alioumeza kwa sababu wakati mwingine wanadanganya, hawasemi ukweli kuhusu kiasi cha mzigo walioumeza, wana mbinu nyingi hawa,” alisema Godfrey.

Alisema baada ya kushikwa mtuhumiwa aliwaambia polisi kuwa amemeza pipi 61, lakini baadaye alisema amemeza pipi 40.

Hadi kufikia jana mchana alikuwa ametoa pipi 72.Mtuhumiwa huyo, alikamatwa juzi akiwa mbioni kwenda China, kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

“Hatuwapi kitu chochote cha kuwafanya wazitoe, lakini anapoendelea kukaa, akila chakula basi na zenyewe kupitia mfumo wa mwili hutoka. Ndiyo maana huyu mwanamke mpaka sasa anaendelea kuzitoa taratibu, mpaka zitakapoisha,”

Nzowa alisema endapo itatokea pipi hizo hazikufungwa vyema zinaweza kupasukia tumboni na aliyemeza kupoteza maisha na kwamba kwa mtuhumiwa jinsi anavyozitoa taratibu upo uwezekano wa kupasuka.

“Ikitokea zikapasuka tumboni mwake hatuna la kufanya kwa sababu jambo hilo lipo kama ambavyo unawasikia vijana wengi wanapoteza maisha kwa njia hiyo,” alisemma

Chanzo cha habari hii:Mwananchi.


Ushauri wa Bure pia umetolewa na waziri wa Uchukuzi kwa Vijana ambao hajaoa kuwa makini na wadada watanashati kwani ukiwaona usoni huwezi amini kuwa wanashugulika na biashara ya pipi na hivi siku za karibuni biashara hiyo imeonekata wadada wengi ndio huifanya ukilinganisha na idadi ya wakaka.
Heroin ni noma jamani achana na hiyo kitu kabisa tafuta biashara nyingine hiyo ni sawa na biashara ya mauaji kwani wengi wamepoteza maisha kwa kutumia madawa ya kulevya.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Wednesday, January 8, 2014

Licha wanaume wengi kunishobokea Sijapata mchumba bado "Ray C afunguka"


Ray C yupo single.. at least kwa muda huu.
Akiongea na Bongo5, Ray C amesema picha alizoziweka Instagram akiwa na mwanaume si maisha halisi bali alitaka ‘kuhave fun’ na mashabiki wake. Lakini amekiri kuwa usumbufu anaoupata kutoka kwa wanaume si mdogo.

“Sijapata bado mchumba nilikuwa nawachombeza fans wangu kwenye Instagram kwasababu nasumbuliwa sana.”
Kuhusu nyimbo mpya, Ray C amesema mwaka huu atarudi kwenye muziki kwa kuachia nyimbo mfululizo akianza na ‘Walimwengu Wote Wajue’utakaotoka mwezi March.
“Wapenzi wa muziki wangu wakae mkao wa kula,nyimbo zipo tayari bado kuziachia tu. Mwaka huu nitaanza na wimbo ‘Walimwengu Wote Wajue’ ambao umefanyikia chini ya C9 Records. Baada ya hapo harakati za muziki zitaendelea,” alisema Ray C.

Katika hatua nyingine, Ray C ameandika ujumbe huu kwenye Instagram: Yes am back……Ingawa wabaya wangu walitamani nisipone…Mungu alinipenda zaid…back to life ….am back Yo!!!Sty Tuned….Big Things r
coming.


Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

Tuesday, January 7, 2014

picha na matukio ya nje ya mahakama ambapo Zitto Kabwe ameshida dai lake la CHADEMA kutomjadili uanachama wake.

Wafuasi  na  wapenzi  wa  CHADEMA leo walielekeza macho ya nn kitajili katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,pale ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Jaji John Utumwa   alikuwa  akitoa  hukumu  dhidi  ya  Zitto Kabwe  na CHADEMA....


Zitto ambaye alikuwa   ni  Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, alifungua kesi katika Mahakama hiyo akipinga hatua ya Kamati Kuu ya Chama hicho  iliyokutana  tarehe  3  na  4  mwezi  huu  kujadili  hatima  ya  uanachama wake  wakati baraza kuu halijakaa na kujadili rufaa yake...

Akisoma  hukumu  ya  kesi  hiyo  baada  ya  kuiahirisha  jana, Jaji  wa mahakama  hiyo,Jaji Utamwa  ameridhia  pingamizi  lililotolewa  na  mh. Zitto Kabwe la  kutojadili  uanachama  wake na  kuitaka  kamati  kuu  ya  CHADEMA  au  chombo  kingine  chochote  kisijadili  uanachama  wake   hadi  kesi  yake  ya  msingi ( rufaa )  itakaposikilizwa  na  baraza  kuu  la  chama  hicho.

Polisi wakihakikisha wafuasi wa Zitto na wale wasiomuunga mkono hawaleti mtafaruku baada ya huku,u kusomwa.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

Hii ni message aliyoiandika zitto baada ya kesi katika twitter

habari kamili :: read more...

Sikiliza alichokisema Mwenyekiti wa Chadema Temeke aliyetekwa na kupigwa vibaya usiku wa kuamkia leo.


Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke Joseph Yona amepigwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa kwenye eneo la Ununio kwenye Magorofa ya Wasomali Kawe Dar es salaam.

Shuhuda Abdul Ally ambae ni mkuu wa nyumba zilizokaribu na alikopigwa Mwenyekiti huyu, anasema walisikia kelele za huyu mtu kupigwa saa tisa usiku na walipomsogelea walimkuta peke yake.
‘Niliomba wasiniue, wamenipiga sana… wamenichukua saa tano nyumbani kwangu Kwa Aziz Ally, wao walikua na gari kama ya Polisi lakini inaonekana sio ya polisi wakasema tunakupeleka Central, tulikua wanne na hawakuhangaika na mtu wakanichukua mimi moja kwa moja..

Ttulipopanda kwenye gari wakachukua nguo yangu wakanifunga uso, wakaanza kunipiga wakisema nisiwajibu na hawakuniambia chochote’




sikiliza audio yake hapa

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya kwenye page yetu

habari kamili :: read more...

IMF yaionya kenya kuhusu kuharakisha mpanga wa sarafu moja katika EAC

 Manager mkurugenzi wa shirika la fedha duniani IMF Christine Lagarde ameionya Kenya na washirika wake kuhusu kuharakisha mpango wa kuwa na sarafu moja katika nchi za Afrika mashariki.

Amesema lazima masuala ya msingi yajadiliwe na kufikiwa kwa makubaliano ya kwa pamoja kabla ya kucukua uamuzi wa kutengeneza sarafu hizo ambazo zitatumika katika nchi zote za jumija ya Afrika mashariki.

Amewaambia wakenya ambao ndio vinara wa uchumi kwa EAC na ndio fedha yao inathamani zaidi katika EAC kuwafahamisha wanachama wengine wa EAC juu ya mpango huo na kujadili matatizo yaliyowahi kutokea katika matifa mengine walipoamua kuwa na sarafu moja kama EURO ambayo ilipoanzishwa ilipata changamoto kubwa licha ya kutengamaa kwa sasa.

Kenya inaushawishi mkubwa katika EAC na tayari nchi tatu yaani  Uganda,Rwanda na Kenya wameanza kutengeza vitambulisho vya EAC ambapo raia wa nchi moja atasafiri hadi nchi nyingine bila ya passport ilimradi tu ana kitambulicho hicho.


habari kamili :: read more...

Monday, January 6, 2014

Mwanamke anyofolewa sikio na mumewe kisa mazungumzo ya simu.


Consolata Edward ni mke wa mtu, mkazi wa Igoma jijini Mwanza ambaye amebaki na kipisi cha sikio baada ya kunyofolewa kiungo hicho kisa kikidaiwa kuwa ni hawara yake.

Tukio hilo lilitokea Desemba 16, mwaka jana ambapo mwanamke huyo alidai kuwa alikuwa akizungumza kwa simu na mfanyakazi mwenzake ambaye anauza naye chakula maeneo ya Mlango Mmoja jijini hapa kabla ya mumewe kumvamia na kumpiga.

Kwa huzuni, Consolatha aliliambia Ijumaa Wikiend kuwa baada ya mumewe kumpiga yeye aliamua kupigana naye kisha kumchania ‘boksa’ na kusababisha viungo vyake vya uzazi kubaki wazi.
 
Alisema wakati timbwili likiendelea, ghafla alitokea mama mwenye nyumba akifuatana na mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la Hawa na kumg’ata sikio lake hadi akalinyofoa na kulitema.
  
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mume wa Consolatha aliyejitambulisha kwa jina moja la Athuman alidai kuwa siku ya tukio alimuona mkewe akiongea na simu usiku jambo ambalo halikuwa kawaida yake na alipomuuliza alikata simu na kwenda kuongelea nje ya nyumba.

Aliongeza kuwa, alimfuata nyumanyuma na kupata wasiwasi kutokana na mada zilizokuwa zikiongelewa ndipo alipomnasa kofi mkewe aliyekimbilia kumchania boksa yake.
 

Athuman alisema kuwa mama mwenye nyumba alipoona ugomvi huo unazidi ndipo alipowaita majirani walioingia wakiwa na huyo Hawa aliyedaiwa kumg’ata mkewe.
 
“Wakati mimi natafuta khanga ili nijistiri ndipo nilipoona mke wangu ameloa damu huku kipande cha sikio lake kikiwa chini kabla ya kuliwa na mbwa, sijui kwa nini Hawa aliingilia ugomvi wetu,” alisema Athuman huku kukiwa na madai Consolatha alikuwa akizungumza na mume wa Hawa.





Baadaye sakata hilo lilipelekwa kwa mwenyekiti wa mtaa na watu hao kutakiwa kuripotiwa Kituo cha Polisi cha Nyakato (Mwatex) ambapo jalada la kesi lilifunguliwa kwa NY/RB/8709/2013 KUPIGANA HADHARANI wakisubiri sheria kuchukua mkondo wake.
Chanzo: Ijumaa Wikiend/ GPL 
 
 

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya

habari kamili :: read more...

Sunday, January 5, 2014

Jose Chameleone na mdogo wake Weasel wamaliza tofauti zao.



Kwa muda mrefu Chameleone na mdogo wake Weasel walikuwa hawaelewani wala kuzungumza. Habari njema ni kuwa mwaka mpya 2014 umekuja na baraka zake ambapo mafahari hao waliamua kuweka tofauti zao pembeni kwenye show ya ‘UG Dance Mix End of Year Party’ iliyofanyika kwenye hoteli ya Sheraton jijini Kampala.


Unaikumbuka beat ya wimbo wa Profesa Jay ‘Nikusaidiaje’ aliomshirikisha Ferooz? Ni beat kali iliyopigwa na Godfather wa Bongo Flava, P-Funk Majani aka Kinywele Kimoja. Beat hiyo ilitumiwa tena miaka saba ijayo na ndugu wa Uganda, Jose Chameleone na Weasel katika wimbo wao uliohit, Bomboklat.

Baada ya kundi la Goodlfye linaloundwa na Radio na Weasel kutumbuiza,  Chameleone alipanda jukwaani akiwa amevalia nguo nyeupe. Aliimba huku fataki zikipigwa hewani kuukaribisha mwaka 2014.
 
 Kisha alisimama na kuwaambia mashabiki amewaandalia surprise ya mwaka.
Chameleone na Weasel wakatumbuiza kwa pamoja wimbo wao, Bomboklat na kuufanya umati uliokuwa ukishuhudia ukulipuka kwa shangwe.

Baadaye Chameleone alimuita Radio na watatu hao wakaahidi kuyaacha yaliyopita ili wagange yajayo.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya

habari kamili :: read more...

Sababu za Penny kuachana na Diamond hizi hapa.


Penny  ambaye  ni mpenzi  wa  zamani  wa  Naseeb Abdul "Diamond"   haonekani  kujutia  kitendo  cha  kumwagana    na  msanii  huyo  na  badala  yake  sasa  ameanza  kuzipa  uzito  hoja  za  kumpiga  chini  Diamond  ambaye  walidumu  naye  kimapenzi  kwa  takribani  mwaka  mmoja.

Kwa mujibu wa watu wa karibu  na  Penny, kitendo  cha  Diamond  kumpandisha  jukwaani  Wema  Sepetu  pale Leaders  Club  kilipata  kila  aina  ya  laana  toka  kwa  mama  mzazi  wa  Diamond  kwani  hakuridhia  jambo  hilo.

"Mama  alilalamika  sana  kuhusu  Diamond  kumpandisha  Wema  pale  leaders  Club, kimsingi  ni  kwamba  hataki  kabisa  uhusiano  kati  ya  Diamond  na  Wema  Sepetu"...Kilisema  chanzo  kimoja ambacho  ni  rafiki  damu  na  familia  hiyo.

Wakati hayo  yakijitokeza  ndani ya familia ya Diamond, kwa upande wa Wema, mama  yake  pia  anadaiwa  kulalamikia  kitendo  cha  mwanaye  kutumika  kila  mara  kumbusti  Diamond  pale  umaarufu  wake  unaposhuka!

"Mama  Wema  naye  analalamika  mwanaye  kutumika  kama  daraja  la  kuwavusha  watu  kwenye  umaarufu  halafu  wakishafanikiwa  wanamgeuka  na  kumdhalilisha, kifupi  ni  kwamba  hataki  kabisa  kusikia  mahusiano  ya  Wema  na  Diamond"  Kilifunguka  chanzo  hicho.

Aidha  imeelezwa  kuwa  Diamond  amekuwa  akimpigia  simu  Penny  mara  kwa  mara  kumuomba  wayamalize  lakini  Penny amekuwa  akimjibu  kwa  kifupi  kuwa  "Nimekuachia  Wema  Wako"

Penny  amekuwa  akijisifu  kuachana  na  Diamond  kwa  hoja  kuu  tatu:
1: Kuondokana  na  skendo  zisizo  na  faida  kwake.
2: Kupunguza  malalamiko  toka  kwa  familia  yake.
3: Penny  aliingia  katika  mahusiano  na  Diamond  si  kwa  ajili  ya  mapenzi, bali  kulipa  kisasi kwa  Wema  ambaye  aliwahi  kumchukulia  mpenzi  wake.

"Hata  kutoa  mimba  ya  Diamond  amekuwa  akisema  kwamba  kama  angezaa  naye  watoto  wake  wangekuwa  na  sura  mbaya  na  midomo  ya  ajabu".Kilimalizia  chanzo  hicho .

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya

habari kamili :: read more...

Saturday, January 4, 2014

Mapokezi ya mwili wa aliyekuwa waziri wa fedha Dk.William Mgimwa yalivyokuwa,na Ratiba ya Mazishi.

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk.William Mgimwa umewasili nchi hii leo kwa ndege ya shirika la Kenya (KQ) na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue pamoja na Mawaziri mbalimbali na Wabunge.



Mjane Mama Jane Mgimwa(katikati) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini Radhia Msuya(kulia) mara baada ya kuwasili kutoka nchini Afrika kusini.




Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wabunge waliojitokeza kuupokea mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Dkt. Willium Mgimwa.




Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (wa kwanza Kushoto)akisalimiana na baadhi wa Watu waliofika kuupokea Mwili wa wa aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. Willium Mgimwa Leo Jijini Dar es Salaam.

TAREHE 4/ 01/ 2013

    MWILI WA MAREHEMU UNATARAJIA KUWASILI UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE TERMINAL II, SAA7: 00 MCHANA. BAADA YA KUWASILI UTAPELEKWA NYUMBANI KWA MAREHEMU MIKOCHENI B.
    SAA 11:00 JIONI MWILI UTAPELEKWA HOSPITALI YA LUGALO.

TAREHE 5/ 01/ 2013

    SAA 3:00 HADI SAA 4:00 ASUBUHI:- CHAKULA NYUMBANI KWA MAREHEMU.
    SAA 4:30 ASUBUHI :- MWILI KUWASILI NYUMBANI MIKOCHENI B.
    SAA 5:30 HADI SAA 8:00 MWILI UTAPELEKWA UKUMBI WA KARIMJEE KWA AJILI YA SHUGHULI ZA IBADA NA HESHIMA ZA MWISHO.
    SAA 8:10 MWILI UTAPELEKWA UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU NYERERE TERMINAL I.
    SAA 10:00 MWILI UNATARAJIA KUWASILI IRINGA UWANJA WA NDULI  NA KUAGWA KATIKA UKUMBI WA SIASA NI KILIMO-IRINGA
    SAA 11:30 JIONI MWILI UTASAFIRISHWA KUELEKEA KIJIJI  CHA MAGUNGA.

TAREHE 6/ 01/ 2013 



    SAA 6:00 MCHANA SHUGHULI ZA MAZISHI KIJIJINI KWA MAREHEMU MAGUNGA. 

MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI;

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya

habari kamili :: read more...

Padre akubali kulipa 580,000/= kama gharama ya matunzo ya mtoto; Je Kanisa litachukua hatua gani?


Kesi iliyokuwa ikimkabili Padri Deogratius Makuri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida kushindwa kutoa fedha za matunzo kwa mwanawe, jana ilifikia ukingoni baada ya mlalamikiwa kuamua kulipa jumla ya Sh 580,000 taslimu ikiwa ni gharama za matunzo, matibabu na mavazi kwa ajili ya mtoto huyo.


Padri Makuri, ambaye alikuwa Katibu wa Askofu Jimbo Katoliki Singida alituhumiwa kushindwa kutunza mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minane (jina limehifadhiwa) aliyezaa na Maria Boniphace (26), mkazi wa eneo la Mitunduruni mjini Singida ambaye anadai alikuwa mfanyakazi jimboni hapo.

Kiasi hicho cha fedha kilikabidhiwa kwa mlalamikaji Maria Boniphace na dadake Padre ajulikanaye kwa jina la Bahati Michael mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Utemini mjini Singida, Ferdinand Njau.

Awali Hakimu Njau aliionesha  barua kutoka kwa Padri Makuri ambapo alisema hawezi kufika mahakamani hapo kutokana na kile alichodai ni sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake.

Kati ya fedha aliyoleta mahakamani hapo, alisema kuwa Sh 480,000 ni matunzo kwa miezi sita kuanzia Des 10, 2013 hadi Juni 10, 2014 ikiwa ni Sh 80,000 kila mwezi ambapo Sh 100,000 ni kwa ajili ya matibabu na gharama ya mavazi kwa mtoto huyo.

Hakimu Njau amemtaka mlalamikiwa kuleta kiasi hicho hicho tena hapo ifikapo Juni 10, mwaka huu vinginevyo kesi itafufuliwa. “Ilichokuwa inataka Mahakama hii ni fedha za matunzo kwa mtoto huyu, basi .... hilo sasa limefanyika.

"Sioni sababu ya kuendelea na shauri hili labda hapo mlalamikiwa atakaposhindwa kuheshimu amri ya Mahakama.” alisema Hakimu Njau aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo.

Sasa kesi imeisha je Kanisa Katoliki litachukua hatua gani na hii inaleta picha gani kwa waumini wa kanisa katoliki????????????????????

 

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya

habari kamili :: read more...

Usichezee nguvu ya umma:Tazama kijana akishushiwa kichapo baada ya kupingana na wenzake kuhusu hoja ya Zito.

 Katika mjadala uliokuwa ukiendelea nje ya mahakama kuu jijin Dar es Salaam baada ya kesi ya Zuberi Zito Kabwe kuhairshwa; makundi mawili yalipingana kati ya linalomuunga mkono Zito na lisilomuunga mkono.
Katika hali hiyo ndipo kijana mmoja wa kundi lisilomuunga Zito akajikuta akipewa za fasta na njemba moja lenye halijali polisi kwani walikuwa karibu kabisa na eneo la mabishano.

 Hatua hiyo ilisababisha Askari wa Jeshi la Polisi kuingilia kati, huku wakiungana na upande wa Chadema na kuwatwanga marungu wafuasi wa Zitto waliokuwa na mabango kama ilivyokuwa kwa wenzao wa Chadema.



Kesi hiyo ilifunguliwa jana na wakili wa Mbunge huyo Albert Msando huku wakili wa Chadema Tundu Lissu akiweka pingamizi,hata hivyo Jaji John Utumwa wa Mahakama hiyo alitupilia mbali mapingamizi yote yaliyowekwa na Tundu Lissu.

Kesi imehairishwa hadi Jumatatu saa 4:00 asubuhi.

Jaji John Utumwa alisitisha kutoa hukumu hiyo mpaka siku ya Jumatatu saa 4:00 asubuhi.Hata hiyo baada ya Jaji huyo kuahirisha kesi hiyo, nje ya Mahakama hiyo kulikuwa na vurugu kubwa baada ya kundi linalo unga mkono maamuzi ya Chadema kutwangana na kundi linalo muunga Zitto Kabwe.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya

habari kamili :: read more...

Friday, January 3, 2014

Wanakwaya wa RC Arusha walipukiwa na kitu kinachozaniwa kuwa ni bomu mkesha wa mwaka mpya.


 
Wanakwaya kadhaa wa kanisa katoliki la Mt Kalory maeneo ya USA River mkoani arusha wamelipukiwa na kitu kinachozaniwa kuwa ni bomu na wamelazwa katika hospitali ya Misheni ya Tengeru.
Sita kati yao ni majeruhi na mmoja hali yake ni mbaya.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas amezungumza na  na waandishi wa habari, akithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kulifuatilia kufaham chanzo cha tukio hilo.

"Taarifa nimezipata lakini uchunguzi unaendelea kujua chanzo na muhusika sambamba na ukweli wa mlipuko huo ili kujua kama kweli ni bom na ni la aina gani".
 

Wakizungumza na mtandao huu, kwa nyakati tofauti katika hospitali ya Tengeru iliyopo wilayani Arumeru, baadhi ya majeruhi wa tukio hilo walisema kuwa siku ya mkesha wa kuupokea mwaka 2014 walipokuwa wakitoka kanisani (Kanisa katoliki parokia ya USA river) waliweza kusikia mlio mkubwa wa kitu kama bom la kurusha ndipo baadhi yao walioangukiwa na bom hilo kuweza kujeruhiwa vibaya na kuanguka chini huku wakivuja dam nyingi sehem mbalimbali za mwili.

Kwa upande wake Askofu mkuu wa kanisa la katoliki jimbo kuu la Arusha, Josephat Lobulu akizungumzia tukio hilo alisema kuwa ni tukio la kulaaniwa, hivyo ameliomba jeshi la polisi kushughulikia jambo hilo.



Alisema kuwa amesikitishwa na tukio hilo, lakini yeye kama mtumishi wa Mungu anapaswa kuwaombea wote walioathrika na tukio hil ikizingatiwa wamepatwa na tukio hilo mita chache tu kutoka katika nyumba ya Mungu (Kanisani).

Tutazidi kukujuza repoti kutoka polisi ikitolewa.

Tafadhali bofya like kama bado hujabofya

habari kamili :: read more...

Thursday, January 2, 2014

Madee amjibu Diamond kwa kumzawadia meneja wake gari aina ya BB New Model siku ya Birthday day yake.

usiku wa kuamkia tarehe 1 – 2014 ilikuwa ni Birth day ya Babu Tale ambaye ni meneja wa kundi la Tip Top connection lenye masikani yake pale manzese dar.

habari kamili :: read more...

Wednesday, January 1, 2014

Basi la TAQWA lapatapa ajali mbaya Mikumi Morogoro.Wawili wathibitishwa kufa.

Basi la Taqwa limepata ajali maeneo ya Mikumi mkoani Morogoro wakati likitaka Kuovertake Lorry Lililokuwa limebeba mbao.

Baadhi ya majeruhi wanasema madereva wawili wa basi hilo walilala na kumwachia msimamizi wao aendeshe ndipo alijaribu kulipita lorry lililobeba Mbao kushindikana baada ya mwendo wa basi hilo ambalo ni Nissan Dizel kuzidiwa na mwendo wa lorry hilo aina ya Scania.

habari kamili :: read more...

Waziri wa Fedha, Dk. William A. Mgimwa (63) amefariki dunia nchini A.Kusini baada ya maradhi ya mda mrefu.


Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa waziri wa fedha amefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikolazwa kwa maradhi yaliyomsumbua mda mrefu.

Mgimwa aliyezaliwa January 20, 1950 alikuwa amelazwa katika hospitali ya Milpark ambayo pia Dk. Sengondo Mvungi. alilazwa kwani hospitali hiyo inaumaarufu wa kusaidia kuwatibu watanzania.

habari kamili :: read more...
 
Copyright © 2014 Chopa News • All Rights Reserved.
| Template Design by Anga Zio Team • Powered by Blogger online
back to top