Manager mkurugenzi wa shirika la fedha duniani IMF Christine Lagarde ameionya Kenya na washirika wake kuhusu kuharakisha mpango wa kuwa na sarafu moja katika nchi za Afrika mashariki.
Amesema lazima masuala ya msingi yajadiliwe na kufikiwa kwa makubaliano ya kwa pamoja kabla ya kucukua uamuzi wa kutengeneza sarafu hizo ambazo zitatumika katika nchi zote za jumija ya Afrika mashariki.
Amewaambia wakenya ambao ndio vinara wa uchumi kwa EAC na ndio fedha yao inathamani zaidi katika EAC kuwafahamisha wanachama wengine wa EAC juu ya mpango huo na kujadili matatizo yaliyowahi kutokea katika matifa mengine walipoamua kuwa na sarafu moja kama EURO ambayo ilipoanzishwa ilipata changamoto kubwa licha ya kutengamaa kwa sasa.
Kenya inaushawishi mkubwa katika EAC na tayari nchi tatu yaani Uganda,Rwanda na Kenya wameanza kutengeza vitambulisho vya EAC ambapo raia wa nchi moja atasafiri hadi nchi nyingine bila ya passport ilimradi tu ana kitambulicho hicho.
Tuesday, January 7, 2014
Browse » Home » » IMF yaionya kenya kuhusu kuharakisha mpanga wa sarafu moja katika EAC
IMF yaionya kenya kuhusu kuharakisha mpanga wa sarafu moja katika EAC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment