Consolata Edward ni mke wa mtu, mkazi wa Igoma jijini Mwanza ambaye
amebaki na kipisi cha sikio baada ya kunyofolewa kiungo hicho kisa
kikidaiwa kuwa ni hawara yake.
Tukio hilo lilitokea Desemba 16, mwaka jana ambapo mwanamke huyo
alidai kuwa alikuwa akizungumza kwa simu na mfanyakazi mwenzake ambaye
anauza naye chakula maeneo ya Mlango Mmoja jijini hapa kabla ya mumewe
kumvamia na kumpiga.
Kwa huzuni, Consolatha aliliambia Ijumaa Wikiend kuwa baada ya
mumewe kumpiga yeye aliamua kupigana naye kisha kumchania ‘boksa’ na
kusababisha viungo vyake vya uzazi kubaki wazi.
Alisema wakati
timbwili likiendelea, ghafla alitokea mama mwenye nyumba akifuatana na
mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la Hawa na kumg’ata sikio lake hadi
akalinyofoa na kulitema.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mume wa Consolatha aliyejitambulisha
kwa jina moja la Athuman alidai kuwa siku ya tukio alimuona mkewe
akiongea na simu usiku jambo ambalo halikuwa kawaida yake na
alipomuuliza alikata simu na kwenda kuongelea nje ya nyumba.
Aliongeza kuwa, alimfuata nyumanyuma na kupata wasiwasi kutokana na
mada zilizokuwa zikiongelewa ndipo alipomnasa kofi mkewe aliyekimbilia
kumchania boksa yake.
Athuman alisema kuwa mama mwenye nyumba
alipoona ugomvi huo unazidi ndipo alipowaita majirani walioingia wakiwa
na huyo Hawa aliyedaiwa kumg’ata mkewe.
“Wakati mimi natafuta khanga ili nijistiri ndipo nilipoona mke wangu
ameloa damu huku kipande cha sikio lake kikiwa chini kabla ya kuliwa na
mbwa, sijui kwa nini Hawa aliingilia ugomvi wetu,” alisema Athuman huku
kukiwa na madai Consolatha alikuwa akizungumza na mume wa Hawa.

Baadaye sakata hilo lilipelekwa kwa mwenyekiti wa mtaa na watu hao
kutakiwa kuripotiwa Kituo cha Polisi cha Nyakato (Mwatex) ambapo jalada
la kesi lilifunguliwa kwa NY/RB/8709/2013 KUPIGANA HADHARANI wakisubiri
sheria kuchukua mkondo wake.
Chanzo: Ijumaa Wikiend/ GPL
0 comments:
ASANTE KWA KUTEMBEA BLOGU YAKO::KARIBU SANA
Toa Mani yako Hapa usiogope Tuko PamojaPost a Comment